Hili linanitatiza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili linanitatiza

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by rain, Jan 11, 2011.

 1. r

  rain Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapendwa, nakwazika na hapa nimekuja kutafuta advice na vilevile kufunguliwa akili.
  Nina mume, nikahamishwa kikazi kwenda mkoa mwingine yeye akabaki dar, nilikuwa niko tayari kuacha kazi ili mradi tu tusitengane, au asione nimejali kazi zaidi yake, lakini alinitia moyo na kuniambia niende kufanya kazi, akani assure kuwa kila kitu kitakuwa sawa, tutakuwa tunaonana kila mara maana mikoa hii ni ya jirani. Cha kushangaza mwenzangu hataki kabisa kuja kutusalimia, yani nisipoenda mimi dar basi, yeye wala hashtuki hata weekend, watoto ninao mimi huku, sasa hii inamaanisha nini? kwa ufupi hajihusishi na kitu chochote kuhusu sisi, hatusaidii hata kodi ya nyumba japo yeye dar halipi kodi, wala matumizi wala nini, nothing. hata nikienda kmimi hatoi hata pesa ya nauli ya mimi kurudia huku wala hajali kama nalazimika kusafiri na watoto sometimes ili wamwone baba yao.
  Nifanyeje? nimechanganyikiwa hapa nilipo, au ndo njia ya kuget rid of me? kanichoka? au ndo nishawaachia wenzangu huko? niache kazi nirudi tubanane? nipeni tafsiri ya haya, is it normal kwa familia zingine? pls nipeni uzoefu wenu.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Pole jamani!Ngoja tuwasubiri wanandoa wengine wakupe ushauri na mazoea yao!Ila ungejaribu kuongea nae taratibu ukamuuliza ingekua vizuri maana majibu yake yatakupa mwangaza!
   
 3. r

  rain Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeshaongea naye
   
 4. Wakuletwa

  Wakuletwa Senior Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ok akasemaje?
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Acha kazi!
   
 6. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Pole dia. Ni kweli muweke kitako vunja ukimya. Mweleze tofauti unayoiona tangu uondoke usikie atakwambia nini.

  Kuhusu kuacha kazi usithubutu kabisa. Ukiacha halafu utaishi vipi kama ukirudi akunyime matumizi? Labda ufight uhamie tena dar lakini c mambo ya kuacha kazi dada. Utaishia kuteseka mpenzi.

  Pia jaribu kumweleza au kumkumbusha jukumu lake yy kama baba ili msaidiane kulea watoto. Najiuliza kama jukumu lote kakuachia ww sasa yy pesa yake anaifanyia nn? Ah,nachoka kabisa.
   
 7. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  mwanamama kakamaa mpaka ujue kinacho vinginevyo utakuwa unasema 'yule pale ndio alikuwa mume wangu'
   
 8. r

  rain Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  madai yeker yuko busy na kazi, na hilo la finance support ndo kabisa haeleweki anaona tu yuko sahihi na kuona mimi ndo mlalamishi
   
 9. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  hebu jaribu kuomba likizo kazini japo ya wiki mbili ukakae na mumeo vizuri upate muda wa kuongea na taratibu na kuchunguza chanzo cha mabadiliko,usikate tamaa kiasi hicho hayo mambo yapo na ukitumia busara am sure everything will be ok
   
 10. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  kasemaje?
   
 11. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  mi siafikiani na ww katavi.
   
 12. r

  rain Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hicho ndo kinanichanganya kabisa, kwamba pesa yake ye anafanyia nini? mara nyingi nafikiria sana na kuona its so unfair mwishowe naishia kuwa stressed na kuwa very bitter
   
 13. Wakuletwa

  Wakuletwa Senior Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unajua maisha ya ndoa dada yana mengi sana ndani yake, huenda wala hajakuchoka wala nini ila mazoea tu ndio yanayomsumbua. Nafikiri omba sana Mungu na pia jaribu kukumbuka mambo yote mazuri mliokuwa mkifanya pamoja then mkumbushe katika hayo. Pia kumbuka kuwa pindi uwapo na mwenzio fanya yale ambayo akiwa peke yake atakumbuka na kusema hili angekuwepo mama rain lingekwishwa. Hii inamaanisha kuwa kila wakati jaribu kuwa muhimu kwakwe na sio kuruhusu kuishi kwa mazoea.
   
 14. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  lazima uwe frustrated and bitter hali yenyewe ilivyo tight hivi na baba yao yupo! Loh bora angekuwa hayupo ungekuwa umeshazoea.
   
 15. Wakuletwa

  Wakuletwa Senior Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  He we katavi unamwambia ache kazi! Je na mumewe akimtema ni atapata uchizi
   
 16. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  sasa jamani ndo asitishe hata huduma ya wanae?
   
 17. LD

  LD JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwanza pole kwa hayo yote dada angu,
  Sina familia lakini kwa hali ya kawaida sidhani kama hio ni sahihi kwa baba kuwa wa staili hio.

  Najua hapa utapata ushauri mzuri tu, lakini na mbaya pia.
  Sasa ili uweze kuchanganya ushauri utakaoupata hapa na akili zako mwenyewe hebu, jaribu kumshirikisha Mungu.

  Ingia chumba chako cha ndani, moyoni mwako I mean, muombe Mungu, akuongeze katika kupata majibu ya hili tatizo lako.
  Halafu omba utulivu wa moyoni, hakikisha moyoni una utulivu, usiwe na hasira, chuki wala lawama juu ya baba huyo.

  Imagine hivi, Angekuwa ametangulia mbele ya haki (si ombei) usingeweza kuhudumia watoto wako na wewe mwenyewe?
  Jitengenezee confidence ndani yako, kwamba you can without him.

  Ukifanikiwa hapo, andaa safari na mpango mzuri tu, wenye hekima na unyekekevu ndani yake.
  Ukae na huyo baba/mume wako mpendwa, uzungumze nae, msikilize, mueleze vile unavyojisikia, hapo nadhani na Mungu akiwa upande wako,
  Utamuelewa tu nia yake ni nini hasa.

  Kumbuka hekima ya pekee inatakiwa hapa dada, zingatia utulivu moyoni, utaipata tu nia yake.
  Ukisha fahamu nia yake hata kama haitakuwa nzuri kwako, still usikate tamaa,
  utaumia lakini usikate tamaa kamwe, kumbuka unaweza, Yes you can even without him. Maana hata sasa umeweza.
   
 18. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  si ndo hapo sasa.
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kama hii ni ngumu basi aombe uhaMisho ili awe jirani na mume wake.
   
 20. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole sana my dear, usiache kazi ongea nae halafu mpelekee watoto wote akaenao wakati unapigania uhamisho wa kurudi dar, mwambie dar ndo kunashule nzuri kwa watoto ili tu na yeye aujue wajibu wake, then wape hali halisi mabosi wako ofisini lazima atatokea hata mmoja wa kukusaidia. Then ukishafanikiwa fight for him ukiwa nae dar.
   
Loading...