Historia ya Issa Kitenge

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
Issa Kitenge ni mmoja kati ya washairi wakubwa Tanzania lakini asiejulikana sana katika jamii ya washairi wengi.
Alizaliwa kunako mwaka 1929 katika mji wa Kigoma na baba yake alikuwa akijulikana kwa jina la Kitenge Bin Fedha ambae alitokea katika nchi ya Congo Zaire.
Mwaka 1935 Kitenge aliaza shule ya katika shule ya msingi ya Bangwe primary hadi mwaka 1938 kabla ya kuhamia katika mkoa wa Dar es salaam ambapo alisoma pia katika shule ya serikali.
Kabla ya Uhuru Issa Kitenge alikuwa ni Kiongozi wa TANU na baadae mwaka 1977 hadi 1981 alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.
Alianza kupenda kujisomea mashairi tangu mwaka 1939 na mwaka 1941 alianza rasmi kuandika mashairi.
Baada ya vita vya Kagera vya mwaka 1978 hadi 1979,Issa Kitenge alipata tunzo baada ya kuandika shairi lake liitwalo "utenzi wa Idd Amino"
Zipo kazi zake kadhaa ambazo bado hazichapishwa:
1.Mwanzo wa ziwa Tanganyika na mazingira yake (utenzi)
2.Historia ya ziwa Tanganyika (utenzi).
Chanzo-HISTORY OF KISWAHILI POETRY, A.D. 1000-2000By M.M Mulokozi na T.S.Y Sengo.
©Kwa mwenye taarifa zaidi kuhusu Issa Kitenge awasiliane nami kwa simu namba +255624010160
Ama barua Pepe ya iddyallyninga@gmail.com
 

Attachments

  • IMG_20190224_000048.jpg
    IMG_20190224_000048.jpg
    12.7 KB · Views: 36

Similar Discussions

Back
Top Bottom