Hisia za wakati wa mvua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hisia za wakati wa mvua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jacaranda, Mar 22, 2012.

 1. J

  Jacaranda Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nazikumbuka vizuri siku kama hizi ,siku ambazo mvua ilikuwa ikinyesha wakati bado niko motto mdogo.Kipindi cha maisha yangu ambapo sikuwa na hofu ya maisha yangu ya baadae,kipindi ambacho wasichana wa rika langu walikuwa wakikata nywele na kukimbizana na mimi kifua wazi usiku na mchana

  Kipindi kile mvua iliponyesha nilisimaa dirishani na kuhesabu kila tone lidondokalo toka mbinguni.Nilishangazwa na jinsi matone ya mvua yalipodondoka chini yalivyofanya vijito vidogo vidogo ambavyo vilitiririka na kusomba mchanga dhaifu na kutokomea mabondeni pamoja .Nilikuwa najiuliza kwa nini maji yasitiririke bila kuondokaa na mchanga ulijishikiza kinyonge juu ya ardhi , sikupata jibu cha nini chanzo cha ukatiri ulioumbwa ndani ya matone ya mvua.

  Miaka mingi sasa imepita toka siku hizo.mvi zimekishambulia kichwa changu kama nzi wakusanyikapo kwenye mzoga ulio oza na kutelekezwa nyikani,mikunjo imeupamba uso wangu mithili ya poda ajikandikazo mwali wakati wa harusi yake na mashavu yangu yameanza kumiminika utafikiri yanataka kuukimbia uso wangu.
  Naposimama kwa fimbo huku nikishika kiuno changu nikigumia kwa maumivu sina shaka nimeona vitu vingi katika maisha yangu.Vingine vitiavyo huruma na masononeko moyoni,vingine vikatishavyo tamaa na kupokonya mori wa kuishi hata wa mashujaa naam na hata vile vizalishavyo jakamoyo ndani ya moyo wangu
  Nimewazika watu niliowapenda zaidi ya kila kitu maishani mwangu , wengine walikuwa wachanga ambao mioyo yao ilikuwa tupu ikisubiri kujazwa na uzuri wa maisha ya dunia na mikono yao ikijiandaa kuwakumbatia wapenzi wao naam nao walikufa ,wengine walikuwa ni vijana ambao dunia ilikuwa ikiwasubiri huku ikiwaita njooni njooni muone nini nimewatunzia ooh walikufa ooh walikufa wakiwa na matumaini bila kuiona hatima yao duniani la hasha sijawasahu wale ambao nilicheza nao tukayachubua magoti yetu pamoja wale ambao tulikuwa tukiitana na kushangaa maungo yetu yalivyokuwa yakibadirika huku tukishangaa kumbe nywele hazioti kichwani peke yake nao pia wamekufa wengine mikononi mwangu na wengine mbele ya macho yangu. Vidole vyangu hivi ambavyo sasa vinaliwa na gauti na kuonekana kama kijiko kilichopondwa pondwa vilitupia mchanga juu ya makaburi yao na kuweka mataji ya maua juu yake na midomo yangu ikiwaombea raheli kwenye safari ya uko waliko elekea .

  Naam sasa hivi nimetambua kwa nini matone mvua yalikuwa katiri kiasi kile.Nimejua kwanini yaliuonea mchanga ule dhaifu. Sasa nimegundua kwanini mchanga haukusimama na kupigana.Maono haya hayana maana tena. Nimezeeka siwezi tena kupigana,naam ningekuwa kijana ningepigana hakika ningepigana bila kuchoka naapia kwa mbigu na ardhi ningepigana bila kikomo.Haina maana tena, mikono yangu,miguu yangu na macho yangu vyote vimekula njamaa juu yangu havitaki kuniruhusu kwenda vitani tena.

  Sitaki tena maono zaidi ya lile la mke wangu alitembea mara ngapi njee ya ndoa.Najua hilo haliwezi kufumbuliwa braah braah braah asali wa moyo wangu amezeeka,kumbukumbu zake zimemkimbia,hamkumbuki hata mpenzi wake wa kwanza braah kila mara ananiita honey honey bila shaka amelisahau jina langu, ila nafurahi bado anakumbuka wapi tulikutana na pia bado hajasau ile ahadi ya kuwa atakufa mikononi mwangu.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Bend it like Beckham.
   
 3. J

  Jacaranda Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijakupata
   
 4. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Very interesting story, Jacaranda ni moja ya mtaa hapa mjini Mbeya, je jina lako lasadifu mahali ulipo??
   
 5. J

  Jacaranda Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thanx saana nope jina langu alisadifu huo mtaa ila natamani kuja mbeya siku moja kwani nasikia baridi ya huko inakomaza mifupa na kufanya watu waishi miaka mingi
   
 6. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sasa wewe si umeshazeeka? Unataka uishi miaka mingi yanini.. Karibu mkuu kweli baridi is available...
   
 7. J

  Jacaranda Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nataka bado kula kula happy za dunia si unajua life is beatiful
   
 8. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hebu tuwaachie hawa kopa Cocacola a.k.a under 17 wafaidi na wao,
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  i see,veri tachingi! Loh!

  Seriously paragraph 2 za mwisho nimezipenda!
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  interesta stori..
   
 11. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,678
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Jacaranda_name of a genus of certain plants (one of whose specie is jacaranda mimosfolia) used to provide shading, under which one feels confortable to relax especially when you are dealing with such a sunny place like where i live. All I can say is u blend to the name big time!
   
 12. J

  Jacaranda Member

  #12
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  your absolutely correct
   
Loading...