Historia ya baada ya Uhuru Tanzania iko vipi?

Jamani ina maana matukio mengi yanahusiana na siasa tu? hawa watoto wetu tutawaonyesha nini five years from now?? Yaani nimejaribu hata ku-google some national memento, na calendar nk kweli tuna hali ngumu

Maana tumeanza na kubomoa historical buildings yaani ndio tunamaliza kabisa histoiry

BTW (sorry off point though), kuna yale makaburi mawili barabara ya kutoka inringa kwenye mafinga yako upande wa kulia ambapo hata tanesco wameyapisha wanasema umeme hauwaki wakipitisha juu yake... ni ya nani?? ile ni baadhi ya ingredients za history kama tutaestablish ukweli wake... Halafu kuna ule mlima ****** ukiwa unatoka arush kwenda namanga (kabla hujafika monduli)

Timu ya taifa kucheza mechi ya kimataifa dhidi ya Timu ya taifa ya Sudan bila jezi wakati mgeni wa heshima ni baba wa taifa. Timu kupigana uwanjani mbele ya Mwalimu Nyerere na toka siku hiyo hakuangalia tena mechi ya mpira live.
 
The only country in the world ambayo haina new City na Old City. Nchi zingine zinakuwa proud na historia yao. Jamani CBD ya Dar ya enzi hizo inakwisha polepole architecture ya kiarabu inatoweka, ya kijerumani, kiingereza na kihindi haipo ni nyundo kwenda mbele na kuweka vioo.

Inatia uchungu sana, tumeshamaliza kubomoa old Dar ndio wanasema twende kigamboni... pace haipo, ni vita tu vya ten percent!!!

Mie sijui tunaenda wapi lakini labda with EAF tutaandika upya history!!!

Kuhusu watu na matukio nadhani hata lile la rais kupigwa mwereka pale mwanza na la kuanguka jangwani (2005) ni ya maana

Pia tunaweza kusema rais huyu ni wa kwanza kusafifi mara nyingi zaidi katika historia yetu, na hata pia ni rais wa kwanza dakitari wake kuja kutetea afya yake hadharani
 
Zakumi acha kutupotezea malengo. Tunajua hizo ni jitihada za Uliberali Mamboleo za kutuambia kuwa hatuna Historia. Hizi jitihada zilianza toka enzi za Hegel aliyesema tuko nje ya Historia. Ni jitihada ambazo zinatufanya tujione hatujafanya lolote na hivyo kutufanya tujisikie kutofanya lolote. Lazima tukemee jitihada hizi za kihaini!

Veracity sasa turudi kwenye mada yetu. Mimi naanza kuweka nyama na mchuzi kuanzia ule mwaka wa 1990 baada ya Mabeberu kulivamia Jiji lenye Historia ya Kale, yaani Baghdadi ya kina Alfu Ulela Ulela. Mara baada ya kujiunga na Sekondari ya Serikali nilijikuta natumia muda mwingi kupiga soga maana hakukuwa na walimu wa kutosha. Miaka hiyo ya mwanzo ya Tisini ilishuhudia migomo mingi ya walimu iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Peter Mashanga. Serikali ilitelekeza Elimu pamoja na huduma zingine muhimu kama Afya na Maji kwa mujibu wa Sera za IMF na WB!

Pia hiyo ndiyo miaka ambayo mradi maarufu wa mabasi ya wanafunzi ulianzishwa hapa Jijini Dar es Salaam. Wanafunzi tuliufurahia maana ulipunguza adha ya usafiri na kutusaidia tujuane kwa undani na wanafunzi wenzetu hasa wa zile shule za Zanaki na Jangwani. Ila lahaula mabasi hayo yakapotea. Sikujua nini kimetokea mpaka majuzi niliposoma historia ya mradi huo ambao uliishia katika mifuko yenye matobo ya kifisadi! Basi tukarudi tena katika kashikashi na makondakta!

Wakati hayo yote yanatokea kumbe wenzetu walishakutana huko Zanzibar na kulizika rasmi Azimio la Arusha ambalo Seti Benjamin Mpinga alilifia!Basi rasilimali zetu zikaanza kuibwa kama pipi. Waziri akakamatwa Uwanja wa Ndege akitorosha mzigo! Viongozi wetu wakaenda Rio Janeiro mwaka 1992 kwenye Mkutano wa Mazingira na Hali ya Hewa, wakatafuna we hela zetu huko badala ya kutembelea Favela na kujifunza kuhusu hatari ya Latin Americanization of Africa!

Itaendelea...
 
Asante Companero kwa kutukumbusha matukio muhimu kama haya ya Mabasi ya wanafunzi - mradi uliokufa kifo cha ghafla na hakuna hata daktari aliyeweza kufanya post mortem kujua chanjo cha kifo.Wenye kujua hebu mwageni ukweli.
Nani ana habari zaidi kuhusu "mapinduzi ya kitamaduni " ya miaka ya 70 ambapo serikali ilipiga marufuku mitindo ya mavazi na nywele ya kimagharibi - kuvaa nguo fupi, kuvaa mawigi, kunyoa nywele kwa akina kaka, kutokuvaa suruali za kubana,- hii nayo ni historia inayofaa kuandikwa maana ukiangalia hali ilivyo sasa ni kinyume kabisa. Watu sasa wanatembea nusu uchi, vitovu viko nje, maungo mengine nayo nje nje- kuna suruali za mlegezo kata K. kwa akina kaka... mawigi yanavaliwa kwa sana....wanaume wanavaa hereni bila woga, nguo za kubana ndio usiseme....
NANI anakumbuka enzi za miezi 18 ya shida baada ya vita ya Iddi amin ambapo hali ilikuwa mbaya sana kiasi cha watu kukosa huduma muhimu kama unga, sabuni, sukari - waatu walipanga foleni kila mahali hasa maduka ya RTC - na hapa rushwa ilishamiri maana unapokuwa na shortage ndio hivyo tena.
Je, enzi za kamatakamata na kupeleka watu Gezaulole wakati wa sheria ya nguvu kazi?..... tunayo historia tajiri sana kama tutaweza kuyaandika kwa lugha rahisi/nyepesi na kujaribu pia kutambua busara iliyokuwepo nyuma ya matukio hayo na kujaribu kuweka urari bila kuwa too critical au kuongeza chumvi sana au kupamba na kutetea wahusika walioweka sera au kutekeleza.Hii itafanya watu wa kila aina - wasomi na wasio wasomi kujua historia ya nchi yao. Wenye kutaka kujua katika level za juu basi wanaweza kutafuta maandishi ya akina profesa Shivji, Kimambo na Temu.
 
Inatia uchungu sana, tumeshamaliza kubomoa old Dar ndio wanasema twende kigamboni... pace haipo, ni vita tu vya ten percent!!!

Mie sijui tunaenda wapi lakini labda with EAF tutaandika upya history!!!

MTM
Huenda EAF ni fursa ila tuwe mbele kufanya yatupasayo.
Ni sisi wenyewe tutakaokaa kiti cha dereva na kuendesha gari letu kuelekea kule tunakotaka.Tukiendeshwa tutarajie kupelekwa kwingine tusikotaka.
 
Naam Veracity, nilikutana na wageni (expatriate) waliofanya kazi miaka hiyo. Wanasema Serikaliya Mwalimu ilipiga marufuku kutembea na magari hovyo maana gharama za kuingiza petroli nchini zilikuwa juu sana. Natamani Serikali yetu leo ingepiga marufuku kutembelea Mashangingi hovyo. Sielewi kwa nini Mashangingi mengi yaongozane Uwanja wa Ndege kwa kodi zetu eti kumuaga au kumlaki Kiongozi fulani!
 
Signature yako imebeba ujumbe mzito sana unaendana sawia na mada yetu.
Kuhusu kupiga marufuku mashangingi... ninachoona mimi miaka ya nyuma kulikua na nidhamu, woga na pia vyote kwa pamoja ( nidhamu ya woga).Sasa hivi hakuna hata kimoja.Hakuna mtu anaogopa kitu.Viongozi wamekuwa wamimi sana, wananchi nao wamejikatia tamaa.Kumbuka PM alisahasema kuhusu mashangingi. NANI ALIMSIKILIZA?
 
MTM
Huenda EAF ni fursa ila tuwe mbele kufanya yatupasayo.
Ni sisi wenyewe tutakaokaa kiti cha dereva na kuendesha gari letu kuelekea kule tunakotaka.Tukiendeshwa tutarajie kupelekwa kwingine tusikotaka.

Mkuu roho yangu iko juu aisee kila nikiangalia mwelekeo, historia fupi ya decades kadhaa na jinsi EAF inavyoweza kuwa mnara wa babeli, umeshawahi kuangalia fungulia mbwa uwanja wa taifa jinsi watu wanavyowahi hovyo?? then that is the coming EAF...

Ili kuweka ladha kwenye hii discussion, we can even compare with our neighbours and you will agree with me we dont have much to offer in terms of continuity of culture and generations norms in Tanzania

Lets wait and see
 
Zakumi acha kutupotezea malengo. Tunajua hizo ni jitihada za Uliberali Mamboleo za kutuambia kuwa hatuna Historia. Hizi jitihada zilianza toka enzi za Hegel aliyesema tuko nje ya Historia. Ni jitihada ambazo zinatufanya tujione hatujafanya lolote na hivyo kutufanya tujisikie kutofanya lolote. Lazima tukemee jitihada hizi za kihaini!

Veracity sasa turudi kwenye mada yetu. Mimi naanza kuweka nyama na mchuzi kuanzia ule mwaka wa 1990 baada ya Mabeberu kulivamia Jiji lenye Historia ya Kale, yaani Baghdadi ya kina Alfu Ulela Ulela. Mara baada ya kujiunga na Sekondari ya Serikali nilijikuta natumia muda mwingi kupiga soga maana hakukuwa na walimu wa kutosha. Miaka hiyo ya mwanzo ya Tisini ilishuhudia migomo mingi ya walimu iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Peter Mashanga. Serikali ilitelekeza Elimu pamoja na huduma zingine muhimu kama Afya na Maji kwa mujibu wa Sera za IMF na WB!

Pia hiyo ndiyo miaka ambayo mradi maarufu wa mabasi ya wanafunzi ulianzishwa hapa Jijini Dar es Salaam. Wanafunzi tuliufurahia maana ulipunguza adha ya usafiri na kutusaidia tujuane kwa undani na wanafunzi wenzetu hasa wa zile shule za Zanaki na Jangwani. Ila lahaula mabasi hayo yakapotea. Sikujua nini kimetokea mpaka majuzi niliposoma historia ya mradi huo ambao uliishia katika mifuko yenye matobo ya kifisadi! Basi tukarudi tena katika kashikashi na makondakta!

Wakati hayo yote yanatokea kumbe wenzetu walishakutana huko Zanzibar na kulizika rasmi Azimio la Arusha ambalo Seti Benjamin Mpinga alilifia!Basi rasilimali zetu zikaanza kuibwa kama pipi. Waziri akakamatwa Uwanja wa Ndege akitorosha mzigo! Viongozi wetu wakaenda Rio Janeiro mwaka 1992 kwenye Mkutano wa Mazingira na Hali ya Hewa, wakatafuna we hela zetu huko badala ya kutembelea Favela na kujifunza kuhusu hatari ya Latin Americanization of Africa!

Itaendelea...

You see Sir, we look at things from different point of views. Mimi naangalia vitu vilivyo-trigger events. Lakini wewe siku zote unaangalia matukio yenyewe.

Miaka ya 70, we did a very terrible job. Na kama tungefanya vizuri kipindi kile, historia ya sasa hivi ingeandikwa vingine.

Tatizo lako unafikiri mimi namchukia Nyerere. Lakini hata mimi ningekuwa madarakani katika kipindi kile, ningefanya makosa tena makubwa.

Kizazi cha sasa kinatakiwa kutorudi makosa yaliopita. Na huwezi kutorudia makosa kama una-glorify failures.
 
9534_179942535338_747855338_4355325_7952301_n.jpg

Toka tupate Uhuru mpaka leo uwezo wetu wa kujenga mashule mazuri mazuri ndo umeishia hapa.
 
I am getting excited with this thread,companero and team please keep on updating we the mwinyi generation we know very little about nyerere era,witnessing bad shamfully moments with Kikwete,please can i get some history which i can be proud of?
 
Companero said:
Veracity sasa turudi kwenye mada yetu. Mimi naanza kuweka nyama na mchuzi kuanzia ule mwaka wa 1990 baada ya Mabeberu kulivamia Jiji lenye Historia ya Kale, yaani Baghdadi ya kina Alfu Ulela Ulela. Mara baada ya kujiunga na Sekondari ya Serikali nilijikuta natumia muda mwingi kupiga soga maana hakukuwa na walimu wa kutosha. Miaka hiyo ya mwanzo ya Tisini ilishuhudia migomo mingi ya walimu iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Peter Mashanga. Serikali ilitelekeza Elimu pamoja na huduma zingine muhimu kama Afya na Maji kwa mujibu wa Sera za IMF na WB!

Pia hiyo ndiyo miaka ambayo mradi maarufu wa mabasi ya wanafunzi ulianzishwa hapa Jijini Dar es Salaam. Wanafunzi tuliufurahia maana ulipunguza adha ya usafiri na kutusaidia tujuane kwa undani na wanafunzi wenzetu hasa wa zile shule za Zanaki na Jangwani. Ila lahaula mabasi hayo yakapotea. Sikujua nini kimetokea mpaka majuzi niliposoma historia ya mradi huo ambao uliishia katika mifuko yenye matobo ya kifisadi! Basi tukarudi tena katika kashikashi na makondakta!

Wakati hayo yote yanatokea kumbe wenzetu walishakutana huko Zanzibar na kulizika rasmi Azimio la Arusha ambalo Seti Benjamin Mpinga alilifia!Basi rasilimali zetu zikaanza kuibwa kama pipi. Waziri akakamatwa Uwanja wa Ndege akitorosha mzigo! Viongozi wetu wakaenda Rio Janeiro mwaka 1992 kwenye Mkutano wa Mazingira na Hali ya Hewa, wakatafuna we hela zetu huko badala ya kutembelea Favela na kujifunza kuhusu hatari ya Latin Americanization of Africa!

Companero,

..kuanzia 1980 mpaka 1985 hali ilikuwa mbaya kuliko hiyo unayoisimulia kuhusu miaka ya 90.

..kwa baadhi yetu maisha hayajawahi kuwa magumu Tanzania kama miaka ile ya kupanga foleni za almost kila bidhaa unayoifikiria.

..wengine tunakumbuka toka wakati unaweza kuanika nguo nje ya nyumba yako hata siku mbili na bado ukaikuta. baada ya hapo wizi mdogo mdogo ukaanza, then ukabaji, na kuendelea mpaka kufikia ujambazi wa kutumia silaha.

..nakumbuka toka msamiati wa jiwe la 'fatuma' ulivyoingia. nakumbuka wale majambazi sugu kama Hamisi Shija "Nyau", Leloo, na wenzao, walivyotoroka Keko au Ukonga na baada ya hapo ku-terrorise nchi nzima.

..nakumbuka RAIDS za polisi,mgambo,na JKT, kukamata wazururaji na kuwapelekea kulima Gezaulole na Kibugumo. ulikuwa unaweza kukuta kikundi cha wananchi wamefunganishwa mashati kiunoni wakiwa chini ya ulinzi tayari kutupwa kwenye karandinga.

..pia ugonjwa wa kipindupindu niliusikia kwa mara ya kwanza miaka hiyo na ugonjwa huo umedumu mpaka leo hii.
 
9534_179942535338_747855338_4355325_7952301_n.jpg

Toka tupate Uhuru mpaka leo uwezo wetu wa kujenga mashule mazuri mazuri ndo umeishia hapa.

Ahahahahahaaa...tatizo ni upumbavu na ujinga wa Miafrika. Hebu cheki madarasa ya shule za msingi za majuu.

classr8.jpg

Cheki kompyuta hizo....
classr16.jpg

Sasa somebody shut me up by proving me wrong that Miafrika Sivyo Tulivyo....
 
You see Sir, we look at things from different point of views. Mimi naangalia vitu vilivyo-trigger events. Lakini wewe siku zote unaangalia matukio yenyewe.

Now you are talking. What/who triggered the following events:

1. Kuanzishwa kwa sheria mpya ya uwekezaji na kuuzwa kwa Nyara za Taifa mara tu baada ya kupitishwa kwa Azimio la Zanzibar?
2. Kukithiri kwa Rushwa iliyopelekea wafadhali wagome kutoa hela mpaka Ripoti ya Jerry Helleiner na ile ya Jaji Warioba zilipotoka?
 
Ahahahahahaaa...tatizo ni upumbavu na ujinga wa Miafrika. Hebu cheki madarasa ya shule za msingi za majuu.

classr8.jpg

Cheki kompyuta hizo....
classr16.jpg

Sasa somebody shut me up by proving me wrong that Miafrika Sivyo Tulivyo....

FYI Hata TZ kunazo shule kama hizi..usidhani kuwa hizi ni maajabu tu kwa majuu.
Ishu ni kuwa majority ya watanzania vijijini bado wanagubikwa na umaskini wa kutisha hiyo ni fact.
Miafrika ndivyo ilivyo sawa..wewe je siyo miafrika ndivyo ilivyo? Unatofauti gani na wengine kwa maana ya kuwa baada ya kupata mwanga umeifanyia nini jamii yako ili tukukumbuke katika historia kuwa alikuwapo Julius, akakataa kuwa kama miafrika mingine akafanya kadha kadha kadha.
Usidhani kukaa majuu na kuponda watanzania ndo utauvua uafrika.
 
Acha longolongo zako wewe. Itisha harambee kuchangisha hela za kununulia rangi mkaipake shule yenu ya Mlimani walau ing'ae kidogo kama hizo za majuu...aaaah
 
Ahahahahahaaa...tatizo ni upumbavu na ujinga wa Miafrika. Hebu cheki madarasa ya shule za msingi za majuu.

classr8.jpg

Cheki kompyuta hizo....
classr16.jpg

Sasa somebody shut me up by proving me wrong that Miafrika Sivyo Tulivyo....

There you go !!!! Afu wale watoto hao watahesabiwa kwenye takwimu kuwa wamepata elimu. Na kwa mawazo ya Companero na Mkandara kuwa taabu wanayopata itaelekeza kwenye innovation.

Kwa maoni yangu binafsi kati ya hayo watoto, wale watakaopata bahati ya kufika chuo kikuu wataishia JF kuendeleza our favorite national past time - ULALAMISHI.
 
FYI Hata TZ kunazo shule kama hizi..usidhani kuwa hizi ni maajabu tu kwa majuu.
Ishu ni kuwa majority ya watanzania vijijini bado wanagubikwa na umaskini wa kutisha hiyo ni fact.
Miafrika ndivyo ilivyo sawa..wewe je siyo miafrika ndivyo ilivyo? Unatofauti gani na wengine kwa maana ya kuwa baada ya kupata mwanga umeifanyia nini jamii yako ili tukukumbuke katika historia kuwa alikuwapo Julius, akakataa kuwa kama miafrika mingine akafanya kadha kadha kadha.
Usidhani kukaa majuu na kuponda watanzania ndo utauvua uafrika.

Hahahahahahaaa...kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti sana. Ni wapi nimesema Miafrika Ndivyo Ilivyo? Ukiangalia signature yangu inasema Miafrika Ndivyo Tulivyo. Na kila sehemu nitumiapo hiyo kauli mbiu natumia neno Tulivyo. Sasa unajua na kuelewa tofauti ya neno Ilivyo dhidi ya Tulivyo? Kama hujui sema, usione aibu, nitakujulisha!
 
Back
Top Bottom