Hili tangazo ITV sio zuri

Hili tangazo ITV sio zuri

MAHEPE

Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
88
Reaction score
30
Kuna Tangazo linatoka ITV la TMT linalosema mpaka utusue, mpaka kieleweke, mpaka ukome. Sasa hili neno 'mpaka utusue' maana yake nini? Kwa sisi wa miaka hiyo, hili neno lina maana mbaya, na ubaya tangazo hili mpaka watoto wanaangalia.

Ni vizuri ITV wakasitisha tangazo hili mara moja.
 
Nini maana ya kutusua? Tukishapata maana halisi ya neno hili tujadili.Vinginevyo zitakuwa mis-interpretation tu.
 
Teh.. teh.. teh.. neno utusue limenikumbusha mbali sana kwa waliozaliwa zamani lilikuwa na tafsiri ya jambo la faragha baina ya watu ya watu wenye jinsia mbili tofauti. Labda kwa sababu siku hizi mambo yote hadharani ndiyo maana tangazo hilo limeruhusiwa na hasa ukikuta Mhariri wa matangazo ni kijana mwenye hulka hiyo. Ngoja tusubiri wenyewe wanakuja tusikie watakavyolidadavua neno hilo.
 
ushasema wewe wa miaka hyo tena una sema watoto wanaangalia

kma miaka hyo ulikua na maana nyingine sio miaka hii
 
Hata neno "kichwa" linaweza kuwa na maana mbaya kwa utavyolitumia.

Mimi nijuavyo enzi zetu "kutusua" ilikuwa kustarehe. Kula raha kwenye shida. Vijana wa siku hizo tulikuwa tunaenda kutusua mpaka saa 9 za usiku huko Afrikana halafu haturudi nyumbani tunawahi foleni ya sukari.
 
Kutusua ni kama kutoka kimaisha/kufanikiwa leo ndiyo nimejua zamani lilikuwa na maana tofauti.
 
Kutusua maana yake ni kutoboa
jamaa kaondoka na Mwanamke kenda mTusua
 
Kutusua enzi zetu maana yake ni kunyofoa nyama toka kwa mfupa ama nyama kubwa kwa kutumia meno ili ule vipande vidogo vidogo. Kama washika nyama kwa mkono unatusua kwa meno ya mbele kwa kuila mpaka inaisha.
 
Kunionesha "typo" ndiyo imekuwa ya "uso".

Amma kweli, mapunguani JF ni wengi.
Nilitegemea hali hii itaendelea kukutokea na itaendelea kuwa hivi hatua kwa hatua. Kwa ujumla inatokana na hicho kilemba cha upuuzi ulichojimbanua nacho. Pole bidada ni malezi yanakutesa.
 
maneno ya mtaani huwa ni mapya kabisa au ya zamani yaliyopewa maana mpya au yaliyopo yakapewa maana mpya. Kwa hiyo hilo la kwako limepewa maana mpya na vijana watumiaji wa sasa. We enzi zako zimeshapita ndo maana unaona ni tusi. Kwa kuwa haliko kwenye kamusi ya kiswahili sanifu, ITV hawana ushahidi kuwa hilo ni tusi. MImi na miaka yangu 40 ndo nimelisikia ITV kwa mara ya kwanza.
 
Nilitegemea hali hii itaendelea kukutokea na itaendelea kuwa hivi hatua kwa hatua. Kwa ujumla inatokana na hicho kilemba cha upuuzi ulichojimbanua nacho. Pole bidada ni malezi yanakutesa.

Wewe itakuwa katika ile listi ya watoto wa mama uliyesahauliwa. Ambao kila mwanamme ajae kwao huambiwa "mwamkie baba'ko".
 
ndugu umesahau Kiswahili O-LEVEL kuwa kuna ukuaji wa lugha. Ndani yake ndio kuongezeka kwa misamiati kama "Tusua"
 
Back
Top Bottom