Hili la shule ya CCM kutaifishwa ni kipimo cha akili zetu za kutafakari mambo

Kwani shida iko wapi..mimi sijaelewa vizuri hebu nisaidie kunielewesha mkuu...maana mimi naona kwamba hata kama hiyo shule imeshindwa kujiendesha..je serikali ikiichukua si inakua ni nafuu kwa serikali kwa sababu imepata shule pasipo kuingia gharama kubwa ukizingatia shule zilizopo hazitoshi nchini.
Mimi naona ukakasi upo kwenye msamiati wa "KUTAIFISHA" tena mali zako mwenyewe badala ya kuzigawa au kutoa msaada kama wengine tulivyofanya.
 
Hatutaki heri yako ya mwaka mpya.....najua roho zinawauma sana jinsi JPM anavyopiga kazi..na baaaado

Viva Magufuli
NINA HAKIKA WATU WANAOSHANGILIA MAKIDA MAKIDA YA JPM NI WATU AMBAO WENGI WAO HAWAJASOMA AU HUENDA WANA UVIVU WA KUFIKIRIA
 
Mimi naona ukakasi upo kwenye msamiati wa "KUTAIFISHA" tena mali zako mwenyewe badala ya kuzigawa au kutoa msaada kama wengine tulivyofanya.
Actually kama tuna nia ya dhati ya kuvutia wawekezaji kuleta hela zao kuwekeza kwenye viwanda, inabidi huu msamiati utuondoke kabisa. Wawekezaji wanaogopa hii kitu kama UKOMA.
 
Shule ya CCM imetaifishwa na Serikali ya CCM kwa amri ya Mwenyekiti wa CCM
point mnayoimiss ni kuwa kasema kama yatahitajika malipo kwa wanaotaifishiwa shule atamwagiza ndally afuatilie suala hilo,

kwa maneno mengine tunaweza sema serikali imenunua shule toka ccm
 
Hatutaki heri yako ya mwaka mpya.....najua roho zinawauma sana jinsi JPM anavyopiga kazi..na baaaado

Viva Magufuli

usikatae heri ya mwaka mpya,pamoja napongezi zangu kwa kutaifisha shule naomba mheshimiwa ataifishe,ccm mkwakwani,kirumba,alihasani tabora,kwani ni mali za wananchi wa tz bila kujali vyama vyao.
 
Swali lingine dogo tu, Je ccm inashule ngapi na kwanini zisitaifishwe zote!
Umesema vyema, waache kutupaka mafuta ya mgongo wa chupa.
Kama kweli ni uzalendo fanyeni hivyo kwa shule zote za wazazi wa CCM tanzania.
 
Sababu moja kubwa ya Omwami kutaifishwa ni kwamba ilikarabatiwa kwa fedha za umma jambo ambalo ni kosa kwani hiyo ilikuwa private property. Njia ya kujinusuru na kosa hilo kubwa ni serikali kuitwaa ili kuhalalisha hayo matumizi ya fedha za umma.
 
Labda ndio ujanja wa kutumia Pesa za Rambi rambi kui rebuild shule ya CCM lakini kuzuga anaodhani ni mazuzu anajfanya anaitaifisha kwani hapo mwanzo Jumuia ya Wazazi ilijenga hizo shule kwa pesa za nani? Si usanii tu kama walivyopora viwanja vya michezo kila kona? Au waluza maganda ya korosho!
 
JMP aliposema eti ametaifisha shule ya ccm (Omwani) na kuwa ya serikali watu wakashangilia na kudai eti ni mzalendo wa kweli.
Kwa ufupi tu ni kwamba kwa wanaoifahamu shule ya omwani hawawezi kushangilia hiki kitu.

Shule hii haikuwa productive kwa ccm na ilikuwa ni mzigo kwa ccm na ilikuwa inajiendesha kwa hasara. Ni shule ambayo ilikuwa inabeba makapi ya wanafunzi na wale wazazi walikuwa hawana huwezo wa kupeleka watoto katika shule zenye sifa nzuri yankufaukisha.

Pili hili jambo lilishajadilika kwenye vikao vya ccm namna ya kutua huo mzigo. Na ndio maana unaona serikali inabeba mzigo wote hadi wa waalimu wake ili kuiokoa ccm na mzigo wa madeni. Kwa kifupi huu ni ufisadi mwingine.

Swali la kujiuliza hivi ni kweli shule hii ingekuwa inafanya vizuri katika elimu na ikawa inajiendesha kwa faida JMP angeitaifisha. Jipu ni hapana. CCM wasingekubali kuiachia. Swali lingine dogo tu, Je ccm inashule ngapi na kwanini zisitaifishwe zote!

Watanzania wenzangu tusiwe wepesi wa kushangilia kila jambo bali tujaribu kujiuliza maswali juu ya nini kiko nyuma ya uamzi uliofikiwa.
Kwa hili la shule ya umwani ni sawa na kupewa gari lililojuu ya mawe ambalo mwenye nalo limemsha mshinda. Hapa tumepigwa changa macho.

Nawatakia Heri ya Mwaka Mpya.
Kuna thread wame imerge ,ila ni kwamba hii ni dalili mbaya na hila nyingi.Siku za nyuma tumeona wakianza muve kuna mtu anaviziwa.Na shule za private zimepigwa vita sana.Hii move inaweza kuwa ni kuchukua shule za private sasa kunafuatia.
 
Mleta mada, tafuta sababu kuu ya kutaifishwa kwa hiyo shule then ndo uanze kuuliza vijiswali vyako vya uchonganishi.
 
Wanajamvi msijitoe ufahamu bure kwani ukweli nyuma ya pazia ni huu.
1. Jina sahihi la shule ile ni "Omumwani" ni shule ya zamani enzi za TAPA.
2. Tayari kuitaifisha ilikuwa haiepukiki kwa kwa ujanja ujanja tayari CCM ilishatumia milioni zaidi ya 178m kuikarabati toka mfuko wa maafa (alitamka mwenyewe kuwa ana mashaka na matumizi ya ukarabati wa shule hiyo kwani wamemtajia 119m wakati makaratasi aliyonayo yanasema 178m) kinyume na malengo ya serikali ya kukarabati taasisi zake na baada ya JPM kugundua "SCANDAL" akaona hakuna NAMNA zaidi ya kuitema. kufunika kombe mwanaharamu apite.
 
Mleta mada, tafuta sababu kuu ya kutaifishwa kwa hiyo shule then ndo uanze kuuliza vijiswali vyako vya uchonganishi.
Ningekuona mwenye maana kama ungepinga na kutueleza sababu unazozijua wewe kwanini imetaifishwa.
 
Back
Top Bottom