Hili ndilo tatizo la Zitto Kabwe

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
*HILI NDIO TATIZO LA ZITTO KABWE.*

Novemba 03, 2018

Jana Ijumaa Zitto Kabwe Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo amepata dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa siku 2.

Zitto alikamatwa kutokana na kauli zake kuwa Jeshi la Polisi limeua watu zaidi ya 100 katika mapigano huko Uvinza Kigoma. Katoa kauli hiyo akiwa hana ushahidi na yeye mwenyewe hakuwepo eneo la tukio.

Alitaka kuwaaminisha Watanzania na dunia nzima kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Jeshi la Polisi inaendesha mauaji ya watu wengi. Hizi sio tuhuma ndogo, zinawaogofya mataifa yote duniani na zaidi zinawaogofya Watanzania wenyewe kwa kutaka kujenga taswira kuwa Tanzania hakuna amani tena na kumetapakaa mauaji yanayofanywa na Serikali.

Tunatambua lengo la Zitto ni kuchochea chuki kwa wananchi ili waichukie Serikali na pengine watimize lengo lake la kuingia kwenye mapambano na vyombo vya dola.

Tunafahamu lengo la Zitto ni kuichonganisha Tanzania na mataifa ya nje kwa kuonesha sura mbaya inayothibitisha matakwa yake ya kisiasa kuwa uongozi uliopo madarakani haufai na unapaswa kuondolewa.

Kwa alipofikia Zitto Kabwe sasa hivi yeye ni mjuzi wa kila kitu na msemaji wa kila kitu.

Na hili ndilo kosa kubwa la Mwanasiasa huyu.

Zitto anajiona ana akili kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania, jana tu alipotoka ametoa kauli kuwa washiriki wa Kongamano la Chuo Kikuu ambalo Rais Magufuli alishiriki wana UKASUKU. Ana maana Maprofesa, Madaktari, Wasomi mbalimbali, wanafunzi na viongozi waliohudhuria kongamano hilo walikuwa wanachangia upuuzi kwamba angekuwepo yeye ndio angezungumza sawasawa.

Ana maana wale wote waliozungumza ni VILAZA yaani akina Prof. Mukandala, Prof Moshi, Prof. Mkumbo, Prof. Qorro, Prof. Shivji na wengine wengi.

Sasa hapa ndipo anapokosea Zitto. Anajiona yeye anajua kuliko mtu mwingine yeyote hapa Tanzania. Watu wana namna hii kamwe huwa hawafanikiwi na hili ndilo anguko la Zitto Kabwe.

Kutekwa kwa Mo Dewji alitoa kauli za dharau dhidi ya Polisi kana kwamba yeye ndio anajua ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao kuliko polisi wote wa nchi hii.

Kwenye korosho Zitto Kabwe ndio mtaalamu aliyebobea katika uzalishaji na masoko ya korosho kuliko mtu yeyote hapa Tanzania na yeye ndio mwenye haki miliki ya kutoa maelekezo ya namna gani zao hili liendeshwe.

Uchumi wa Tanzania, Zitto Kabwe ndio anajua kila kitu kuliko BOT, Wizara ya Fedha, wasomi, Mawaziri, Wabunge na wananchi wote wa Tanzania.

Sheria za Tanzania Zitto Kabwe ndiye anajua zaidi kuliko Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yake, Wabunge, Mawakili na kila mwananchi wa Tanzania.

Mahusiano ya kimataifa, Zitto Kabwe ndio mwenyewe. Hata nguli wa Diplomasia Balozi Augustine Mahiga haoni ndani. Na mengine mengimengi.

Tena sasa anatumia neno lake maarufu kuwaita watu wengine ni MAZWAZWA. Yaani Watanzania wote Mazwazwa isipokuwa yeye.

Naipongeza sana Serikali kwa hatua inazochukua dhidi ya mtu huyu, nampongeza Rais Magufuli kwa jinsi anavyosimamia msimamo wa kuwataka Watanzania wafanye kazi. Wapiga maneno wa aina ya Zitto Kabwe watatuchelewesha sana na kuwaendekeza ni sawa na kulikabidhi Taifa kwa wahuni.

Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata na natarajia atafunguliwa mashitaka ili athibitishe watu 100 waliouawa huko Uvinza Kigoma, vinginevyo afungwe gerezani kama wanavyofungwa Watanzania wengine wanaokutwa na hatia.

Akifingwa huyu tutapata muda wa kufanya kazi na zaidi tutakuwa tumemtimizia kiu yake ya kukamatwa na Polisi na kisha kufungwa maana kwa anayoyafanya ni dhahiri anataka kukamatwa na kufungwa ili apate umaarufu wa kisiasa na ndio maana alipotoka mahabusu kaanza kujifananisha na Nelson Mandela.

Amesahau kuwa Nelson Mandela alikuwa anapigania uhuru wa Afrika Kusini na yeye anapigania tumbo lake baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kubana mianya yake ya upigaji wa hela kupitia kamati ya Bunge. Amebaki kupokea hela za Wazungu wanaomfadhili aje avuruge Tanzania. Kwingine kumebana.

Aidha, Zitto anakosea sana kuweka juhudi nyingi za kutafuta kujijenga yeye binafsi kisiasa ilihali chama chake cha ACT kipo hoi taabani, wanachama wanamkimbia, viongozi wanamkimbia, amebaki na vijana wachache anaowatumia kujijenga. Lakini kiuhalisia hivi sasa anaendesha chama chake kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hajali hata kuwapigania wananchi wa Kigoma Mjini, bila shaka anatambua kuwa 2020 hatakuwa Mbunge kwa hiyo anafanya fujo za mwishomwisho na kukusanya fedha za Wazungu anaowadanganya kuwa upinzani wa Tanzania una uwezo wa kushika madaraka ya nchi katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Mwisho niseme kinachompata Zitto leo ni haki yake na anastahili. Kwa tulipofikia hakuna jema kwake. Kila kinachofanywa na Serikali ni kibaya na akilala akiamka anafikiria kuichafua nchi na kuichonganisha Serikali na wananchi. Naamini Serikali inaliona jambo hili na itaendelea kumdhibiti.

Mungu Ibariki Afrika.
Mungu Ibariki Tanzania.
 
kwan mpaka sasa ww unaamini lipi,kwamba walikufa wanne au 100?hivi hujiulizi kuwa had polisi zaid ya mmoja wanakufa kwny battle na RAIA madhara yake ni kuishia vifo vya watu wanne tu??mm simwamin yyte kat ya zito na jeshi la polisi,labda kama itaundwa tume huru kuchunguza na kutoa taarfa sahihi,hawa waliopishana kwny takwimu siwaamin wote,wote wanaweza kuwa sahihi au siyo sahihi
 
kwan mpaka sasa ww unaamini lipi,kwamba walikufa wanne au 100?hivi hujiulizi kuwa had polisi zaid ya mmoja wanakufa kwny battle na RAIA madhara yake ni kuishia vifo vya watu wanne tu??mm simwamin yyte kat ya zito na jeshi la polisi,labda kama itaundwa tume huru kuchunguza na kutoa taarfa sahihi,hawa waliopishana kwny takwimu siwaamin wote wote wanaweza kuwa sahihi au siyo sahihi

Yeye anauona uongo na mapungufu ya Zitto lakini wakati huo huo anawaamini watu ambao wana historia ya kusema uongo hadharani. Anamkosoa Zitto kwa ujuaji lakini wakati huo huo anatutajia watu anaoamini kila wakisemacho au wakifanyacho ni sahihi siku zote.
Watu wengine bwana!
 
Tatzo la Zitto yeye anaongea, wengine tunakaa zetu kimnya. Kwa hiyo kwa akili zako ule ulikua mdahalo? Au amefanya kuwatumia maprofesa wamsifie mbele ya media basi! Na kwa nini serikal inatumia nguvu nyingi kutuambia ilichofanya, hofu ya nn? Mara kongamano mara vipindi tunatekeleza; Kwan sisi hatuoni? Watu wanaokotwa kwenye viroba hatuoni? Watumishi sio mishahara wala madaraja kuongezwa kwan hawajui? Watu kutekwa si kila mtu anatembea na roho mkononi, hata bashe wa ccm alitekwa? Watu kupigwa risasi na vyombo vyake (akwilina) hatuoni? Watu kushambuliwa kwa risasi mbele ya vyombo na macctv kwan hatuoni? Maprofesa wa Tanzania wanaendeshwa na tumbo sio wa kuwapa credibility yoyote mtu kama kabudi kwa sasa hawezi kuongea ukamwambia mtu eti anaeongea n proffesa !
 
Naamini kabisa kama Zitto angekuwepo hapo akapata nafasi ya kuongea asingepindisha maneno.
 
Zitto najiona ana akili kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania
Sidhani kama Watanzania wanamchukulia ZZK kama ulivomuelezea kwenye huu mstari nilio u quote. Inawezekana Zito anajua mambo mengi sio kwa sababu ya uhitimu wake wa Shahada ya Uzamili katika Uchumi bali ni bidii yake ya kujifunza mambo mengi, ku interact na watu wa kada mbalimbali za kimaisha, kiutamaduni na kielimu wa ndani na nje ya nchi(exposure) na huko sio kujifanya unajua kilakitu

On the contrary Watanzania wanamjua ni nani katika nchi hii anayejifanya anajua kila kitu japo kwa hakika ni mtu aliyekua nyuma sana kiustaarabu, mshamba na na limbukeni wa vitu viingi sana( exposure ni ziro) ingawa mwenyewe hajui kama hajui
 
kiukweli tz hatuna mazwazwa wengi kiasi cha zitto anavyosema isipokuwa watu wengi hasa wasomi wanashindwa kutoa maoni yao halisi kwa sababau za ukosefu wa ujasiri na ndio maana toka awamu hii ya 5 ianze zitto mwana wa kabwe anaonekana kujua kila kitu
 
*HILI NDIO TATIZO LA ZITTO KABWE.*

Novemba 03, 2018

Jana Ijumaa Zitto Kabwe Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo amepata dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa siku 2.

Zitto alikamatwa kutokana na kauli zake kuwa Jeshi la Polisi limeua watu zaidi ya 100 katika mapigano huko Uvinza Kigoma. Katoa kauli hiyo akiwa hana ushahidi na yeye mwenyewe hakuwepo eneo la tukio.

Alitaka kuwaaminisha Watanzania na dunia nzima kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Jeshi la Polisi inaendesha mauaji ya watu wengi. Hizi sio tuhuma ndogo, zinawaogofya mataifa yote duniani na zaidi zinawaogofya Watanzania wenyewe kwa kutaka kujenga taswira kuwa Tanzania hakuna amani tena na kumetapakaa mauaji yanayofanywa na Serikali.

Tunatambua lengo la Zitto ni kuchochea chuki kwa wananchi ili waichukie Serikali na pengine watimize lengo lake la kuingia kwenye mapambano na vyombo vya dola.

Tunafahamu lengo la Zitto ni kuichonganisha Tanzania na mataifa ya nje kwa kuonesha sura mbaya inayothibitisha matakwa yake ya kisiasa kuwa uongozi uliopo madarakani haufai na unapaswa kuondolewa.

Kwa alipofikia Zitto Kabwe sasa hivi yeye ni mjuzi wa kila kitu na msemaji wa kila kitu.

Na hili ndilo kosa kubwa la Mwanasiasa huyu.

Zitto anajiona ana akili kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania, jana tu alipotoka ametoa kauli kuwa washiriki wa Kongamano la Chuo Kikuu ambalo Rais Magufuli alishiriki wana UKASUKU. Ana maana Maprofesa, Madaktari, Wasomi mbalimbali, wanafunzi na viongozi waliohudhuria kongamano hilo walikuwa wanachangia upuuzi kwamba angekuwepo yeye ndio angezungumza sawasawa.

Ana maana wale wote waliozungumza ni VILAZA yaani akina Prof. Mukandala, Prof Moshi, Prof. Mkumbo, Prof. Qorro, Prof. Shivji na wengine wengi.

Sasa hapa ndipo anapokosea Zitto. Anajiona yeye anajua kuliko mtu mwingine yeyote hapa Tanzania. Watu wana namna hii kamwe huwa hawafanikiwi na hili ndilo anguko la Zitto Kabwe.

Kutekwa kwa Mo Dewji alitoa kauli za dharau dhidi ya Polisi kana kwamba yeye ndio anajua ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao kuliko polisi wote wa nchi hii.

Kwenye korosho Zitto Kabwe ndio mtaalamu aliyebobea katika uzalishaji na masoko ya korosho kuliko mtu yeyote hapa Tanzania na yeye ndio mwenye haki miliki ya kutoa maelekezo ya namna gani zao hili liendeshwe.

Uchumi wa Tanzania, Zitto Kabwe ndio anajua kila kitu kuliko BOT, Wizara ya Fedha, wasomi, Mawaziri, Wabunge na wananchi wote wa Tanzania.

Sheria za Tanzania Zitto Kabwe ndiye anajua zaidi kuliko Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yake, Wabunge, Mawakili na kila mwananchi wa Tanzania.

Mahusiano ya kimataifa, Zitto Kabwe ndio mwenyewe. Hata nguli wa Diplomasia Balozi Augustine Mahiga haoni ndani. Na mengine mengimengi.

Tena sasa anatumia neno lake maarufu kuwaita watu wengine ni MAZWAZWA. Yaani Watanzania wote Mazwazwa isipokuwa yeye.

Naipongeza sana Serikali kwa hatua inazochukua dhidi ya mtu huyu, nampongeza Rais Magufuli kwa jinsi anavyosimamia msimamo wa kuwataka Watanzania wafanye kazi. Wapiga maneno wa aina ya Zitto Kabwe watatuchelewesha sana na kuwaendekeza ni sawa na kulikabidhi Taifa kwa wahuni.

Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata na natarajia atafunguliwa mashitaka ili athibitishe watu 100 waliouawa huko Uvinza Kigoma, vinginevyo afungwe gerezani kama wanavyofungwa Watanzania wengine wanaokutwa na hatia.

Akifingwa huyu tutapata muda wa kufanya kazi na zaidi tutakuwa tumemtimizia kiu yake ya kukamatwa na Polisi na kisha kufungwa maana kwa anayoyafanya ni dhahiri anataka kukamatwa na kufungwa ili apate umaarufu wa kisiasa na ndio maana alipotoka mahabusu kaanza kujifananisha na Nelson Mandela.

Amesahau kuwa Nelson Mandela alikuwa anapigania uhuru wa Afrika Kusini na yeye anapigania tumbo lake baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kubana mianya yake ya upigaji wa hela kupitia kamati ya Bunge. Amebaki kupokea hela za Wazungu wanaomfadhili aje avuruge Tanzania. Kwingine kumebana.

Aidha, Zitto anakosea sana kuweka juhudi nyingi za kutafuta kujijenga yeye binafsi kisiasa ilihali chama chake cha ACT kipo hoi taabani, wanachama wanamkimbia, viongozi wanamkimbia, amebaki na vijana wachache anaowatumia kujijenga. Lakini kiuhalisia hivi sasa anaendesha chama chake kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hajali hata kuwapigania wananchi wa Kigoma Mjini, bila shaka anatambua kuwa 2020 hatakuwa Mbunge kwa hiyo anafanya fujo za mwishomwisho na kukusanya fedha za Wazungu anaowadanganya kuwa upinzani wa Tanzania una uwezo wa kushika madaraka ya nchi katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Mwisho niseme kinachompata Zitto leo ni haki yake na anastahili. Kwa tulipofikia hakuna jema kwake. Kila kinachofanywa na Serikali ni kibaya na akilala akiamka anafikiria kuichafua nchi na kuichonganisha Serikali na wananchi. Naamini Serikali inaliona jambo hili na itaendelea kumdhibiti.

Mungu Ibariki Afrika.
Mungu Ibariki Tanzania.
Unareport kutoka Lumumba street nn?
 
Back
Top Bottom