Hili litawashangaza wanawake………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili litawashangaza wanawake………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 8, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni jambo ambalo litawashtua wanawake, hasa walioolewa au ambao wana wapenzi wanaoaminika, kwamba, kila wanaume kumi ambao unakutana nao kila siku, watano kati yao ni lazima wameshakutana na kufanya mapenzi na wanaoitwa makahaba. Ni wepi watano kati ya hao kumi, ni jambo lenye kushangaza zaidi. Unaweza kuhisi kwamba, kati ya hao kumi, ni wale wanaume wahuni na chakaramu, ndio watakaokuwa wamekutana kimwili na makahaba……… Umekosea!

  Kwa kawaida kati ya hao kumi, watano ambao watakuwa wameshatembea na makahaba watakuwa ni wale ambao huwezi kuwategemea. Kwa nini? Kwa sababu ni wale wenye kujiheshimu kwa nje, wenye uwezo na pengine waliosoma vizuri. Hapa hata hivyo tunazungumzia makahaba ambao wanajiuza kwa kiwango kinachoweza kukubalika kwa watu wengi wakiwemo wageni kutoka nje. Wale makahaba kama wa Uwanja wa Fisi au Kimboka pale Buguruni hawahesabiwi kama makahaba katika viwango vya kiutafiti kama huu uliofanywa duniani kote.

  Kahaba kwa kawaida huhitaji fedha na pengine mahali pa kwenda kufanyia mapenzi na hili linawezekana kwa mwanaume mwenye uwezo kifedha. Kwa hali hiyo, watano kati ya hao wanaume kumi ni lazima wawe ni wale wenye uwezo mzuri kifedha. Kuna tafiti zinazoonesha kwamba, wanaume wanaochukua makahaba angalau mara moja kwenye maisha yao, ni zaidi ya watano kati ya kila kumi. Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba, wanaume sita hadi saba, huchukua makahaba katika maisha yao, hata kama ni mara moja tu.

  Lakini jambo la kushangaza na kusikitisha ni kwamba, imebainika sasa kuwa, wanaume wanaochukua makahaba, nusu yake ni wanaume ambao wameoa au wana wapenzi wanaowaamini sana. Kwa haraka mtu anaweza kuichukulia taarifa hii kama jambo lisilo na maana sana au lisilo jipya, lakini ni taarifa isiyopendeza kwa wanandoa au wapenzi.

  Tofauti na nyumba ndogo, kuchukua kahaba kunaweza kumfanya mwanaume asikamatwe kwa maisha yake yote, kwani kahaba na mnunuzi wake humaliza biashara huko huko. Kwa wale wakazi wa jijini Dar wanajua vizuri kwamba, makahaba wengi hufanyia mapenzi kwenye magari na hata makaburini na wanaofanya nao kuna miongoni mwao wanaoheshimika katika jamii. Ndio maana wanawake ambao wana waume wenye uwezo kifedha hawapaswi kujidanganya kwamba, waume zao hawawezi kutembea na makahaba. Kwa sehemu kubwa tafiti zinaonesha kwamba, uwezekano huo ni mkubwa sana. Kama watano kati ya kila kumi wanaweza kufanya hivyo, basi idadi ni kubwa
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  kutembea na kahaba kwa kijana mdogo lina uwezekano mkubwa............kwani kiu yake yawezekana ni kukutana kimwili na mwanamke yeyote atakayembahatisha......lakini baada ya kuoa hapo ni pasua kichwa.........inamaanisha sasa njemba hiyo ana matatizo makubwa.........................kwa sababu anachofuata huko siyo kujaamiana kwa sababu hana kiu...........................kama ana kiu basi hatosheki au hatoshelezwi..............................na huyo kahaba hawezi kumtosheleza kwa sababu kujaamiana is more than the physical contact..................it has to be the fulfilling emotional contact..............with the rapturous sex just a physical conduit to get the couple there..............and that is always gone lacuna when sex is bartered for cash......................
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  watano tu?
  nilifikiri 8 ya 10.....lol
   
 4. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye Red.....hujanishawishi, kujaamiana kwa wanaume wakati mwingine ni kwa ajabu sana, wakati wewe unasema kahaba hawezi kumtosheleza, lakini jambo ambalo wewe hulijui ni kwamba, katika swala zima la kujamiaana wanaume wengi huvutwa na udadisi wa sifa za nje za wanawake fulani.......... haiyumkini, mwanaume mwenye akili zake timamu anaweza hata kujamiaana na mwendawazimu ili kujua ana ladha gani. usifikiri wale omba omba pale mjini wenye watoto na wengine wana ujauzito wamepata wapi, ni kwa hao hao wanaume tena wengine ni watu wa heshima na wana familia zao.
  Sifa za nje za wanawake kama weupe tena wa kujichubua kwa mikorogo, Makalio makubwa, mahipsi, matiti makubwa nk....... huwashawishi wanaume kuwa na udadisi wa kutaka kuonja................
  Si hivyo tu wanaume pia hudanganyana wanapokuwa kwenye vijiwe vyao, humo huwajadili na kuwanyambua wanawake vya kutosha na ndio maana kuna wengine hujaribu hata kuwaruka ukuta wake zao kwa kutaka kuwaonja kama upande wa pili ukoje.........
   
 5. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hata mie nilihisi tu kuwa hizo takwimu Mtambuzi kazichakachua.............labda kama atakuw ame-base kwenye vigezo vya Kimagharibi..................
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hivi wewe vukani ni mwanamke kabisaaa?

  mbona nnatia shaka?????/
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  Oct 8, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Ungesema 10 kati ya 10 ningeamini utafiti huo...
   
 8. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  possibly mkuu!
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Tobaa! Ila Wa kwangu hayupo kati ya hao.
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Afadhali yangu ninayetembea na ma house girl! chungeni wafanyakazi wenu wa ndani!
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  hahahaa haya bana,hata mimi siko katika hao!
   
 12. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Suala la ukahaba huwa linajitokeza na kujadiliwa sana humu mmu. Kuna kipindi tulilijadili ikaonekana ukahabu ni wa aina nyingi.Sex for cash hiyo ndiyo straightforward ukahaba,lakini swali lilikuja je na anayetoa maksi za chu...i darasani,anayepandishwa cheo kwa kutoa nonino? anayepewa tenda kwa kumalizana biashara chumbani sea cliff? anayepunguziwa bei na mpemba dukani? je huu nao sio umalaya? Kama jibu ni ndiyo hapo kuna tena mambo ya 5/10 au ni 10/10?
   
 13. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Zile aibu za uanamke zilishanitoka kitambo................ hapa ni kuwachana wanaume kwa kwenda mbele.....................
   
 14. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapo umenena....................
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  sijashtuka
  I guess siangukii kwenye moja ya kundi...lol!
   
 16. s

  shalis JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani mtambuzi usiwaambie ya wanawake maana wanaume watazimia .... kwana hao makahaba si wanawake na wengine ni wake za watu so ..
  maisha is blah blah aaaa daima mpaka kifo
   
 17. M

  MyTz JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hata mimi mineangukia kwenye kundi la wa kwako......
   
 18. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,659
  Likes Received: 940
  Trophy Points: 280
  Haya tumekusikia.....
   
 19. B

  Bakeza JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Naunga mkono au tufanye 9 basi.
   
 20. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mtambuz jamni mbona unaniogopesha so utanifanya nisimkubali mtu
   
Loading...