Hili linawezekana Tanzania tu!.....

Wadau nchi yetu imeingia kwenye kitabu cha orodha ya maajabu baada ya wanafunzi wa Darasa la saba kufanya mtihani wa Hesabu wenye majibu ya kuchagua......a..b..c..d nakumbuka nilipokuwa nasoma mimi mtihani wa hesabu ukiandika jibu tu bila kuonyesha njia hupewi marks...sasa hii Tanzania yetu inaelekea wapi?? Nani wa Kulaumiwa????

sina hakika kama umefanya uchunguzi wa kutosha kuweza kugundua kuwa tanzania ni nchi pekee yenye kutumia mfumo wa kuchagua kwenye hesabu.... hebu fanya kuhusu mitihani ya kawaida kabisa kwa shule za kenya then uje upya
 
Mkuu huenda ni kweli kuwa Kenya walitangulia kufanya hivyo na huenda basi ndio maana Wakenya wanatupita kwa Lugha tu........(Kingereza sio Hesabu) ..... kama na sisi tumeamua kuwaiga sawa, tutakujakuwa na kizazi kisichojua kufikia kinachotaka kiwekewe majibu kichagu!!!.....
 
chama cha waalimu wa hesabu wamepinga kitendo hiki cha hesabu kuwa na herufi A,B,C,D kama majibu,should be numbers
 
sina hakika kama umefanya uchunguzi wa kutosha kuweza kugundua kuwa tanzania ni nchi pekee yenye kutumia mfumo wa kuchagua kwenye hesabu.... hebu fanya kuhusu mitihani ya kawaida kabisa kwa shule za kenya then uje upya

binafsi mimi ni mmoja wa watu wanaopinga mfumo huo maana serikali kupitia baraza la mitihani nahisi wamekurupuka tu kuanzisha mfumo bila kuwashirikisha wadau wa somo la hesabu.. kimsingi mimi ninahisi wameamua kutumia mfumo kuongeza idadi ya wanfunzi wanaofaulu ili wajiunge na shule zao za kata walizozianzisha kwa kukurupuka pia. hapa ijulikane kuwa mfumo huu hauzingatii efficiency ama kiwango cha elimu bali kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofaulu (nasema kuwa hiki ni kiini mamcho cha serikali kujisafisha kutokana na kushuka kwa kiwango cha ufaulu tanzania). hii itapelekea kupata kikazi cha watu wasiokuwa na uwezo kwa kufikiri maana katika masomo ynayomwezesha mtu kuwa na kiwango kikubwa cha kufikiri (nikosolewe kama siko sahihi)....
 
wadau nchi yetu imeingia kwenye kitabu cha orodha ya maajabu baada ya wanafunzi wa darasa la saba kufanya mtihani wa hesabu wenye majibu ya kuchagua......a..b..c..d nakumbuka nilipokuwa nasoma mimi mtihani wa hesabu ukiandika jibu tu bila kuonyesha njia hupewi marks...sasa hii tanzania yetu inaelekea wapi?? Nani wa kulaumiwa????

tunaiga mnooo, kila kitu copy and paste kutoka nchi za wenzetu. Wenzetu wanafanya research za hali ya juu kabla ya kuingiza mfumo wowote ili kuhakikisha unafaa na unamanufaa kwa jamii yao.
Hilo mie binafsi naona ni dili la mtu tuu. Mtu kapata tenda ya kuleta mshine za kusahihisha hiyo mitihani na makaratasi ya kufanyia hiyo mitihani, kaitoza serikali mara mia zaidi na ghalama yake ya kweli.
NA KITU KINGINE WAMESHAU PIA HIYO IMECHUKUA AJIRA YA WATU. SASA HIVI BADALA YA KUMLIPA MWALIMU ASAHIHISHE MTIHANI, MASHINE NDIO INAFANYA TENA KWA DAKIKA CHACHE TU.
Only in tanzania!
 
Asubuhi ya leo nlikuwa naskiliza Radio One, nikamskia NW wa Elimu Mh. Mulugo akisema wanafunzi wamepewa na working sheets za kuonyesha calculations na zinakusanywa.

Mulogo alikuwa smart alipo kuwa mwalimu wa kuandaa scheme of work, lesson plan, lesson notes na kujaza ma log book lakini na yeye sasa naona akili yake kubwa inaongozwa na akili ndogo kama wenzake. Naye ni msanii tu!

Kwa nini.

1. Working sheet lazima zikusanywe kama jinsi zinavyo kusanywa question pepars! Huo ndio utaratibu wa kawaida wa mitihani ya taifa. Anapo sema working sheet zitakusanywa hamaanishi kuwa zitakusanywa na ndio zitakazo sahihishwa ili kuoanisha na majibu ya kubuni kwenye karatasi, bali ana maanisha zita kusanywa kama makombo ya baada ya watoto kujaza majibu. Na hizo working sheet zitabaki shuleni kama zinavyo baki past papers zinyinge.

2. Kauli yake ni hadaa na usanii mtupu maana wamesha tutangazia kuwa kuna mashine maalumu zimenunuliwa kwa ajili kusahihisha mitihani hiyo. Mashine hizo hazisahihishi working sheet, bali zina sahihisha karatasi ya majibu kwa mtindo wa aidha A, B, C au D tena majibu yaliyo andikwa kwa wino maalum wa penseli za HB kwenye vyumba vya majawabu. Sio njia iliyofuatwa kwenye working sheet. Vinginevyo kungekuwa hakuna haja ya kutumia mashine.

3. Mtoto aliye amka vizuri na kubuni vizuri herufi za majibu ndiye atakaye faulu bila kujalisha kuwa ametumia working sheet au hakutumia lakini pia bila kujalisha kuwa ni kilaza au si kilaza. Mwisho wa siku ataenda kata maana working sheet sio final justification ya kumfanya mtoto afaulu na kupangiwa shule.

4. Tutegemee kuongozeka kwa kiwango kikubwa cha udanganyifu maana tayari udanganyifu umeanzia kwa waziri husika wa elimu (anasema working sheet zitakusanywa, ni kweli zitakusanywa lakini je, ndio zitakazo sahihishwa? Kwa nini asikubali kuwa zitakusanywa kama yatakavyo kusanywa makaratasi ya maswali?) Kwenye mtihani udanganyifu utakuwa mkubwa maana kuna watoto wenye uwezo wa kupepesa jicho/macho na kukamata majibu ya page nzima. Hawa watafaulu hisabati bila kujua 1 mara 1 ni ngapi.

5. Mtindo kwa SWALI, NJIA, JIBU ndio pekee unaweza kupima uwezo wa mtoto kwenye kunyambulisha milinganyo na kuonyesha umahiri wa kukokotoa au kujieleza kwa sentensi fupi na ndefu kwenye maswali ya kujieleza. Mulugo analeta longolongo na sidhani kama mwanae yuko st kayumba government school of Tanzania where we don't have desk and library for books.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
sina hakika kama umefanya uchunguzi wa kutosha kuweza kugundua kuwa tanzania ni nchi pekee yenye kutumia mfumo wa kuchagua kwenye hesabu.... hebu fanya kuhusu mitihani ya kawaida kabisa kwa shule za kenya then uje upya

binafsi mimi ni mmoja wa watu wanaopinga mfumo huo maana serikali kupitia baraza la mitihani nahisi wamekurupuka tu kuanzisha mfumo bila kuwashirikisha wadau wa somo la hesabu.. kimsingi mimi ninahisi wameamua kutumia mfumo kuongeza idadi ya wanfunzi wanaofaulu ili wajiunge na shule zao za kata walizozianzisha kwa kukurupuka pia. hapa ijulikane kuwa mfumo huu hauzingatii efficiency ama kiwango cha elimu bali kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofaulu (nasema kuwa hiki ni kiini mamcho cha serikali kujisafisha kutokana na kushuka kwa kiwango cha ufaulu tanzania). hii itapelekea kupata kikazi cha watu wasiokuwa na uwezo kwa kufikiri maana katika masomo ynayomwezesha mtu kuwa na kiwango kikubwa cha kufikiri (nikosolewe kama siko sahihi)....

Mkuu hapa umenichanganya!!
 
Back
Top Bottom