Hili ndilo tatizo la Zitto Kabwe

Hili ndilo tatizo la Zitto Kabwe

Ushajipatia ya kwenda kunywa ka serengeti badae uku una angalia mechi ya liverpool na arsenal
 
*HILI NDIO TATIZO LA ZITTO KABWE.*

Novemba 03, 2018

Jana Ijumaa Zitto Kabwe Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo amepata dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa siku 2.

Zitto alikamatwa kutokana na kauli zake kuwa Jeshi la Polisi limeua watu zaidi ya 100 katika mapigano huko Uvinza Kigoma. Katoa kauli hiyo akiwa hana ushahidi na yeye mwenyewe hakuwepo eneo la tukio.

Alitaka kuwaaminisha Watanzania na dunia nzima kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Jeshi la Polisi inaendesha mauaji ya watu wengi. Hizi sio tuhuma ndogo, zinawaogofya mataifa yote duniani na zaidi zinawaogofya Watanzania wenyewe kwa kutaka kujenga taswira kuwa Tanzania hakuna amani tena na kumetapakaa mauaji yanayofanywa na Serikali.

Tunatambua lengo la Zitto ni kuchochea chuki kwa wananchi ili waichukie Serikali na pengine watimize lengo lake la kuingia kwenye mapambano na vyombo vya dola.

Tunafahamu lengo la Zitto ni kuichonganisha Tanzania na mataifa ya nje kwa kuonesha sura mbaya inayothibitisha matakwa yake ya kisiasa kuwa uongozi uliopo madarakani haufai na unapaswa kuondolewa.

Kwa alipofikia Zitto Kabwe sasa hivi yeye ni mjuzi wa kila kitu na msemaji wa kila kitu.

Na hili ndilo kosa kubwa la Mwanasiasa huyu.

Zitto anajiona ana akili kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania, jana tu alipotoka ametoa kauli kuwa washiriki wa Kongamano la Chuo Kikuu ambalo Rais Magufuli alishiriki wana UKASUKU. Ana maana Maprofesa, Madaktari, Wasomi mbalimbali, wanafunzi na viongozi waliohudhuria kongamano hilo walikuwa wanachangia upuuzi kwamba angekuwepo yeye ndio angezungumza sawasawa.

Ana maana wale wote waliozungumza ni VILAZA yaani akina Prof. Mukandala, Prof Moshi, Prof. Mkumbo, Prof. Qorro, Prof. Shivji na wengine wengi.

Sasa hapa ndipo anapokosea Zitto. Anajiona yeye anajua kuliko mtu mwingine yeyote hapa Tanzania. Watu wana namna hii kamwe huwa hawafanikiwi na hili ndilo anguko la Zitto Kabwe.

Kutekwa kwa Mo Dewji alitoa kauli za dharau dhidi ya Polisi kana kwamba yeye ndio anajua ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao kuliko polisi wote wa nchi hii.

Kwenye korosho Zitto Kabwe ndio mtaalamu aliyebobea katika uzalishaji na masoko ya korosho kuliko mtu yeyote hapa Tanzania na yeye ndio mwenye haki miliki ya kutoa maelekezo ya namna gani zao hili liendeshwe.

Uchumi wa Tanzania, Zitto Kabwe ndio anajua kila kitu kuliko BOT, Wizara ya Fedha, wasomi, Mawaziri, Wabunge na wananchi wote wa Tanzania.

Sheria za Tanzania Zitto Kabwe ndiye anajua zaidi kuliko Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yake, Wabunge, Mawakili na kila mwananchi wa Tanzania.

Mahusiano ya kimataifa, Zitto Kabwe ndio mwenyewe. Hata nguli wa Diplomasia Balozi Augustine Mahiga haoni ndani. Na mengine mengimengi.

Tena sasa anatumia neno lake maarufu kuwaita watu wengine ni MAZWAZWA. Yaani Watanzania wote Mazwazwa isipokuwa yeye.

Naipongeza sana Serikali kwa hatua inazochukua dhidi ya mtu huyu, nampongeza Rais Magufuli kwa jinsi anavyosimamia msimamo wa kuwataka Watanzania wafanye kazi. Wapiga maneno wa aina ya Zitto Kabwe watatuchelewesha sana na kuwaendekeza ni sawa na kulikabidhi Taifa kwa wahuni.

Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata na natarajia atafunguliwa mashitaka ili athibitishe watu 100 waliouawa huko Uvinza Kigoma, vinginevyo afungwe gerezani kama wanavyofungwa Watanzania wengine wanaokutwa na hatia.

Akifingwa huyu tutapata muda wa kufanya kazi na zaidi tutakuwa tumemtimizia kiu yake ya kukamatwa na Polisi na kisha kufungwa maana kwa anayoyafanya ni dhahiri anataka kukamatwa na kufungwa ili apate umaarufu wa kisiasa na ndio maana alipotoka mahabusu kaanza kujifananisha na Nelson Mandela.

Amesahau kuwa Nelson Mandela alikuwa anapigania uhuru wa Afrika Kusini na yeye anapigania tumbo lake baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kubana mianya yake ya upigaji wa hela kupitia kamati ya Bunge. Amebaki kupokea hela za Wazungu wanaomfadhili aje avuruge Tanzania. Kwingine kumebana.

Aidha, Zitto anakosea sana kuweka juhudi nyingi za kutafuta kujijenga yeye binafsi kisiasa ilihali chama chake cha ACT kipo hoi taabani, wanachama wanamkimbia, viongozi wanamkimbia, amebaki na vijana wachache anaowatumia kujijenga. Lakini kiuhalisia hivi sasa anaendesha chama chake kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hajali hata kuwapigania wananchi wa Kigoma Mjini, bila shaka anatambua kuwa 2020 hatakuwa Mbunge kwa hiyo anafanya fujo za mwishomwisho na kukusanya fedha za Wazungu anaowadanganya kuwa upinzani wa Tanzania una uwezo wa kushika madaraka ya nchi katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Mwisho niseme kinachompata Zitto leo ni haki yake na anastahili. Kwa tulipofikia hakuna jema kwake. Kila kinachofanywa na Serikali ni kibaya na akilala akiamka anafikiria kuichafua nchi na kuichonganisha Serikali na wananchi. Naamini Serikali inaliona jambo hili na itaendelea kumdhibiti.

Mungu Ibariki Afrika.
Mungu Ibariki Tanzania.
mzee siyo kukubaliana na kila jambo hata kwenye upuuzi, jifunze kuhoji na kusimamia ukweli.
 
Je wewe unaemtuhumu zito asie na ushahidi wa mauaji ya watu 100 unao ushahidi wa zito kupewa hela na wazungu ili avuruge amani Tanzania? Kama huna basi wewe ni kama zito mnaongea bila ushahidi.Halafu siasa za kigoma waachie wanakigoma wao ndio wanaotakiw waseme zito hawasaidii kitu sio kazi yako.
 
Nchi hii Ukijua sheria mtu akuonei, na woga unakuwa una zitto ni miongoni atawasumbua na mahakamani atashinda na ajua kujenga hoja
Wamesahau ya yule aliemnyooshea zito mkono kisha mkono ukachinjwa na tume ya mwakyembe ikaja kuonesha ukweli.Hivi zito akiiomba mahakama iuende kajopo kadogo kakahoji huko kijijini nini kiyajiri
 
Kama hujasoma USISOME
Nimemsoma hapo anaposema kuhusu ma Prof na madokta akimaanisha wao ndio wanaojua sana na ZZK sio lolote.

Anasahau kusema lolote kuhusu mkuu wake kuiponda ripoti ya Professor kwasababu tu ripoti haikutoka kama anavyopenda.
 
Yaani nikisoma hili bandiko kama nakuona unataka kulia kisa ZZK anajua vitu vingi kuliko watawala.

mkuu kama ulisikia lile kongamano sema ukweli prof. palamagamba aliongea nini cha maana au prof. moshi

ukweli ZZK anajua, nao walijua atawalaza na viatu wakamshikiria kwa muda
 
Mjomba wakati fulani alipata kunambia kwa zipo nyakati ambazo mwanadamu anaweza akaishi bila UBONGO awali sikuamini.
Lakini kwa andiko lako hili sasa naamini kabisa maneno ya Mjomba angu ......wewe medula huna
 
Ujinga unaanza kuamini kuwa Mtu akiwa Profesa ama dkt hawezi kuwa mjinga tena. Ujinga una namna na kila mtu ana ujinga wake. Hivyo usishangae kabisa kundi kuonekana linawasomi wengi lakini bado likawa na wajinga wengi.
 
*HILI NDIO TATIZO LA ZITTO KABWE.*

Novemba 03, 2018

Jana Ijumaa Zitto Kabwe Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo amepata dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa siku 2.

Zitto alikamatwa kutokana na kauli zake kuwa Jeshi la Polisi limeua watu zaidi ya 100 katika mapigano huko Uvinza Kigoma. Katoa kauli hiyo akiwa hana ushahidi na yeye mwenyewe hakuwepo eneo la tukio.

Alitaka kuwaaminisha Watanzania na dunia nzima kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Jeshi la Polisi inaendesha mauaji ya watu wengi. Hizi sio tuhuma ndogo, zinawaogofya mataifa yote duniani na zaidi zinawaogofya Watanzania wenyewe kwa kutaka kujenga taswira kuwa Tanzania hakuna amani tena na kumetapakaa mauaji yanayofanywa na Serikali.

Tunatambua lengo la Zitto ni kuchochea chuki kwa wananchi ili waichukie Serikali na pengine watimize lengo lake la kuingia kwenye mapambano na vyombo vya dola.

Tunafahamu lengo la Zitto ni kuichonganisha Tanzania na mataifa ya nje kwa kuonesha sura mbaya inayothibitisha matakwa yake ya kisiasa kuwa uongozi uliopo madarakani haufai na unapaswa kuondolewa.

Kwa alipofikia Zitto Kabwe sasa hivi yeye ni mjuzi wa kila kitu na msemaji wa kila kitu.

Na hili ndilo kosa kubwa la Mwanasiasa huyu.

Zitto anajiona ana akili kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania, jana tu alipotoka ametoa kauli kuwa washiriki wa Kongamano la Chuo Kikuu ambalo Rais Magufuli alishiriki wana UKASUKU. Ana maana Maprofesa, Madaktari, Wasomi mbalimbali, wanafunzi na viongozi waliohudhuria kongamano hilo walikuwa wanachangia upuuzi kwamba angekuwepo yeye ndio angezungumza sawasawa.

Ana maana wale wote waliozungumza ni VILAZA yaani akina Prof. Mukandala, Prof Moshi, Prof. Mkumbo, Prof. Qorro, Prof. Shivji na wengine wengi.

Sasa hapa ndipo anapokosea Zitto. Anajiona yeye anajua kuliko mtu mwingine yeyote hapa Tanzania. Watu wana namna hii kamwe huwa hawafanikiwi na hili ndilo anguko la Zitto Kabwe.

Kutekwa kwa Mo Dewji alitoa kauli za dharau dhidi ya Polisi kana kwamba yeye ndio anajua ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao kuliko polisi wote wa nchi hii.

Kwenye korosho Zitto Kabwe ndio mtaalamu aliyebobea katika uzalishaji na masoko ya korosho kuliko mtu yeyote hapa Tanzania na yeye ndio mwenye haki miliki ya kutoa maelekezo ya namna gani zao hili liendeshwe.

Uchumi wa Tanzania, Zitto Kabwe ndio anajua kila kitu kuliko BOT, Wizara ya Fedha, wasomi, Mawaziri, Wabunge na wananchi wote wa Tanzania.

Sheria za Tanzania Zitto Kabwe ndiye anajua zaidi kuliko Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yake, Wabunge, Mawakili na kila mwananchi wa Tanzania.

Mahusiano ya kimataifa, Zitto Kabwe ndio mwenyewe. Hata nguli wa Diplomasia Balozi Augustine Mahiga haoni ndani. Na mengine mengimengi.

Tena sasa anatumia neno lake maarufu kuwaita watu wengine ni MAZWAZWA. Yaani Watanzania wote Mazwazwa isipokuwa yeye.

Naipongeza sana Serikali kwa hatua inazochukua dhidi ya mtu huyu, nampongeza Rais Magufuli kwa jinsi anavyosimamia msimamo wa kuwataka Watanzania wafanye kazi. Wapiga maneno wa aina ya Zitto Kabwe watatuchelewesha sana na kuwaendekeza ni sawa na kulikabidhi Taifa kwa wahuni.

Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata na natarajia atafunguliwa mashitaka ili athibitishe watu 100 waliouawa huko Uvinza Kigoma, vinginevyo afungwe gerezani kama wanavyofungwa Watanzania wengine wanaokutwa na hatia.

Akifingwa huyu tutapata muda wa kufanya kazi na zaidi tutakuwa tumemtimizia kiu yake ya kukamatwa na Polisi na kisha kufungwa maana kwa anayoyafanya ni dhahiri anataka kukamatwa na kufungwa ili apate umaarufu wa kisiasa na ndio maana alipotoka mahabusu kaanza kujifananisha na Nelson Mandela.

Amesahau kuwa Nelson Mandela alikuwa anapigania uhuru wa Afrika Kusini na yeye anapigania tumbo lake baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kubana mianya yake ya upigaji wa hela kupitia kamati ya Bunge. Amebaki kupokea hela za Wazungu wanaomfadhili aje avuruge Tanzania. Kwingine kumebana.

Aidha, Zitto anakosea sana kuweka juhudi nyingi za kutafuta kujijenga yeye binafsi kisiasa ilihali chama chake cha ACT kipo hoi taabani, wanachama wanamkimbia, viongozi wanamkimbia, amebaki na vijana wachache anaowatumia kujijenga. Lakini kiuhalisia hivi sasa anaendesha chama chake kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hajali hata kuwapigania wananchi wa Kigoma Mjini, bila shaka anatambua kuwa 2020 hatakuwa Mbunge kwa hiyo anafanya fujo za mwishomwisho na kukusanya fedha za Wazungu anaowadanganya kuwa upinzani wa Tanzania una uwezo wa kushika madaraka ya nchi katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Mwisho niseme kinachompata Zitto leo ni haki yake na anastahili. Kwa tulipofikia hakuna jema kwake. Kila kinachofanywa na Serikali ni kibaya na akilala akiamka anafikiria kuichafua nchi na kuichonganisha Serikali na wananchi. Naamini Serikali inaliona jambo hili na itaendelea kumdhibiti.

Mungu Ibariki Afrika.
Mungu Ibariki Tanzania.
Umemuhukumu na unataka wote tukubaliane na jukumu yako kwa sababu wewe ndiye mwenye kiwango cha juu cha uelewa kuliko watu wote.
Umeshindwa kuelewa polisi walianzisha chuki na wananchi hao na ndicho kisa cha mapambano, Zitto uanayemchukia hakuwepo huko na jeshi la polisi lilikaa kimya. Ungekuwa mtu wa busara endapo ungemkalili Zitto akilitaka jeshi la polisi lifanye uchunguzi ili like na taarifa rasmi, hili umelikwepa kwa kusudi uzijuazo wewe.
Tafakari kauli yako yakuwa Zitto anataka kuchochea uadui kati ya polisi na wananchi! Unasahau uadui ulianza kutokea kabla ya Zitto kuongea, sasa rejea haya; Polisi wanasema waliouawa ni polisi watatu/wawili! Na RAIA wawili. Mbunge wa eneo husika, waliouawa ni raia kumi na saba na Zitto waliouawa ni kumi na saba, sasa kama ni uongo basi makundi yote matatu yamedanganya lakini Zitto pekee ametaka uchunguzi ufanyike hivyo kuonesha mashaka ya hao mia moja aliowataja.
 
Kelele Zitto zinanifanya niamini kuwa nchi inaenda sawa, Nchi inapanda kimaendeleo maana ukiona mabepari wamepata watetezi sio jambo dogo ujue wanafanya juu chini watusimamishe lakini chini ya jemedali John Pombe Magufuli tutasimama.
 
Back
Top Bottom