Hisa za Zanzibar katika Benki Kuu: Je, SMZ imewahi kuipa ruzuku BoT? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hisa za Zanzibar katika Benki Kuu: Je, SMZ imewahi kuipa ruzuku BoT?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Oct 6, 2012.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, Mchambuzi, Nonda, Mdondoaji, Barubaru, Ritz, Jasusi, Taso,

  ..hebu tuendelee kuuchunguza huu muungano wetu zaidi.

  ..kuna taarifa kwamba ZNZ ilitoa 11% ya mtaji wa kuanzisha BOT.

  ..pia AG wa ZNZ aliwahi kunukuliwa akisema kwamba pamoja na kutoa hisa hizo, SMZ ilianzisha PBZ[People's Bank of Zanzibar] ambayo ilikuwa ikifanya kazi kama "benki kuu" ya ZNZ kwa kipindi kirefu mpaka miaka ya 80 au 90.

  ..katika gazeti la raia mwema, gavana wa BOT, Prof.Ndulu, amenukuliwa akisema kwamba kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa BOT, benki hiyo imepata faida na kutoa gawio la $ 173 million kwa serikali.

  ..kwa msingi huo huenda basi ZNZ na SMZ wamepewa mgao stahiki kutokana na faida iliyopatikana BOT.

  ..hapa nitapenda kuhakikishiwa kwamba ZNZ imepata stahiki yake kutokana na kiwango cha hisa ilichotoa mwaka 1966.

  ..kitu kingine ambacho amekieleza Prof.Ndulu ni kwamba kwa muda wote tangu kuanzishwa kwake BOT ilikuwa ikiendeshwa kwa RUZUKU kutoka serikalini.

  ..sasa mimi napenda kuuliza: Katika miaka yote ambayo BOT ilikuwa ikiendeshwa kwa HASARA na kutegemea RUZUKU toka serikalini, ZNZ au SMZ ilikuwa ikitoa kiasi gani??

  Nakala:
  takashi, Zitto, Edwin Mtei, Mkandara, EMT, Kitila Mkumbo, Masanja, Rev. Kishoka, Kasheshe, Nnauye Jr, Maxence Melo, Kiranga, Geza Ulole, Kubwajinga, Nonda, Malila, Kichuguu, Nyani Ngabu, Selemani, Mohamed Said, maggid

  NB:

  ..nawaomba wote mchangie hoja hii. hata wale ambao sikuwa-tag mjisikie huru kabisa kuchangia hapa. kila mmoja wenu achangie tafadhali.
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Joka kuu, pia kuna asilimia 7 ZNZ inapata kutoka pato la taifa.
  Ruzuku iliyokuwa BoT inapata ni kodi ya Tanganyika, SMZ haikutoa kitu.
  Haiwezi kutoa kitu kwasababu kipindi cha miaka 15 mishahara ya wafanyakazi wa SMZ inatoka hazina Dar es Slaam.

  Kama wamepewa gawawio basi ni pesa za bure kwasababu SMZ haitoi ruzuku kwa JMT, ila kinyume chaeke ni kweli.
  Utashangaa pia kuna bilioni 32 ambazo hazijulikani Gharibu Bilal anapewa kwa ajili gani.

  Jana nimeona Shein anapokea nyaya za umeme, kumbuka hizo zimelipiwa na JMT, kama ni mkopo huo ni wa Mtanganyika.

  Mambo kama hayo ndiyo yanawafanya WZNZ wang'ang'anie mkataba. Wanajua wanachokipata ndani ya huu muungano wasiotaka kuuvunja lakini kelele nyingi.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3, Kibunango, Barubaru, Taso,

  ..I think we have a BIG mess here.

  ..sasa hebu tusogee mbele kidogo.

  ..Ismail Jussa amenukuliwa akisema ZNZ inataka kuwa na BENKI KUU na SARAFU yake yenyewe.

  ..kwa msingi huo itabidi wapewe fedha fulani kutokana na hisa zao ktk BOT ili waweze kuanzisha benki kuu ya ZNZ.

  ..Je, wakati tunavunja BOT, na kuanzisha benki kuu za Tanganyika, na Zanzibar, suala la kwamba Zanzibar imekuwa haichangii kuipa ruzuku BOT litakuwa na nafasi gani??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mjadala kuhusu Zanzibar katika Muungano ni kama mjadala wa dini.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Kama Gavana Ndullu amesema kuwa benki kuu imepata faida kwa mara ya kwanza tangu iundwe basi ama hajui anachosema au anapotosha ukweli makusudi.

  Nakumbuka mwaka 1977 kabla ya vita vya Uganda kulikuwa na mjadala mkubwa pale Benki kuu wakati Gavana akiwa Nyirabu. Wakati huo benki kuu ilikuwa imepata faida na Gavana Nyirabu alikuwa amependekeza wafanyikazi wapewe bonus. Kuna baadhi ya wasocialist pale waliokuwa wanapinga wazo hilo eti kuwapa wafanyikazi bonus ni kinyume cha maadili ya ujamaa.

  Kwa hiyo hii si mara ya kwanza kwa benki kuu kupata faida.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Kichuguu,

  ..hebu tupe mchango wako basi.

  ..suala hili ni muhimu na linahitaji sauti ya kila Mtanganyika isikike.

  ..msipochangia moderators wataitia kapuni thread hii.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..Thank u.

  ..OK, tuchukulie kwamba 1977 BOT ilipata faida.

  ..Je, SMZ ilipewa gawio stahiki?

  ..kwa miaka ile ambapo BOT ilikuwa ikiendeshwa kwa hasara, SMZ ilikuwa inaipa ruzuku kiasi gani??
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  That is a good question. Sina data zozote kama SMZ ilipewa gawiwo lake lakini ninachojua alikuwepo naibu gavana kutoka Zanzibar wakati huo.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..hapa nakuomba urejee makabrasha yako kidogo.

  ..kwa uelewa wangu wakati wa Nyirabu, BOT ilikuwa na naibu gavana Mohamed "Bob" Makani.

  ..Naibu Gavana toka ZNZ naamini aliteuliwa wakati wa uongozi wa Dr.Idris Rashid.

  ..sasa hebu turejee katika topic husika na tujaribu ku-expand mjadala ili tupate wachangiaji wengi zaidi.

  ..Hivi karibuni serikali ya muungano[read Tanganyika] ilitoa sh.32 bilion kwa Makamu wa Raisi kwa ajili ya maendeleo ya ZNZ.

  ..Je, una kumbukumbu ya wakati wowote ule SMZ kutupatia Watanganyika na serikali yetu mapesa kwa ajili ya shughuli za maendeleo??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Sijawahi kusikia hata siku moja kuwa serikali ya SMZ imetoa pesa kwa ajili ya shughuli za maendeleo bara. Nimesoma tu propaganda za Wazanzibari wanaochukia muungano wakitoa madai hayo kama mojawapo ya sababu za kutoupenda muungano bila kutoa ushahidi wowote. Labda niulizie kwenye vyanzo vyangu kama madai hayo yana mantiki yoyote.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  hapana sii kweli hata kidogo maana hapa tunauliza maswali ambayo tukipewa majibu tutayaangalia ukweli wake. Tunachotaka kujua hapa ni ukweli..Ikiwa madai wanayodai yana Ukweli wowote tutajifunza na sisi. Wakisema hawapewi, wakisema hawajapewa ni lazima tukubali kuwaonea...
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu bila data za mchango wako unategemea nini?
  Tatizo nyie wenzetu mentality ya kubebwabebwa bado ni tatizo.
   
 13. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kiukweli serikali ya muungano inamapungufu mengi sana!

  Ndio maana Dr Slaa aliwahi kusema kwa level ya ufahamu wake (PhD) akijifunza falsafa ya muungano wa vitu viwili ,hajawahi kuona muungano wa vitu viwili vikiunganishwa kisha vikatokea vitu viwili tena vyenye sura ya vitu vilele viwili tofauti. MAPUNGUFU YA MUUNGANO YAPO, ILA HAIPO NIA YA DHATI YA KUTATUA KERO ZA MUUNGANO....!
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  huu muungano haufai kabisa, Mtanganyika amebebeshwa zigo la misumari bila sababu ya msingi, wanaofaidika ni wazanzibari lakini midomo juu kuleta vurugu.

  Katiba mpya inapaswa kurekebisha haya, ni wakati wa Watanganyika kuamka na kukataa unyonyaji huu....

  Samahanini nimetoka nje ya mada, nawatakia majadiliano mema, hapanifai hapa
   
 15. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mie nitampigia kura yeyote mwaka 2015, atakayekuwa na sera ya kuuvunja muungano.
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mkuu Joka kuu, unajua hili tatizo la muungano kuumiza upande mmoja linakuzwa kwa sauti, kimantiki si kweli.

  Hizo bilioni 32 alizopewa gharibu Bilal ni kwa ajili ya maendeleo ya ZNZ. Hakuna maelezo.
  Ninakuhakikishia kuwa kuanzia komandoo hadi sasa mishahara inatoka hazina.

  Tuje kinadharia, bajeti ya ZNZ mwaka huu ni bilion 660. Hizi ni pesa ambazo haiwezi kuendesha hata wizara moja ya muungano. Nitashangaa kusikia kama ZNZ inachangia hata senti tano.

  Muungano ukivunjika itabidi kuwepo na msuluhishi wa kimataifa atakayeanagalia Assets and Liabilities.
  Itakuwa ni uonevu kwa Watanganyika kama itachukuliwa 11 ya BoT ili waanzishe Bank.
  Kumbuka waziri wao amekiri kuwa kuanzia katikati ya 1995 wamekuwa wanapata gawio lao la 4% kutoka katika pato la Taifa.

  Pato la taifa hapa ni Tanzania. Katika siku za karibuni wanapata 7.5% na bado wanataka ifike 11%
  Jambo la kuijuiliza wanatumbukiza nini katika pato la taifa kutoka SMZ?

  Nimeongelea msulsuhishi wa kimataifa kwasababu ilipovunjika EAC kulikuwa na mali na madeni. Aliteuliwa marehem Dr Victor Umbrich aliyekuja na formula ambayo kila mwanachama aliridhika.

  Kwasasa hivi madeni ni mali ya JMT ambayo ni Tanganyika kwa vile ni deni.
  Hatuwezi kuongelea uchumi, BoT na kuacha pembeni madeni.
  Hoja ya madeni ni kuwa wao wanapata 4% ya misaada kwa mujibu wao. Vyovyote iwavyo ni lazima wawe na sehemu ya deni la taifa.

  Miaka michache iliyopita kifaa cha umeme kiliharibika kule ZNZ. Baada ya kushindwa kununu ilibidi waombe JMT(Nahodha Shamsi Vuai). BoT ilitoa bilioni 5 kwa kusaidia umeme unaokwenda kuhudumia SMZ.
  Jana wamepokea nyaya zilzionunulia na JMT siyo SMZ, sasa hapo ndipo unaweza kupata jibu wanatumbukiza nini katika muungano.

  Ikumbukwe pia mapato yote yanabaki ZNZ ingawa soko la bidhaa linakuwa la JMT. Kwa mneno mengine kodi ya makontena n.k. yanayotua bandari huru ZNZ inabaki ZNZ. Soko linatakiwa liwe la Tanzania ambako TRA wanakusanya mapato. Umeona mkanganyiko hapo?

  Na mwisho kama wanataka sarafu, tayari wana kila kitu, je, wanataka mkataba wa kitu gani?
  Kwanini tusiwaunge mkono waanzishe sarafu yao ili hatimaye tuvunje jahazi na tuchukue mbao zetu maana hawana mbao!
  Kwa wenzetu WZN madeni si yao, wanachotaka ni simple formula tupeni pesa.
   
 17. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  JokaKuu angalia facts zako vizuri.

  kwa kifupi benki kuu imekua ikijiendesha yenyewe kwa muda mrefu sana, hata twin towers zimejengwa na faida ya bot, hata mwaka jana ilipeleka gawio serikalini, tofauti ni kuwa mwaka huu wamepata faida sana.

  Mwaka jana smz wamepewa gawio lao na benk kuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kuweka nini ktk pato la Taifa si hoja sana, maana hata huku Tanganyika kuna mikoa inaiingiza kidogo sana ama hakuna kabisa kwa pato, tunachofanya ni kushare huu umasikini ili ku-balance equation.

  Kinachouuzi ni kelele za wazanzibari, inakera sana. Mtu yeyote atakaye kuwa na sera za kuuvunja muungano atakuwa ame book kura. Tunalalamika umasikini umasikini hivi ni moja ya sababu ya umasikini wa TZ, watu badala ya kuchapa kazi wanapoteza malighafi mda, na malighafi material.
  Why keep nagging, it needs to be done once and for all.
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280

  Semilong,

  ..taarifa nilizozileta hapa nimezitoa kwenye gazeti la raia mwema ambao walifanya mahojiano na Prof.Ndulu.

  ..lakini swali langu linabaki pale pale. miaka ile ambayo BOT ilipata ruzuku toka serikalini, kila upande wa muungano ulichangia kiasi gani ktk ruzuku hiyo??

  ..pia nimeuliza ni lini ZNZ imetupatia Tanganyika mapesa kwa ajili ya shughuli za maendeleo? nauliza hivyo kwasababu majuzi tumesikia kupitia kikao cha bunge kwamba Dr.Bilali amepewa bilion 32 kwa ajili ya maendeleo ya ZNZ.

   
 20. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  JokaKuu,

  Nashukuru sana kwa kunialika kwenye mjadala huu muhimu; Kwa kweli kwa upande wangu, suala la muungano, pamoja na kwamba naunga mkono uwepo wake, kwangu mimi, kama anavyosema Tundu Lissu, limetawaliwa na kiini macho kuliko reality; Hii ndio maana muungano wetu unayumba, ingawa wakubwa hawataki kukubali ukweli juu ya hili kwa sababu za kisiasa, hasa ubinafsi wa madaraka;

  Naomba pia niseme kwamba katika mjadala huu, lakini pia suala la muungano kwa ujumla, mimi ni Mwanafunzi kuliko mwelewa, hivyo mawazo yangu katika huu mjadala yataegemea zaidi huko. Ningependa kujadili hoja iliyopo mbele yetu kwa mtindo wa kiini macho – kutoelewa ukweli, kwahiyo nisipoeleweka, naomba ieleweke kwamba ni kwa sababu Mchambuzi sio muelewa wa suala husika.

  Moja, Zanzibar ilipata uhuru wake mwaka 1964, na ndani ya mitano na nusu, ikaungana na Tanganyika, na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Originally, kwa ufahamu wangu, suala la FEDHA halikuwa sehemu ya mkataba wa muungano, suala hili liliingizwa baadae kwenye katiba ya Muda ya mwaka 1965, na likaendelea kuwa treated KIMUDA MUDA mpaka 1977 katiba ya kudumu ilipozaliwa. Sasa iwapo Zanzibar ilichangia 11% towards uanzishwaji wa BOT in 1966, ningependa kwa wale waelewa zaidi wanisaidie kunielimisha kwamba mchango huu ulifanyika chini ya makubaliano yepi - mazingira haya yalihalalishwa na nguvu gani;

  Pili, kipindi cha 1961 – 1966 kilikuwa ni kipindi cha maandalizi ya nationalization katika nyanja zote za uchumi, huku sekta ya benki ikiwa ndio TARGET NUMBER MOJA; Tulifanya uamuzi wa kuwa WAJAMAA in every aspect, including Banking; Lakini hapa hapa pia tunaelimishwa na historia kwamba Zanzibar chini ya Karume haikuwa inafuata UJAMAA, na actually muungano chini ya Karume ulikuwa unaonekana umetulia na hauna matatizo kwa sababu tu - Karume alikuwa anapuuzia constitutional and union matters; Ningependa kuelewa zaidi, Je Banking Sector katika uchumi wa KIJAMAA ilikuwa inafanya mambo gani kule Zanzibar, na iwapo walichangia hiyo 11%, walitegemea au walipata kitu gani in return;

  Tatu, katika original articles of the Union, kama tulivyokwisha ona, banking issues hazikuwepo, mpaka 1965 ndani ya katiba ya muda; Lakini suala la mapato ya ndani/internal revenues i.e. personal income tax and corporate tax, haya yalikuwepo in the original articles of the union kama masuala ya muungano; Ningependa kufahamu, je Zanzibar made their contribution to BOT from what sort of income, na pia walikuwa wanaendesha mambo yasiyokuwa ya muungano kwa what source of income? Corporate Tax? Je Zanzibar kulikuwa na state owned enterprises za mfumo wa kijamaa? Au mapato yake yalitegemea zaidi Karafuu na Income Tax kutoka mishahara ya watumishi wa serikali? Kuna mtu mwenye records za mapato ya Zanzibar atusaidie – ya kipindi cha 1964-1967?

  Nne, before 1965 mwaka ambao BOT ilianzishwa, Tanzania had no monetary policy, instead mambo yote ya kibenki yalikuwa yanaendeshwa na East Africa Currency Board chini ya mkuu mmoja mwingereza aliyekuwa anasimamia nchi zote za East Afrika katika hili – EACB ilikuwa zaidi ni monetary changer, converting currencies and exporting it to the mother land (Britain); Mabadiliko juu ya hili yalianza mwaka 1965 ambapo tulianzisha our monetary policy and financial controls, na mwaka mmoja baade kuanzishwa kwa BOT; Ningependa kuelewa Zanzibar ilikuwa inajiendeshaje, hasa to finance finance its economic development wakati mikopo ya aina yoyote kutoka nje ya nchi was a UNION MATTER;

  Kuna sehemu nimesoma (from Yilma Makonnen) kwamba:

  "…Zanzibar did not make any official declaration explaining its position with regards to the effect of state succession on the international rights and obligations of the colonial predecessor state which applied or extended to or contracted on behalf of Zanzibar; Even upon the request of the UN secretary general, Zanzibar refrained from making any statement clarifying its position."

  Kwa mtazamo wangu ambapo unaweza kuwa ni finyu sana, total silence ya Zanzibar "during its brief existence as a nation", ingeleta tatizo kubwa sana miaka ile ya mwanzo wa mapinduzi, kama sio miaka ya baadae; tumekuja kuona hili miaka ya baadae, in the context of mikwaruzo mbalimbali, kuanzia sakata la Jumbe, OIC, n.k; Lakini swali muhimu kwangu ni je, katika kipindi hiki cha ukimya, maana yake ni kwamba Zanzibar haikuwa in any position kupata ushirikiano wowote na mataifa ya nje; Ushirikiano na nje kimakubaliano na kimikataba ilianza baada ya muungano, which means hata uwezo wa kujiendesha ulitegemea zaidi ruzuku kutoka bara chini ya kipengele cha articles of the union kinachosema kwamba masuala yote ya mikopo kutoka nje kwa ajili ya biashara ya kimataifa n.k ni masuala ya muungano; hii inazidi kuniaminisha kwamba nguruvi3 yupo sahihi kwamba Zanzibar ilikuwa inaendeshwa kupitia ruzuku toka bara;

  Naelewa kwamba nimejadili kishagala bagala na inawezekana nimezidi kuchanganya watu, lakini hivyo ndivyo muungano wetu ulivyo;
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...