jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Wanajamvi, hili suala la vipimo vya Corona, hata Marekani wanapambana kuhakikisha vinapatikana nchi nzima kadri ya mahitaji. Trump yeye alilalamikiwa kwa kuzikataa zile walizotoa W.H.O hapo awali.
Lakini leo nimemsikia Waziri Mkuu (na juzi Ummy), akisema sample za wanaohisiwa kuwa na Virusi vya Corona zinachukuliwa hospital zilizoko maeneo ya karibu na airports kutoka kwa washukiwa, na kusafirishwa kwenda Dar kufanyiwa vipimo vya Corona. Mfano yule mama wa Arusha ilichukuwa siku tatu! Hatua zinazochukuliwa sasa hivi ni kama patapotea tu. Mara sijui guest house inafungwa na Dereva taxi na familia yake wanatafutwa, as if wako na bidhaa za wizi!
Sasa najiuliza upatikanaji wa vifaa vya kufanya vipimo hivyo ndo umeleta hii shida au ni sisi tulijiamulia kuwa kifaa kimoja tu kinatosha? Kwanini hatukuanza na kuhakikisha kila hospital aliyoitaja waziri mkuu inakuwa na uwezo huo?
Kwasababu nimeona kama vile serikali inakuwa reactive badala ya kuwa proactive. Yaani mpaka malalamiko yazidi ndo hatua inachukuliwa. Na sasa ile tabia ya kudharau ushauri unaotolewa pengine kutokana na itikadi zetu inatakiwa iachwe mara moja. Mfano kuhusu hoja nzuri tu ya Msigwa kule bungeni ya kutaka bunge lijadili suala la Corona ilipozimwa huku ile ya kutaka Zitto auawe ikipigiwa meza, makofi na vigelegele.
Kwa sasa hivi Europe wanataka kupiga kura ili kufunga mipaka yao. Mataifa haya makubwa lazima chumi zao zitayumba na wamejiandaa kwa hilo. Sisi hatuna ujanja zaidi ya kuchukua tahadhari ili tusipoteze maisha ya wananchi kizembe. Halafu tujiandae kwa changamoto ya kiuchumi.
Kitu kinachosababisha panic ni kuchelewa kuchukua hatua. Marekani panic imekuwa kubwa kiasi kwamba kuna wanaoamini ni mwisho wa dunia nk. Lakini cha msingi hapa, ni kwamba bidhaa nyingi muhimu hazipatikani tena kwenye supermarkets. Hata vyakula watu wamerundika nyumbani. Lakini wale tuliowacheka, bahati yetu itakuwa pale tu hili janga litakapoanza kupungua makali. Yaani kuwepo na sufuri kwenye ripoti ya wagonjwa na wale wanaopoteza maisha. Kwasababu ni wazi uzalishaji na upatikanaji wa baadhi ya bidhaa utapungua, na uwezekano wa serikali kulazimisha rationing. Hilo lilishawahi kutokea kwenye sukari.
Serikali itambuwe kwamba kuchukua hatua mapema kutasaidia siyo tu kuokoa maisha, bali pia na uchumi wetu. Nchi ya Italia ambao pia tunawategemea kwa utalii, wamefunga mipaka yao. Na wao pia wanajilaumu kwa kuchelewa kuchukua hatua. Sisi tulitakiwa tujifunze na siyo kuhisi kwamba tuko immune kwasababu ya hizo habari kwamba virusi hivyo haviishi kwa muda mrefu kwenye miale ya jua na joto kali. Hata kama ikiwa hilo ni kweli, bado kutakuwepo na uambukizaji, hapo kwa rate ya chini.
Nashauri serikali iongeze vifaa vya kupima Corona, na kila anayeingia kuzuiwa kwa siku 14 ndipo waruhusiwe hata kama wamepima na kukutwa hawana. Nilimsikia Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiongelea kuwazuia walioko guest bila kutaja muda watakaowazuia. Ni vyema viongozi hao wakawa busy kujifunza kuhusu janga hili la dunia badala ya kuhangaika na upinzani.
Pia ni wakati wa kuwa activate vile vikosi vyetu vinavyoshughulika na majanga. Ni wakati wa kulinda Taifa na siyo chama fulani peke yake. Marekani wao wameanza kuwa deploy wale national guards. Hata mapolisi tunao wengi sana na wanatafuna kodi zetu tu wapewe kazi kwenye hili janga la Corona, mfano traffic police. Na pia JKT kutengeneza vitanda vya wagonjwa na pengine kambi nk.