Hili la mwandishi Privatus Karugendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la mwandishi Privatus Karugendo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ARV, May 3, 2012.

 1. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 311
  Trophy Points: 180
  Katika gazeti la Raia mwema la jana May 2, ana makala yenye kichwa cha habari 'Mwalimu Nyerere amefufuka.Yuko Sumbawanga'katika aya ya pili ya makala yake anaandika,"kisa ninachokisimulia kwenye makala hii ni cha kweli na kimetokea mbele ya macho yangu pamoja na watu wengine niliokuwa nao kwenye gari.Tumekutana na Mwalimu Nyerere! akiwa mzima."

  Haya mambo ya 'kusadikika' kwa nini yanapewa nafasi katika magazeti haya makini? Kwa nini yasipelekwe kwenye vile vigazeti vya udaku?
   
 2. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Muulize kwanza Mwandishi Ndugu...
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Inaweza kuwa ni fasihi simulizi, ungetuwekea makala yote ili nasi tuone maudhui.
   
 4. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Nikiri kwamba sijaona gazeti tajwa (Raia Mwema), Nikiri kumfahamu mwandishi tajwa (Privatus Karugendo) kwa kusoma makala zake na kwa kufahamiana naye, Nikiri gazeti tajwa kuwa makini kati ya magazeti yaliyopo kwa sasa. Siamini kama Karugendo (ex-Padri) anaweza kuandika hayo na gazeti makini likachapisha. Kwa upande mwingine ARV utudhibitishie kwamba umesoma kwa makini kati ya msitari na mstari lakini pia umezingatia lugha ya picha/fasihi simulizi.
   
 5. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana ni nini kilimfanya akaasi Upadri?
   
 6. papason

  papason JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  ARV!

  Inawezekana kabisa hujamuelewa vizuri Karugendo, huyo mwandishi ni bingwa wa kutumia fasihi simulizi kinoma, ukisoma makala zake kijuju unaweza usimwele kabisa!
   
 7. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndo shida ya kusoma kitu kishabi shabiki.
  Karugendo hayuko Ulaya useme hawezi ulizika kama una shaka na alicho kiandika.
  kwa kawaida yake huwa anaweka mawasiliano yake mwisho wa makala zake,muulize kisha njoo hapa!
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ARV, Nimesoma hiyo article ya Karugendo na sijaona ni wapi amekosea. Kama umesoma 'headline' peke yake utapata dhana potofu, lakini kubwa kama hujaenda shule basi unaweza kupata tafsiri potofu.

  Anachoongelea Karugendo ni 'legacy' ya Mwl Nyerere kupitia vijiji vya ujamaa alivyoanzisha huko Sumbawanga. Na kwa maoni yake Karugendo ni kwamba initiative hiyo ya vijiji vya ujamaa ilifanikiwa na sana huko Sumbawanga na hadi sasa watu wanaishi kwenye huo mfumo. Na anashangaa ni kwa nini ;'sucess story' hiyo haijawafakia watanzania sehemu zingine!

  Kwa kifupi, inabidi usome kwa makini makala nzima ili upate kile anachojaribu kusema.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nimeisoma hiyo makala......ARV inaelekea umezoea kusoma makala nyepesi nyepesi sana hivyo hujamuelewa Karugendo......ni bingwa wa fasihi
   
 10. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,636
  Likes Received: 1,998
  Trophy Points: 280
  Sio mnafiki!
   
 11. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,487
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Tatizo la kutokupenda kusoma ndo linamsumbua, akishasoma kichwa cha habari tayari amemaliza kila kitu. Kwa mwaandishi kama Karugendo unatakiwa utulie tena sana ndo utaelewa makala zake. Ni moja kati ya waandishi wanaojua kutumia nguvu ya hoja kuelezea kitu.
   
 12. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Wewe ndio umekurupuka,hujamuelewa. Tatizo umesoma heading na kajisehemu tu. Nenda kaisome yote ndio utamuelewa vizuri. Sisi tuliosoma yote wala hatujaona tatizo
   
 13. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Tehe, inaonekana ARV ni mwenzangu na mie ambao ni mabingwa wa kusimama pembezoni mwa barabara kusoma vichwa vya habari magazetini then tunaishia kusema "aah! waandishi bwana" bila kununua gazeti na kusoma yaliyomo ndani.
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,279
  Trophy Points: 280
  Siwashangai watu kama huyu ARV wao wameshazoea magazeti yao yenye heading kama Kanumba aonekana Tabata, Okwi, Boba Sunzu watakiwa Chelsea, Kikwete Chaguo la Mungu na a lot of the same rubbish.

  Sasa kama ameshindwa kumuelewa muhandishi huyo je anaweza kumuelewa Jenerali Ulimwengu? halafu ningependa kuuliza hiyo Makala imeandikwa na Padri Privatus Karugendo au Prudence Karugendo? maana hawa ni watu wawili tofauti.
   
 15. k

  kamili JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Hakuna makala kama hiyo kwenye gazeti na tarehe ulilolitaja, labla kama unafanya mzaha, ambapo hapa si pake. Yafuatayo ndio makala yanayopatikana Raia Mwema la tarehe uliyotaja.


  [h=2]Makala[/h] Pinda alifanya kosa, asirudie kosa

  Msomaji Raia  Tume ya Warioba isije ikawa kama Tume ya Warioba
  Utata kifo cha Karume: Chuki binafsi au mapinduzi? IV  CHADEMA wana wananchi CCM ina dola  Mizengwe hadi bungeni  Wana usalama na nguvu yao kwa viongozi

  Evarist Chahali  Shivji na mapambano ya wanyonge

  Ahmed Rajab  Mgogoro wa ardhi sasa wapambanisha wageni


  Mwandishi Wetu
  Huyu leo, kesho mimi au wewe ni maisha kama vile hakuna tatizo


  Hidaya  Toleo la 237


  Watanzania wajitose katika mafuriko gani, ya Sunami au mtoni?


  Ayub Rioba  Wakubwa wapagawa

  Waandishi Wetu  Arumeru bado kwafukuta

  Paul Sarwatt
  Msipandishe tena bei za vinywaji - Mbunge


  Mwandishi Wetu  Waziri mkuu asiye waziri mkuu, serikali iliyobinafsishwa: hatuendi ko kote


  Jenerali Ulimwengu


  ama Zitto katumwa na Rais Kikwete; Jakaya Kikwete katumwa na nani?


  Msomaji Raia   
 16. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  haya sasa naona watu tunazidi kuchanganyikiwa
   
 17. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 311
  Trophy Points: 180
  KAMILI!
  Hiyo makala iko gazeti la raia mwema ya May 2, kama nilivyosema awali, page no.18. Naona unataka kutuchanganya zaidi, nadhani tatizo huna nakala halisi unasomea kwenye internet ambako makala zingine huwa hawaziweki. Tafuta hilo gazeti utaiona hiyo artical ya 'Padri' Privatus Karugendo..
   
 18. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Hili ndo tatizo la wabongo wengi, kukurupuka. Isome vizuri hiyo makala kabla hujaleta ***** humu
   
Loading...