Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 12,747
- 29,987
Ila dada mi bucha natoa wapi
Mungu wangu😅😅
Sijui hata huwa yanatokaga wapi 🤣🤣
Ila dada mi bucha natoa wapi
Mungu wangu😅😅
Hisia ni hali ya ndani ya mtu inayohusiana na moyo au akili, kama vile furaha, huzuni, hasira, au woga. Kwa kifupi, hisia ni namna mtu anavyojisikia kuhusu jambo fulani. Kisayansi hisia ni mechanism ya mwili inayoongozwa na parasympathetic nervous system ambayo inatumika zaidi kwnye kukabiliana na maamuzi ambavyo hayana control ya ubongo ambayo mara nyingi ni pale mwili unapojudge emergency na kutaka kitendo cha haraka ambacho kingepitia kwnye ubongo kingechelewa kufanyiwa maamuzi, kama vile unapokutana ghafla na simba maamuzi ya hapo ni hisia za kifo na unaweza kukuta umeruka shimo ambalo kawaida akili isngekutuma uruke!
Mtu mwenye kutawaliwa na hisia anaitwa ana emotional immaturity au ana low emotional quotient km so hafanyi maamuzi kwa kufikiria sawasawa anarukaruka tu km anafanya emergency
Huyu hatuna msaada nae 😃View attachment 3578226
Sijui hata huwa yanatokaga wapi 🤣🤣
You deserve a platinum membership 🫡
Nimeelewa vizuri sana kwamba moja ya kazi ya hisia ni kukusukuma kufanya kitu ambacho, kama ungetumia akili pekee, pengine usingefanya kwa sababu akili isingekuruhusu. Hapo sawa kabisa nimeelewa
Sasa swali linakuja
Je, mtu ambaye anaendeshwa zaidi na hisia anawezaje kujicontrol na kuacha tabia ya kutumia hisia pale ambapo alipaswa kutumia akili zaidi?
Nilifikiri huu uzi kila mtu anaruhusiwa tu kuchangia,Binti wa zamani
win-one
ERoni babu
Grahams
Seran mom
Mshana Jr Dad
Mbaga Jr mdogo wangu
Robert Heriel Mtibeli my Brother
Nimerudia kusoma zaidi ya mala 1Ukiona mtu mzima bado yupo emotional ni kwamba tunasema alidekezwa, mtoto wa mama, hakupata malezi bora, nk. Kwa sababu through human growth and development kuna achievements katika kila stage zinategemewa kuonekana anaweza, na ndio maana ukipeleka mtoto clinic unaulizwa maswali kuhusu anaweza kufanya nini ili walinganishe na benchmark.
Samahani kama nimeeleweka vibayaNilifikiri huu uzi kila mtu anaruhusiwa tu kuchangia,
Haya ngoja tuwasibiri hao uliowaita ili watupe majibu.
Asante sana MkuuHisia ni hali ya ndani ya akili na mwili inayokufanya uhisi jambo fulani kihisia—kama furaha, huzuni, hasira, hofu, au upendo. Ni namna ubongo wako unavyoitikia kile unachopitia au kufikiria.
hisia zinahusiana na:
Ubongo (hasa sehemu kama limbic system)
Homoni (mfano adrenaline, dopamine)
Mwili (mapigo ya moyo kuongezeka, jasho, n.k.)
Kwa hiyo, hisia si mawazo tu—ni mchanganyiko wa mawazo + mwitikio wa mwili + uzoefu wa ndani.
Nimerudia kusoma zaidi ya mala 1
Lakini nimechukua hicho kipande hapo👆 Asante Mkuu nimepata kitu
Kwa mkutadha huu ni kwamba hisia ni sehemu nzuri inayotoka ndani inayofanya mambo mbali mbaliKibiblia zaidi..
Wanadamu wangekuwa wapi kama hatungekuwa na hisia, ikiwa tulikuwa na uwezo wa kudhibiti hisia wakati wote? Pengine tungekuwa kama wakala, tuitikia hali zote kwa mantiki na kamwe si hisia. Lakini Mungu alituumba kwa mfano wake, na hisia za Mungu zinafunuliwa katika Maandiko; Kwa hivyo, Mungu alituumba viumbe vya kihisia. Tunahisi upendo, furaha, uheri, hatia, hasira, kukata tamaa, hofu, nk. Wakati mwingine hisia zetu ni nzuri kwa uzoefu na wakati mwingine sio. Wakati mwingine hisia zetu zinatokana na ukweli, na wakati mwingine hisia "hudanganya" kwa kuwa zinategemea ahadi za uongo. Kwa mfano, ikiwa tunaamini uongo kwamba Mungu hawezi kudhibiti hali ya maisha yetu, tunaweza kupata hisia za hofu au kukata tamaa au hasira kulingana na imani hiyo ya uwongo. Bila kujali, kama hisia ni za nguvu na halisi kwa mtu anayehisi. Na hisia zinaweza kuwa viashiria vya manufaa ya kile kinachoendelea ndani ya mioyo yetu.
Hayo kusemwa, ni muhimu kwamba tujifunze kuhusu kudhibiti hisia badala ya kuruhusu hisia zetu kutudhibiti. Kwa mfano, tunapopatwa na hamaki, ni muhimu kuweza kuacha chenye tunafanya na kutambua kwamba tuna hasira, kuchunguza mioyo yetu kuamua ni kwa nini tuna hasira, na kisha kuendelea kwa njia ya Biblia. Hisia sizizodhibitika huwa hazizalishi matokeo ya kumheshimu Mungu: "Kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu" (Yakobo 1:20).
Sawa sawa dearHisia ni mihemko ambayo binadamu na wanyama hujisikia moyoni na huathiri mwili pia kupitia ubongo. Kadiri ya saikolojia zinaweza kuwa za pendo, hamu, furaha, au kinyume chake za chuki, woga, hasira, huzuni na nyingine nyingi tu.
Umeeleweka mkuu asante🙏Yes ukisikia mswahili anasema huyu jamaa ana utoto mwingi ujue anamaanisha ana emotional immaturity au low EQ na anatawaliwa na hisia, na mtu wa namna hii anakuwa na mapungufu mengine mengi kwenye mahusiano na watu kwa kuwa anakuwa more of self directed and selfish asiyejali hisia za wengine au anajali kidogo lakini anajipakulia kila kitu kwa ulafi mkubwa bila kujali maumivu ya watu wengine
ShesRise_1Hisia ni hali ya ndani ya mtu inayohusiana na moyo au akili, kama vile furaha, huzuni, hasira, au woga. Kwa kifupi, hisia ni namna mtu anavyojisikia kuhusu jambo fulani. Kisayansi hisia ni mechanism ya mwili inayoongozwa na parasympathetic nervous system ambayo inatumika zaidi kwnye kukabiliana na maamuzi ambavyo hayana control ya ubongo ambayo mara nyingi ni pale mwili unapojudge emergency na kutaka kitendo cha haraka ambacho kingepitia kwnye ubongo kingechelewa kufanyiwa maamuzi, kama vile unapokutana ghafla na simba maamuzi ya hapo ni hisia za kifo na unaweza kukuta umeruka shimo ambalo kawaida akili isngekutuma uruke!
Mtu mwenye kutawaliwa na hisia anaitwa ana emotional immaturity au ana low emotional quotient so hafanyi maamuzi kwa kufikiria sawasawa anarukaruka tu km anafanya emergency
Babu shikamoo
Ni kuhisiJe, hisia ni nini?
Mara nyingi utasikia mtu akisema baada ya jambo kutokea
Nilihisi tu itakuwa hivi au
Kabla hii issue haijatokea, nilihisi kuna kitu hakipo sawa
Maneno haya hujitokeza mara nyingi baada ya tukio husika kutokea
Je, hisia ndizo zinazoitwa machale?
Wengine husema :Machale yalinicheza
Hapa tnajiuliza, je hisia na machale ni kitu kimoja au kuna tofauti?
Hisia ni kitu gani hasa?
Zipo aina mbalimbali za hisia, kama vile
Hisia za maumivu
Hisia za furaha
Na ile hali ya kuhisi jambo fulani kabla halijatokea, mfano kuhisi hatari iliyo mbele
Je, inawezekana ku control hisia zako?
Je, unaweza kuzifanya ziwe nzuri au mbaya kulingana na hali?
Ni namna gani mtu anayetawaliwa na hisia anaweza kujinasua na kutumia akili zaidi?
Karibuni kwa mjadala 🙏
ShesRise_1
ShukranNi kuhisi
Nimetikisa enhee hatua inayofata?Tikisa Bega kidogo.
Mjukuu,Asante sana Mkuu
Hivi ni nini hua kinatokea mpka unasikia mtu akisema Mf: yule anaendeshwa na hisia je kuna namna ya mtu kujigundua kia ni mtu wa hisia zaidi kuliko akili
Na unaweza vp kuthibiti matumizi ya hisia kuliko akili