Hili la Godbless Lema ni la kuiga, kubeza au kuunga mkono? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la Godbless Lema ni la kuiga, kubeza au kuunga mkono?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 2, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Mwl. Julius K. Nyerere alikoswakoswa kwenda jela mwaka 1958 baada ya kushtakiwa na serikali ya mkoloni kuwa alitoa kauli za kashfa kwa watendaji mbalimbali wa serikali. Alikutwa na hatia na alitakiwa kufungwa jela au kulipa faini. Kwa vile walikuwa wanaelekea kwenye uchaguzi wa kwanza ambapo TANU ilikuwa inaelekea kushinda mjadala mkubwa ulikuwa ni je alipe faini au akubali kwenda jela? Yeye mwenyewe alikuwa anataka kwenda jela kama walivyokuwa wanaenda viongozi wengine wa Afrika. Lakini waasisi wenzake walimtaka akubali kulipa faini ili TANU isipoteze nafasi yake kwenye uchaguzi ule. Nyerere mwenyewe alisema kwenda jela kungekuwa ni kama “kuhitimu” katika siasa za harakati za uhuru.

  [​IMG]Mhe Godbless Lema (MB) - Arusha Mjini

  Jana huko Arusha Mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema alikubali kufanya kinyume chake. Alikuwa na uchaguzi wa kupewa dhamana katika kesi inayomhusu na kwenda zake nje na kufurahia uhuru au kwenda jela. Katika kitu ambacho alikipanga mapema Lema aliamua kwenda jela na kukataa kuwekewa dhamana. Uamuzi huu kwa baadhi ya watu unaweza kuonekana ni wa kujitafutia sifa na umaarufu wa kisiasa. Hilo siwezi kulipinga kwani Lema ni mwanasiasa na wanasiasa huhitaji umaarufu mara zote na si kosa.


  Lakini zaidi kilichonigusa mimi ni sababu alizotoa na kwanini alifikia uamuzi huo. Ninaziangalia sababu hizi kwa mwanga mpya wa kisiasa ambapo Lema amejaribu kutuma ujumbe usio na utata kuwa wanasiasa wa Tanzania hawapaswi tena kuishi kwa hofu ya kufikishwa mahakamani au kupewa vifungo kwa sababu ya harakati zao. Alichokifanya ni kutaka kutuma ujumbe kuwa watawala wetu hawawezi kutumia mahakama na polisi kama rungu la kuwatisha wanasiasa.


  Lema alisema katika taarifa iliyotangulia uamuzi wake huo kuwa “Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu. Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari”


  Aliendelea na kusema kuwa “nitaenda jela kwa hiari yangu binafsi… wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu”. Kosa kubwa ambalo lilifanywa na watu wa mahakamani labda ni kukubali kutomwachilia kwa utambulisho wake mwenyewe (self-recognizance) na hivyo kumpa nafasi. Hivi kweli Mbunge wa Jamhuri ya Muungano anaweza kufungwa kwa kosa dhamana?

  MALIZIA MAKALA HII YA KUFIKIRISHA

  KUTOKA MAKANGE BLOG
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Very interesting analysis...aksante kwa somo zuri sana Mwanakijiji!...Natamani watu wa upande wa pili wote wangalisoma hapa wafunguke!
   
 3. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi napata wasiwasi sana hivi watu na hasa viongozi wa cdm wamemuelewa Lema kweli? Kama vile sioni kuungwa mkono na viongozi wa chama chake? Kukaa ndani kwa Lema kama hakutakuwa na pressure groups za kupinga kuonewa kwake kutakuwa ni kazi bure, kabisa. Hapa ndipo palipo na ugumu wa kuendesha harakati za ukombozi na mabadiliko kwa kizazi hiki cha waTZ.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Broda,
  Usikate tamaa...unavyowaza sivyo!
  Lazima tukubali kuwa somo analotupa Lema nigumu kidogo kwenye bongo za wengi wetu!

  Mimi mwenyewe niliposikia kwa mara ya kwanza nilijiuliza mara mbilimbili kuwa ana maana gani kujitakia shida hiyo!
  Lakini siku hazigandi, walisema waswahili...anaweza akatoka bila pressure groups kureact kwa namna yoyote, lakini Historia tayari imesharekodi tukio hilo, hata mtoto kwasasa anajua juu ya tukio hilo, maana ndiyo burning issue nchini.

  Tupende tusipende, je waliomkamata Lema last time watamwendesha au kumtishia kirahisi kwa suala la jela tena pindi akianzisha harakati mtaani siku nyingine?...ni lazimam watajiuliza sana na kutafuta altenative!

  Tusitegemee mambo haya kulipuka kama petroli overnight...ni hatua...kesho tutakuwa tumesogea pale, na hatimaye nchinzima ita-take'off!
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tanzania tumekuwa chini ya uongozi wa CCM siku zote na kwa bahati mbaya sana tumekuwa na viongozi wasiosimamia chochote! Ukiondoa Mwl. Nyerere,the rest stand for nothing - absolutely nothing. Kuanzia Magogoni hadi balozi wa nyumba kumi. Matokeo yake huwezi kumuamini kiongozi kwa lolote analosema/ahidi kwa sababu hakawii kugeuka jiwe! Sote tunakumbuka speed ya Stella Manyanya mwaka 2010 na sasa. masikitiko!

  Lema is such a rare gem to to this nation such that we need to wrap him up in a cotton-wool ili asidhurike na vumbi. Ametuonesha kwa vitendo ule usemi wa 'If you have nothing to die for then you have nothing to live for'. Wako wataobeza hatua yake hii na pengine watasema anatafuta umaarufu, fine, waseme hivyo lakini watuambie wao wanasimamia nini na kwa vipi wanasimamia kile wanachoamini?
   
 6. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Atleast nimefarijika kwa maneno yako. Huyu bwana ni kiongozi wa watu tena kutoka katika chama cha siasa, wakati mwingine mimi napata taabu sana kuelewa nini kinaendelea mkuu.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  maigizo aisee....angeanza kugomea posho
   
 8. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Pamoja wakuu naunga mkono kwa asilimia zote. Lema ni shujaa
   
 9. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wanaokwenda JERA sio wote wanahatia,wengine wameenda kwa kesi za kusingiziwa.!!!!!!!!!!!!!!
  Sooon and very Soooooooooooon!!!!!!!!!
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  One-Man-Show?
  Then wengine wafanye nini?
  Wewe uta'play role gani?...
  Kuna watu bado tunaamini kuwa ukombozi wa nchi hii ni kazi ya fulani na fulani!
   
 11. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Jibu linategemea kama upo au unashabikia CCM au CUF, CDM, et al. CUF et al watabeza au kuiga. CDM wataunga mkono au kukaa kimya. CCM watabeza na kukashfu. Hii iko dhahiri kabisa.

  ...Nadhani kitendo hiki kinazaa aina mpya ya kupigana kisiasa nchini. Nategemea kuona mambo yanayovutia zaidi huko mbeleni.
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Lema kawapa hard time viongozi wa Kitaifa na kwa mwendo huu JK hana amani na kule anako omba omba pesa nk .Hakika mtaona ni jambo la kawaida lakini they are really boiling hawa watu na mwisho utaona nini kitatokea.

  Let's wait and see tarehe 14 akija mahakamani hali itakuwaje na akitoka kwa dhamani nini kitaendelea .Kuna mtu kasema hapa Lema siasa zake ni za next level si rahisi watu kuelewa na impact yake ni mbaya mno kwa wanao kandamiza na kumzonga zonga .

  Time now Chadema kupiga hodi huko JK anajieleza kuwa ni msimamizi wa utawala bora na ushahidi wa kutosha ili akumbane na maswali na aibu .
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  aisee watu tunatofautiana kuelewa na mtazamo

  mimi naamini 'confrontational politics' hazitasaidia hii nchi
  sana sana zitaleta 'machafuko'
  na watakaoumia ni wasio na hatia...mke wa lema anaweza kupanda ndege na watoto haooo nairobi au kampala

  CCM ni kama 'machizi wenye silaha'
  unahitaji kutumia 'akili' ku deal nao
  na sio kuanzisha 'mapambano'
   
 14. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wapiga kura wa arusha mwaka 2015 hawataangalia yote haya wataangalia kawafanyia nini,kwa maoni yangu huyu angefaa kuwa kiongozi kati ya viongozi wa juu Chadema amekaa kitaifa/kifikra zaidi ubunge haumfai.

  Kati ya wabunge vijana wa upinzani Lema na Sugu wamechaguliwa katika maeneo mawilii ambayo wakazi wake kwa dhati kabisa waliamua kujaribu upinzani na ingekuwa ngazi ya kuiteka mikoa hii 2015 na litakuwa kosa kubwa kwa Lema kujikita sana kitaifa au kifikra kama afanyavyo sasa ukizingatia Sugu nae kila kukicha anaongelea bifu lake na Clouds au wanamuziki wanaochipukia akiacha kiu kubwa ya wana Mbeya iliyomleta bungeni.
   
 15. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ............ni sahihi yote kwa utatu wake, kuiga na au kuunga mkono kama kuna sababu za msingi za kufanya hivyo; kubeza kwa upande moja kama ni muumini wa uvivu wa kufikiri.
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mwanaharati anaeipinga serikali
  wakati anachukua posho na shangingi juu
   
 17. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Wewe unawasiwasi gani na kuanzishwa mapambano, hiyo akili ya kupambana nao mbona hujaitoa hapa? Unachokifanya hapa ni kutishia watu na kuwakatisha tamaa wasiikabili hiyo ccm, anyway may be is your way of earning daily bread, jiulize hao watz wa kesho watakua salama kwa utaratibu huu tunaouona? Je hicho unachopigania leo kupata na kufanikisha kesho kitakuwa na maana kama mambo yenyewe yanaendeshwa kiholelaholela hivi?
   
 18. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Si la kubeza ila sidhani kama lina mshiko, au linaconnect na watanzania wengi..... even waarusha wengi. I heard life goes on as normal.
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mliambiwa tenganisheni daftari la mahudhurio na posho mkauchuna. Sasa jaribu kutenganisha ndio utajua fundi na kibarua ni nani?

  Pamoja na kejeli zenu, nina hakika next time Lema akisema jambo mtajua hatanii. He will do exactly what he says.
   
 20. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Boss usini-quote vibaya huyu jamaa namkubali sana na si mtu wa maneno yeye ni wa vitendo na kwa mbali naona tabia za Marehemu Sokoine,naona kama ubunge utambana he is destined for bigger things.

  Hilo swala la posho mimi naliona kivingine ,itakuwa na impact kama itafutwa kwa wabunge wote lakini hili la wabunge 20-30 kukataa na wengine wanachukua na hela zenyewe usidhani zitarudi hazina.
   
Loading...