Hillary Clinton: Somebody who attacks everybody has something missing

Hata uwanja mpya wa taifa ulijengwa baada ya kuona ule wa zamani kila wakichimbua wanakuta vichwa vya fisi, mbuzi, ngedere na mahirizi mambo ya Simba na Yanga.So ili tupate maendeleo serikali kuhamia Dodoma ni LAZIMA
Sifahamu umeelimika kwa kiwango gani au una umri gani, lakini nikuulize tu kwamba ina maana serikali kuhama toka mji mmoja kwenda mwingine ndiyo msingi wa maendeleo?
Ama kweli kazi tunayo!
 
Sifahamu umeelimika kwa kiwango gani au una umri gani, lakini nikuulize tu kwamba ina maana serikali kuhama toka mji mmoja kwenda mwingine ndiyo msingi wa maendeleo?
Ama kweli kazi tunayo!
Wewe unadhani kwanini tunahama labda tuanzie hapo.Mambo ya elimu na umri sidhani kama yatakusaidia sana, mfano nikisema tulicheza na your father nitakuwa sijakujibu bado utataka kudadisi zaidi
 
JPM ANA KAZI KUBWA KUIWEKA NCHI HII KWENYE MADILI KWELI NCHI ILIKUA KWENYE ICU ANA MADUI WENGI MAPAPA TENA MAFSADI NA WAHUJUMU UCHUMI UKIWA ATTACK LAZIMA WAPIGE KELELE
Jibu lako lina matatizo makubwa mawili, moja ni kule kuamini na kudhani kuwa Magufuli ataiweka nchi sawa. Hii siyo kazi ya mtu mmoja wala kazi ya miaka mitano au kumi; inahitaji kiongozi mwenye maono, kipaji cha uongozi, ushirikiano na watu wengine, kutambua kuwa yeye hajui wala hawezi kila kitu, na kwamba ni lazima kuwepo na mkakati. Hizi sifa hana.
Pili, adui wa taifa letu siyo ufisadi na mafisadi bali ni mfululizo wa uongozi mbovu usio na akili mpya wala mawazo ya kuona nje ya mipaka yetu na kujifunza kutoka kwa waliopiga hatua. Ufisadi ni matokeo ya hali hii na JPM haonekani kuwa na mbinu au uwezo wa kuibadilisha. Sanasana anachagua ufisadi gani wa kupambana nao na mwingine anauacha kwa hofu.
 
Kweli kabisa mkuu. Huyu wa kwetu anataka awe anaongea yeye tu. Anataka kuonesha kuwa wenzake walifanya hovyo kabisa hivyo yeye ndiye pekee anayeweza kufanya vyema na hatak kupngwa na ndiyo maana anasema hakuna rais mwingine isipokuwa ni yeye tu kitu ambacho hakina haja ya kukisema ila ni kama kusema yeye ndiye alfa na omega
Kujivuna kwiiingi hadi kero sasa sijui anatupeleka wapi huyu mtukufu wetu?
 
Mkuu nchi yako inategemea misaada ya wahisani, hao wanaotuletea fedha kila mwaka hawana muda wa kuandamana, sisi tunaowategemea tuna muda mwingi wa kuchomwa na jua tukimsubiri mwanasiasa aje atuhutubie. Huoni kwamba tunajenga taifa la masikini wa miili na akili pia?.

..mhh.

..lakini wenzetu wana uhuru wa kutoa maoni yao.

..pia viongozi wao hawavitumii vyombo vya ulinzi na usalama kuandama vyama vya upinzani kama hapa Tz.

..pia wana uvumilivu wa hali ya juu wanapotofautiana mawazo. Sijui kama uliangalia wale waandamanaji ktk mikutano ya vyama vya Democratic na Republican. Je umemsikia Hillary Clinton au Donald Trump akiwasema vibaya waandamanaji wale?

..Tatizo Magufuli anataka kusikia sauti yake yeye mwenyewe wakati wote. Hata akipewa ushauri mzuri anaona anapingwa.
 
Sasa wewe unalinganisha mazingira ya America na Tanzania
Mnachekesha kweli!!
Siasa za Tanzania ni Attack Attack Attack!! Mikakati+Fitina
Hizo ni siasa chafu (uchwara, za maji taka) popote pale duniani. Natumaini ujumbe huu wa ukweli unaouma umemfikia "mlengwa"
 
Siku zote mtu anaeona wenzake ndo wenye matatizo hapo aelewe kwamba yeye ndio tatizo
Sikh moja niliona kichaa mmoja kakaa na ghafla akapita chizi mbele yake, basi aliangua kicheko kikali sana na alipoulizwa akasema hamumuoni mwendawazimu huyo?
 
Jibu lako lina matatizo makubwa mawili, moja ni kule kuamini na kudhani kuwa Magufuli ataiweka nchi sawa. Hii siyo kazi ya mtu mmoja wala kazi ya miaka mitano au kumi; inahitaji kiongozi mwenye maono, kipaji cha uongozi, ushirikiano na watu wengine, kutambua kuwa yeye hajui wala hawezi kila kitu, na kwamba ni lazima kuwepo na mkakati. Hizi sifa hana.
Pili, adui wa taifa letu siyo ufisadi na mafisadi bali ni mfululizo wa uongozi mbovu usio na akili mpya wala mawazo ya kuona nje ya mipaka yetu na kujifunza kutoka kwa waliopiga hatua. Ufisadi ni matokeo ya hali hii na JPM haonekani kuwa na mbinu au uwezo wa kuibadilisha. Sanasana anachagua ufisadi gani wa kupambana nao na mwingine anauacha kwa hofu.
Masernberg, Kama huyu anayejiita mzalendo hajakuelewa hatakaa amwelewe yeyote yule. Tatio la nchi hii iku ote limekuwa uongozi bora. Hata sasa bado tunahiotaji kiongozi borfa!
 
ilikua ni dhiara zakushtukiza sasa tuhakiki na hatutoa ajira mpaka zoezi liishe ilikua kwa watumishi sasa ni wanavyuo nimesema tunahakiki
 
Akiongea katika kampeni zake kasema mano haya. "somebody who attacks everybody has something missing". Namuona Rais Magufuli kila mara katika hotuba zake ni lawama, vitisho, matamko yasiyozingatia katiba nk.

Asante mama kwa kinifumbua macho
Mlia muattack sana JK na kumuita dhaifu na kweli you had something missing... Na sasa mmekipata na si kingine ni kiboko ya mafisadi na wasio na adabu na wasio na heshima na si mwingine ni Magufuli akisema amesema na sasa ana wasubiri tarehe 1 September.
 
Jibu lako lina matatizo makubwa mawili, moja ni kule kuamini na kudhani kuwa Magufuli ataiweka nchi sawa. Hii siyo kazi ya mtu mmoja wala kazi ya miaka mitano au kumi; inahitaji kiongozi mwenye maono, kipaji cha uongozi, ushirikiano na watu wengine, kutambua kuwa yeye hajui wala hawezi kila kitu, na kwamba ni lazima kuwepo na mkakati. Hizi sifa hana.
Pili, adui wa taifa letu siyo ufisadi na mafisadi bali ni mfululizo wa uongozi mbovu usio na akili mpya wala mawazo ya kuona nje ya mipaka yetu na kujifunza kutoka kwa waliopiga hatua. Ufisadi ni matokeo ya hali hii na JPM haonekani kuwa na mbinu au uwezo wa kuibadilisha. Sanasana anachagua ufisadi gani wa kupambana nao na mwingine anauacha kwa hofu.
ADUI WA NCHI YETU KWA SASA NAMBA MOJA NI UFSADI UKISHA MALIZA UFSAD NA RUSHWA NCHI INAKUA SAWA LAKINI BILA KUONDOA UFSADI HATA UPANGE MIKAKATI YA MAENDELEO UNAFANYA BURE HELA ZA SERIKALI ZITAISHIA MIKONONI MWA WATU WACHACHE JPM KAZAA BUTI MAFSAD LAZIMA WANYOOKE
 
Wewe unadhani kwanini tunahama labda tuanzie hapo.Mambo ya elimu na umri sidhani kama yatakusaidia sana, mfano nikisema tulicheza na your father nitakuwa sijakujibu bado utataka kudadisi zaidi
Kwamba umecheza na baba yangu au la hainihusu kwa sababu mliamua wenyewe kucheza. Msingi wa kupinga habari ya kuhama ni kwamba kama ilivyo kawaida ya Magufuli anaamua tu mambo kienyeji na kiholela kutokana na kutokuwa na kipaji au uwezo wa kuwa kiongozi.
Nadhani wengi wenu mnadhani kuhamishia serikali Dodoma ni kama kutoka sebuleni na kwenda chumbani nyumbani kwako. Dodoma haijawahi kuandaliwa kuwa mji mkuu; hakuna miundombinu ya kutosha, hakuna makazi ya kutosha, hakuna shule wala hospitali za kutosha, wizara nyingi hazijajenga maofisi kule, hakuna nchi yeyote yenye ofisi ya ubalozi Dodoma, uwanja wa ndege ni kioja tu, na mengineyo mengi.
Mfano, kuna madereva chungu mbovu wa mawizara na taasisi za serikali. Fikiri dereva aliyejinyima akajenga nyumba yake na familia yake Chanika au Mbagala leo unamhamishia Dodoma; ataishi wapi kule?
Msiwe wepesi kumtukuza tu Magufuli, muwe mnachunguza mambo yake pia, anaipeleka nchi shimoni hii.
 
Back
Top Bottom