Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,775
Huyu kijana ambae ni kaka mshikaji kiaina kwa sasa baba yake alikua mfanya biashara. Biashara ilianza kunenepa wakati wa awamu wa pili, awamu ya tatu biashara ilikua nzuri kiasi ambacho msure aliamua kijana akasome nje baada ya six.
Alisoma first degree huko nchi za wenzetu. Akiwa mwaka wa pili katika masomo yake, hali ya afya ya mzee ilianza kuzorota. Akiwa kama mtoto mkubwa ilibidi arudi nyumbani. Amerudi Masters ilibidi aingie UDSM. Wakati yuko pale alikutana na mdada mmoja, baba yake akiwa waziri wa awamu ya nne. Mdada alibabaika na swaga za mamtoni za jamaa.
Mtaani kuna binti amemaliza six nae anamzimikia kaka vibaya sana mshikaji akawa anajipoza akija home lakini roho yake yote ilikuwa kwa mtoto wa waziri ambae alishampeleka mpaka kwao.
Wakati anafanya research yake alikuwa nyumbani muda mwingi, baba yake alimshauri kheri aoe kwakua ndiye kijana mkubwa na baba alisema kama sitaona wajukuu zangu angalau nishuhudie harusi yako, kama unavyoona afya yangu inaleta matata.
Lile wazo lilimuingia kijana. Amerudi Dar akaanza kumtafuta mpenzi, alipropose moja kwa moja. Binti kwa dharau sana alimwambia, khe wewe vipi, zaidi ya hivyo vi nguo, sijui simu, na laptop una nini cha maana, unaweza kunitunza mimi wewe? Kwa fedheha kaka wa watu aliondoka. Alirudi kwao weekend ile na kupropose kwa yule dada wa form six mtaani kwao. Kumbe mdada alikua anafunga na kusali lile jambo litokee.
Harusi ilikua nzuri kwani baba aliigharamia kwa uwezo wake wote, kijana alimaliza shule na kupata ajira nzuri. Alianza kumsomesha mke wake, mke yuko chuo bado anasoma, mtoto wa waziri analia anadai jamani ulikua ni utoto, mimi nina kazi yangu basi niko tayari kuzaa tu na wewe.