Hili la shule ya CCM kutaifishwa ni kipimo cha akili zetu za kutafakari mambo

ataifishe viwanja vya mpira Tanzania nzima, ni mali ya wananchi wote na sio ccm tu
 
Nyerere alipotaifisha shule za Makanisa alikuwa na nia ya kutua mzigo wa kanisa?
Nyerere alitaifisha shule zote za kanisa na misikiti. Je rais anapata wapi uwezo wa kutaifisha mali za chama cha siasa. Kama iliendeshwa kwa hasara, mbona viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na ccm na vinaendehwa kwa hasara havitaifishwi? Au ni suala la muda!
Heri wanaokosoa kuliko wanaosifisia makosa ya mfalme.
 
Haiingii akilini kuwa "eti ametaifisha" shule,
Kutaifisha maana yake ni kuchukua mali bila ya ridhaa na bila fidia. Sasa Magufuli ndiye Serikali, na ndiye SisiEm. Hapa anataisha je? Alichofanya ni kuhamishia umiliki upande wa pili alipoona ni rahisi kufaniskisha uendeshaji wa shule. Ingekuwa shule ni ya CUF ningeelewa huo utaifishaji, lkn sio shule ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM Magufuli na rais wa JMT Magufuli.
 
Haiingii akilini kuwa "eti ametaifisha" shule,
Kutaifisha maana yake ni kuchukua mali bila ya ridhaa na bila fidia. Sasa Magufuli ndiye Serikali, na ndiye SisiEm. Hapa anataisha je? Alichofanya ni kuhamishia umiliki upande wa pili alipoona ni rahisi kufaniskisha uendeshaji wa shule. Ingekuwa shule ni ya CUF ningeelewa huo utaifishaji, lkn sio shule ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM Magufuli na rais wa JMT Magufuli.
Shule ya CCM imetaifishwa na Serikali ya CCM kwa amri ya Mwenyekiti wa CCM
 
Nyerere alipotaifisha shule za Makanisa alikuwa na nia ya kutua mzigo wa kanisa?

Kwani ulikuwa hujui?!!! Hilo mbona halihitaji PhD kulifahamu! Toka zama za ukoloni shule za kanisa zilikuwa zinaendeshwa kwa ruzuku toka serikalini. Tulipopata uhuru ruzuku kwenye shule hizi ilikatwa na shule hizi zilikuwa na hali mbaya na nyingi zilishindwa kujiendesha. Hapo mpango wa utaifishaji wa hizi shule ukabuniwa ili kuzinusuru hadi pale makanisa yatakapokuwa na uchumi mkubwa wa kuendesha shule hizi. Hii ndiyo maana shule nyingi za kanisa zilizotaifishwa zimerejeshwa kwa makanisa na baadhi zimefanywa vyuo vikuu. Mfano wa shule zilizorejeshwa kwenye umiliki wa makanisa ni Mihayo Tabora, Mazengo Dodoma na Magamba Lushoto. Unalo?!!!
 
Hatutaki heri yako ya mwaka mpya.....najua roho zinawauma sana jinsi JPM anavyopiga kazi..na baaaado

Viva Magufuli


Ataifishe na viwanja vilivyojengwa kwa michango ya watanzania wote kabla ya mfumo wa vyama vingi viwe mali ya serikali
Kuna aganda ya kutaka kutaifisha shule za taasisi zingine ndio maana wanajidanganyishia kutaifiosha shule ya ccm hiyo ni njia ya kuhadaha watanzania
 
kiukweli wapinzani wa Tanzania mnatia aibu,yaan mi mwenyewe siwakubali ccm kwa 100% lakini bado sijakiona chama cha upinzani Tanzania kinachojielewa....hv kwani hiyo shule ikiboreshwa na serikali na kuwapa ajira za kudumu waalim atakayefaidika ni nani?atafaidika magufuli na familia yake au ni watanzania wanaolia kuwa hakuna ajira??
hiyo shule hata kama ilikuwa inawanafunzi 200 kwa mfano ambao wazazi wao kama vile ww mtoa mada unavyodai kuwa walikuwa ni maskini kiasi kwamba walishindwa kuwapeleka watoto wao ktk shule za maana lakini leo hii watoto wao wakisomeshwa bure tena bila hao wazazi kulipa ada yeyote itakuwa faida wa wakazi wa bukoba au kwa magufuli yy na familia yake????hebu wakati mwingne muwe mnafikiria kabla ya kupost..wakati mwingine chadema pamoja na wapinzani uchwara wengne mnawakatisha tamaa watanzania kuingia katika movements zetu coz hakuna mtu mwenye akili anayetaman kujiunga katika jopo la wapumbavu ambao wao kila kitu kwao ni kupinga tuu.
 
Kwanini hajataifisha shule zote zilizo chini Ya ccm? Mwenye uelewa usiokuwa na Mashaka atanijibu

Omumwani sec school imetaifishwa kujustify matumizi ya kuikarabati kwa mfuko wa maafa!
 
Kwanini hajataifisha shule zote zilizo chini Ya ccm? Mwenye uelewa usiokuwa na Mashaka atanijibu
Mimi sijabahatika kuisikiliza hotuba yake. Nisaidieni kujua ametoa sababu zipi zilizopelekea uamuzi wa "kuitaifisha" shule hiyo?
 
Kuna tatizo gani la serikali kunusuru shule hiyo kutokana na mapungufu makubwa yaliopita kutoka kuanzishwa kwake hadi leo?
Serikali haihesabu wingi wa shule tu,ni wajibu wake kuhakikisha mahitaji ya shule yanatimizwa.
Vivyo hivyo mali za wananchi zinazohodhiwa na CCM na huku chama kimeshindwa kuboresha Kama Kirumba stadium zirejeshwe kwenye serikali.
 
Hao walitaka kupiga pesa za rambirambi kwa kujikarabatia shuile yao...
Dili likabainika sasa wanakabidhi shule kwa serikali...

Wadanganyika wenzangu mpo...??
 
Back
Top Bottom