Hili la Godbless Lema ni la kuiga, kubeza au kuunga mkono?

Kwanza tujiulize, Lema amekamatwa kwa kosa lipi? Hilo la kuandamana? Kesi imeundwa ndani ya kesi! Amechaguliwa kwa wingi wa kura, landslide victory, dhidi ya aliyekuwa mgombea mwenza, Dokta Batilda Salha Burian (CCM). Wakaunda kesi ya mizengwe kuhakikisha kwamba Lema anashindwa kutimiza wajibu wake kama Mbunge, kwa kumuundia kesi ya mizengwe, na kuhakikisha kwamba wanamkamata mara kwa mara, na kuwasumbua viongozi wenzake wa CHADEMA. Nimeona jinsi alivyokamatwa akiwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa kumtafuta Meya wa Manispaa ya Arusha!

Polisi wanaingia kwenye mkutano, wanawakamata wajumbe, madiwani, na Mbunge wa Jimbo! Hii inaingia akilini kweli? Tumekuwa lini Police State?

Sasa kilichobaki ni Civil Disobedience. Tusiogope kwenda jela! Twende huko kwa wingi tu! Wao walidhani tutaendelea kuogopa vitisho vyao na jela zao. Sasa tuzikubali tu! Hata mie nishaenda jela, kwa ishu nyingine ya kipuuzi tu! So, hata wakinikamata, sawa tu! Ntaenda nikicheka, hata kama ntapigwa virungu!

Amandla! Awethu! A Luta Continua!

Sasa kazi imeanza rasmi! Tunaikomboa nchi yetu kutoka kwa GENGE LA MAFISADI!

./Mwana wa Haki
Asilimia aliyoipata lema huwezi kuiita landslide, kama hivyo basi hata JK alipata landslide victory.
Nyekundu ya pili:Huwezi kuingilia kazi ya mwenyekiti wa kikao (meya) na kubatilisha uchaguzi kinguvu bila kutumia sheria, huwezi kusema..diwani fulani hebu simama ujieleze!, bila ruhusa ya mwenyekiti.
Ukiambiwa acha kufanya hivyo, unakasirika na kuendelea kuongoza kikao... ukiambiwa nenda nje unakataa na una resist arrest, kisa... unawaambia polisi hamuwezi/huruhusiwi kunikamata.
Nadhani huko ni kutojali au kudharau sheria na mamlaka....But I wish him all the best, may be one day nitamuelewa but up to now bado sijaelewa somo!!
 
Taratibu mama; nenda ukazodoane na akina mama wenzio huko jiko na wala si kwa kila mtu hivi.

Wewe umeshafunga safari? au ndio unawaendesha kwa "remote control". Ungeanza kuonesha mfano, kwanini utarajie wengine wafanye unachoshindwa wewe kukifanya? una ulema wa kutokufanya hayo unayo hubiri?
 
Kuiga ni ushujaa
Kubeza ni ujinga
Kuunga mkono ni uzalendo.
Tafsiri yoyote tofauti ni unafiki.
WanaJF tuwe mfano angalau kwa kujiondoa kwenye hizi IDs bandia. Vinginevyo kama ni unafiki sisi tunaongoza.
 
Bora umeliona hilo huyu jamaa ni kichwa haswa kwenye mjadala wa Mzee Said Mohamed nilikuwa nasoma nondo zake huwezi kukubali ndiye huyu anaandika upuuzi hapa kupenda kweli upofu.

WanaJF tuwe mfano angalau kwa kujiondoa kwenye hizi IDs bandia. Vinginevyo kama ni unafiki sisi tunaongoza.
 
nimependa comment yako lakini kwa hali iliyopo sasa nchini tulitegemea labda wachungaji na masheikh wafanye kitu hawafanyi chochote, wasomi hawasemi chochote, vyama havitaki kuungana, wananchi tu waoga sana hata juzi (dsm) tuligwaya 'vitisho vya Al-Shaabab', kwa kifupi makundi yote yanaangalia tu na hakuna anayeonekana kuonyesha njia mbali na kulalamika tu!!!
Tuelewe kuwa na Mh. Lema ni sehemu ya jamii hii tunamoishi, kwa hiyo aliloamua kufanya linaweza kuwapa kwanza mtazamo mpya polisi ambao wamekuwa wakitutisha na mahabusu zao.
Lakini cha msingi hapa ni kuwa moto wa kuunguza nyika nzima huanza kidogo sana! ...hata Mzee Mandela mwaka/mwezi wake wa kwanza watu walimcheka sana na hawakuwahi kujua nini kingejiri miaka 25 baadae.
Na kwa feeling kidogo jaribu kusikiliza wimbo mmoja wa mwanamuziki (Mungu amlaze mahala pema peponi) Luck Dude unaitwa 'the house of exile'
sema wewe. Hakuna pilitical correctness kwa wanasiasa wetu. Hii haina tofauti na fisadi kupewa uongozi.

Labda tunaweza analyse kitu conflict of interest kwanza kabla hatujang'ang'ania mahabusu kutafuta public symphathy. Hakuna Mandela wa karne hii.
 
Hawa ndiyo wafuasi wa kijana Lema, pamoja na Chadema kila siku sisi watumishi wa Mungu tunaomba Chadema wasikamate dola watatumaliza kama Somalia

Kama watumishi ndio mna kauli uharo kama hizi basi kweli Mungu ana masikitiko sana huko mbinguni...naomba kujua haya yafuatayo toka kwako..
  1. Una elimu gani...?
  2. Umewai kuumwa ugonjwa wowote wa akili...?
  3. CCM wamefanya mazuri yapi? Au kwenda ku-sign ushoga na uchafu mwingine ndio unaona ni ishu ya maana?
  4. Kanisa gani unaongoza maana kama ndio hivi basi akili za waumini ni mbaya zaidi...
Naomba majibu...
 
Nchini Tunisia kijana mmoja msomi wa Chuo Kikuu aliyekuwa amekosa kazi huku akiishi maisha ya dhiki sana aliamua kujiua. Tokea hapo, maandamano yalianza, yalisambaa nchi nzima na leo utawala huo umeangushwa. Tumesubiri nini watanzania?
 
You mean anaweza kuvaa viatu vya Mbowe kama mwenyekiti wa CDM Taifa?
Mbowe aondoke tu na vyatu vyake huyu ashonewe viatu vingine ikitokea kuchaguliwa,nilikuwa namwona mtu wa vurugu lakini sasa nimemwelewa na kumkubali -prisoner of concience a.k.a Steve biko wetu.Yuko kwenye level ingine kabisa na ni vigumu kwa wabongo wengi kumwelewa tuna hulka ya kuogopa utawala na vyombo vyake.

mkuukn kuna mtu alipita hapa jf akatuambia sugu anafanya mambo ktk jimbo lake si kitoto, khs bifu na clouds zizani km lina athari sana coz sio kwamba anashinda ofc za clouds akipaka la hasha ni kwamba munaona bifu sababu akipata sehemu ya kuongea ndio anaongea lkn sio muda wote anaongelea clouds.
Mkuu mimi kwetu Mbeya mjini 4th street house no.6 najua nachoongelea na pia mkuu mpya wa Mkoa kaahidi kufanya kazi na wabunge/madiwani bila kujali ni wa chama gani Sugu aitumie vizuri nafasi hii,angekuwepo Mwakipesile tungekuwa tunaongea mengine.

Hiyo nadhani ni approach ya NTC ya Libya. Ni kujipeleka utumwani. Kwa nini tusipiganie haki zetu sisi wenyewe bila kwenda kuwasujudia wazungu? Unapokwenda kushitaki kwenye ubalozi wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, n.k. ni sihara ya kukiri kuwa wale ni mabwana zako na bila wao huwezi kitu. Nia ibu.
Utatuzi wowote kutoka nje hautatuwi kitu na ndio maana tuko hapa baada ya miaka 50 na tulipata Uhuru muda mmoja na Malasia,Korea na Singapore.
 
Kisheria mbunge ni kama mwananchi mwingine, unless akiwa mjengoni, akielekea au kutoka mjengoni au akiwa kwenye vibaraza na bustani za mjengoni... zaidi ya hapo anaweza kukamatwa kama sisi wengine.

Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!
Ahsantee.gif

Ooops kwa hisani ya Invisible khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Bora umeliona hilo huyu jamaa ni kichwa haswa kwenye mjadala wa Mzee Said Mohamed nilikuwa nasoma nondo zake huwezi kukubali ndiye huyu anaandika upuuzi hapa kupenda kweli upofu.

Ngongo, kwa mara nyingine nitavunja msimamo wa kutojibu post kama hii yako hapo juu na baada ya hapo naomba tuelewane kwa jambo moja tu. Mimi sikuwahi kuwa mwana TANU, sikuwahi kuwa mwana CCM na katika msingi huo huo sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa katika maisha yangu yote. Amini usiamini sijawahi hata kupiga kura na sababu ninayo sana lakini hayo tuyaache angalau kwa sasa. Ni chama kimoja tu kilichonivutia kwa muda mfupi hadi nikafikiria kujiingiza kwenye siasa hapo mwaka 1992 nacho ni NCCR - Mageuzi lakini kilipomkaribisha tu mtu moja anayeitwa Mrema kukiongoza, hamu yote ilipotea.

Mwaka 2007 alipotokea Mwanasiasa kwa jina Dr. P. W. Slaa, akasimama jukwaani Mwembeyanga na bila kumung'unya maneno akatangaza 1st Eleven ya ufisadi kwa wakati huo, kusema kweli aliniteka. Toka wakati huo nimeiangalia Chadema kwa jicho tofauti na nimejaribu kufuatilia tena siasa nchini kama wakati fulani hapo nyuma. Mimi CCM siipendi na wala sijawahi kuipenda iwe ni katika awamu ya kwanza, ya pili, ya tatu na sasa ya nne kwa sababu naamini adui wa taifa letu la Tanzania ni CCM.

Simfahamu Lema, simfahamu Mbowe, simfahamu Zitto na hata Dr Slaa simfahamu lakini nafahamu vitendo vyao kisiasa na jinsi wameweza kuwafungua macho Watanzania hadi sasa wengine, si wote, tunauona usanii wa CCM na viongozi wake. Kubali usikubali pole pole Watanzania walio wengi wanazinduka na kutambua kwa nini hili taifa lenye kila neema liko hapa lilipo na kwa sasa ni jinsi ya kuondokana na hilo tatizo, CCM.

Unaweza kwa ujinga wako, kwa kukosa ushujaa na kwa kukosa uzalendo ukabeza kitendo cha Lema, hiyo ni haki yako kabisa na hakuna wa kukuzuia. Katika misingi hiyo hiyo na mimi nina haki yangu ya kukiona kitendo cha Lema kama cha kishujaa, tafadhali usijaribu kuzuia hiyo haki yangu, not now, not ever. Kwa miaka hamsini tumekuwa kama wapangaji ndani ya nchi yetu, tumenyanyaswa ndani ya nchi yetu na tumepuuzwa ndani ya nchi yetu lakini sasa thanx to Lema, Dr. Slaa na wengine wengi tu, tumeamka na kwa sauti tunasema imetosha.

Ngongo una haki ya kunibeza na hata kunitukana lakini moto huu unaofukuta huwezi kuuzima na ukae ukijua hivyo.
 
aisee watu tunatofautiana kuelewa na mtazamo

mimi naamini 'confrontational politics' hazitasaidia hii nchi
sana sana zitaleta 'machafuko'
na watakaoumia ni wasio na hatia...mke wa lema anaweza kupanda ndege na watoto haooo nairobi au kampala

CCM ni kama 'machizi wenye silaha'
unahitaji kutumia 'akili' ku deal nao
na sio kuanzisha 'mapambano'
Mkuu its all peoples move! setting back and relaxing haisaidii, huoni hata katiba mpya CCM wameshaitunga? hold ya breaths mkuu, this is how it should go!
 
siasa hizi huwa hazikawii kuchuja na wale unao waongoza kukuchoka, kitendo alichofanya lema cha kugomea dhamana ni mchezo wa kitoto wa kisiasa ambao waliupanga yeye na mwenyekiti wake, haingii akilini hata siku moja, Lema agome halafu haijapita hata mwezi mmoja mwenyekiti anaenda kumsihi ati atoke ili aweze kuhudhuria vikao vya bunge, JE? kwani hakuwa anajua kuwa tarehe ya kuanza kwa bunge? dhamira halisi hakuwa nayo ndiyo maana hata chakula chake kilitoka nyumbani kwake! hatukusikia amegoma kula! ipo siku wale wanao mshabikia watabaki kulia na kushika vichwa, wakumbuke aliyekuwa MB Dkt Walid kabouru amewaacha vijana wengi wa kigoma mjini wakiwa viwete kutokana na ushabiki kama huu, Matokeo yake yupo CCM leo anakula kuku, Vijana tusitumike kama ngazi ya watu kufikia malengo yao, tuwe makini.
 
Magamba at work......!!!!

nafikiri ni haki kufanya vile ili ulimwengu uingilie kati haki yake ipatikane,ni njia mojawapo ya ku protest'
 
siasa hizi huwa hazikawii kuchuja na wale unao waongoza kukuchoka, kitendo alichofanya lema cha kugomea dhamana ni mchezo wa kitoto wa kisiasa ambao waliupanga yeye na mwenyekiti wake, haingii akilini hata siku moja, Lema agome halafu haijapita hata mwezi mmoja mwenyekiti anaenda kumsihi ati atoke ili aweze kuhudhuria vikao vya bunge, JE? kwani hakuwa anajua kuwa tarehe ya kuanza kwa bunge? dhamira halisi hakuwa nayo ndiyo maana hata chakula chake kilitoka nyumbani kwake! hatukusikia amegoma kula! ipo siku wale wanao mshabikia watabaki kulia na kushika vichwa, wakumbuke aliyekuwa MB Dkt Walid kabouru amewaacha vijana wengi wa kigoma mjini wakiwa viwete kutokana na ushabiki kama huu, Matokeo yake yupo CCM leo anakula kuku, Vijana tusitumike kama ngazi ya watu kufikia malengo yao, tuwe makini.

Kuku gani mkuu, kuwa mwanasheria wa magamba au? Lamwai yuko wapi sasa hivi naye anakula kuku au? Ondoa huo ukungu kichwani akili zako zitakurudia ndugu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom