Caren
JF-Expert Member
- Feb 12, 2010
- 278
- 91
Ushauri mzuri pia. Unajua mara nyingi binadamu tunapotoa ushauri huwa tunatengeneza bias na kukupa ushauri kuonyesha kuwa tatizo liko kwa wengine na mara chache sana watu wanafikiria kukupa ushauri kuonyesha kuwa labda wewe ndio tatizo.
Sisi wanasheria tumeligundua hili mara nying sana tunapowashauri wateja wetu. Mara nyingi mteja anakuja akidai kuwa kaonewa na mwenzi wake lakini ukichunguza sana unakuja kugundua kuwa mteja wako ndiye tatizo na unaanza kazi ya damage litigation.
Sisi wanasheria tumeligundua hili mara nying sana tunapowashauri wateja wetu. Mara nyingi mteja anakuja akidai kuwa kaonewa na mwenzi wake lakini ukichunguza sana unakuja kugundua kuwa mteja wako ndiye tatizo na unaanza kazi ya damage litigation.
Wengi wamesaidia kukupa mchango mzuri wa mawazo nakuomba kwa yale mema basi yafanyie kazi.
Unajua hakuna kitu kinachouma kama unampenda mtu na ukaona mhusika haguswi hata kidogo kuthamini upendo unao-mpa hadi inafikia hatua unakuwa-bitter as you said.
Ushauri ni huu: Wala usipoteze muda, fanya uchunguzi wa kina utabaini ukweli. Umesema upo mkoa wa jirani na Dar, sasa kama una-moyo wa ujasiri sema hivi: panga safari ya kustukiza nenda kwa mume wako-dar lakini endapo nitamkuta na mwanamke mwingine zaidi yako usiwe na hasira yeyote ile-na umuombe mungu akuongoze vema- muda wa kufika home iwe ni usiku atleast saa 4 hivi piga hodi home au kama una-funguo spare we fungua mlango choma ndani.
Kama ukimkuta yupo alone take easy tu, akiuliza mwambie gari iliharibika ndio maana nimekuja muda huu, ukimkuta na mwanamke mwingine wewe wala usijali-take simple na uone je huyo mwanamke atalala humo ndani au itakuaje na yeye je atasema nini? Wewe lala asubuhi amka kama usafi fanya kisha muandalie chai anywe! Sasa mwambie tena kwa mahaba dah mume wangu nakupenda sana na muonyeshee kweli unampenda. Sasa utaona jinsi atakavyokuwa anajikanyaga kutaka kusawazisha mambo yake wakati wewe hujamuuliza. Hapo jibu utakuwa umelipata na yeye hatarudia huo mchezo kama anao. Still bado nadhani kwa uhakika kutakuwa ma mwanamke ambaye wewe anakufahamu fika na anajua upo mkoani hivyo yeye anaona ni bora au muda muafaka kufanya apendavyo na mumeo.
Nimeongea hilo kwa sababu ya uzeefu niliokuwa nao wa kubaini matatizo madogo madogo kama ya mapenzi ambayo wengi huwa wanatatizwa nayo.
NB: If you will do that, plse usiwe na hasira hata chembe na umuombe mungu wako akuongoze ili hatimaye ujue u-kweli na hata ukijua bado mume wako utampenda zaidi ili yeye ajione mjinga na kisha ajirudi