Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,243
Reaction score
44,520
Labda wengine mmeshaliona hili:


My Take: Sasa kama ni kweli wanafikiria hili au wanaamini hili basi bila ya shaka wanatufikiria sisi sote akili zetu ziko kwenye chupa. Hivi kweli video zote hizi zimewekwa slow motion? Seriously? Inawezekana Lowassa hana matatizo makubwa ya kiafya kama inavyohisiwa na baadhi ya watu lakini kusema kuwa video zimefojiwa ili kumfanya aonekane dhaifu zaidi nadhani si kutendea haki watu wengine. Kuna njia moja ya uhakika pkuondoa wasiwasi huu.





 
Bahati mbaya, ndugu yangu malihoja nakufahamu vizuri sana. huu ni mwendelezo wako wa kujifanya unafikiri juu ya vichwa vya watu wengine. hivi una mamlaka gani ya kutupa maelekezo kana kwamba tuna fikra zinazofanana kwa huyo mtu wako mgonjwa kweli? hivi unaweza kutoka na akili timamu na kupinga kuumwa kwa huyo mzee hata kama si kwa kiwango hicho unachofikiri wewe? mbona hamtuamibii kwamba mpaka sasa ameshaanguka mara ngapi badala yake unakuja na suala la slow motion? unadhani atakusadia katika mkakati wako wa kugombea ubunge kule kwenu? kuna jambo moja tu linakuja nalo haliko mbali sana, ambapo mtakaa kama watoto yatima.
 
Kila mtanzania anaumwa...tofauti ni kiwango cha uuguaji, Lowassa hata kama anaumwa maradhi yake hayamfanyi asiwe Rais, Mbona kuna kiongozi mkubwa tu ana kifafa? na tulimchagua sisi wenyewe? hizi team za Urais sasa zitatupeleka pabaya sana.
 
Na ile live event iliyokuwa inarushwa pale Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati akitangaza nia nayo ilifanyiwa "slow motion"? Kila mtu alishuhudia jinsi viungo vya mzee visivyopatana; kila kimoja kikitenda jinsi kipendavyo pasi na "central command".
 
Lowassa ni mgonjwa wa kutupwa, hata wasemeje ukweli ndiyo huo.
 

1) Mbona wao hawatupi au kusambaza hizo ambazo hazina slow motion? Kama hizo video ziko edited, wasambaze wao basi ambazo ni original.

2) Na video itakuaje edited kwenye vitendo tu halafu sauti isiwe edited? si maneno yatapishana na vitendo?

3) Inawezekanaje wanaonekana watu wawili kisha mmoja akawekewa slow motion mwingine asiwekewe na wote tunawaona pamoja kwa wakati huohuo mmoja? Editing ya wapi hiyo?
 
Tatizo kubwa kwa sasa hivi kuna "vita".....na katika vita kitu cha kwanza "kuangamia" au "kuangamizwa" ni UKWELI. Inaweza kuwa vigumu sana kujua ukweli wa suala hili.

Hivi kama nchi hatuna sheria ya kuwataka wagombea kupata clean bill ya afya kabla ya kukubaliwa kugombea. Hii ingeweza kuondoa utata....wote wapimwe afya zao na wale ambao hawatimizi vigezo vya kiafya tunaweka pembeni.

Nilimsikia EL mwenyewe akitaka hili lifanyike....inawezekana kuna vitu anajua kuhusu wapinzani wake ambavyo sisi wengine hatuvijui?
 
Kila mtanzania anaumwa...tofauti ni kiwango cha uuguaji, Lowassa hata kama anaumwa maradhi yake hayamfanyi asiwe Rais, Mbona kuna kiongozi mkubwa tu ana kifafa? na tulimchagua sisi wenyewe? hizi team za Urais sasa zitatupeleka pabaya sana.
Umebakiza hatua moja tu ya kusema 'kila mtanzania ni fisadi.....tofauti ni kiwango cha ufisidi..." I love Bongo
 
Lowasa anaumwa hata ukimwangalia usoni tu anaonyesha dalili ya kutaka tiba ya kimwili na kiroho.
 

Kwenye sheria za kazi huu ubaguzi unaruhusiwa? Ni waathirika wangapi wa ukimwi wako makazini na hawajabaguliwa sembuse ugonjwa wa kutetemeka?
 
Kila mtanzania anaumwa...tofauti ni kiwango cha uuguaji, Lowassa hata kama anaumwa maradhi yake hayamfanyi asiwe Rais, Mbona kuna kiongozi mkubwa tu ana kifafa? na tulimchagua sisi wenyewe? hizi team za Urais sasa zitatupeleka pabaya sana.

UMENIKUMBUSHA kuna siku kweli huyo mgonjwa wa kifafa alianguka jukwaani. na baadae tena tukaskia ameugua busha
 
Kwenye sheria za kazi huu ubaguzi unaruhusiwa? Ni waathirika wangapi wa ukimwi wako makazini na hawajabaguliwa sembuse ugonjwa wa kutetemeka?
Ndio maana nikauliza kama tunayo sheria ili tuache kuongozwa na hisia.

Kama vipo vigezo vya mtu kuitwa "mwenye afya" inayotosha kuwa Rais, tutumie vigezo hivyo hivyo kwa wote ili kuwa fair. Tunaweza kuona mtu "anatetemeka" lakini hao wengine wakawa na magonjwa hatari zaidi. Njia pekee ni kupima kama "afya" ndio kigezo pekee cha kutusaidia kuchuja!

Lakini yote kwa yote, ni muda tu utaamua. Tatizo la nchi hii ni system sio mtu.....tuondoe hii inayoitwa CCM ili tuweze kutoka hapa tulipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…