Hili la Diamond Kutumbuzia AFCON

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,134
2,000
Kitendo cha Diamond kuchagulia kutumbuiza AFCON ni cha kupongezwa sana ila hakiachi tusifanye tafakuri jadidi

  1. Kwamba Mtanzania amefuzu kwenda kutumbuiza huku TIMU YA TAIFA IKISHINDWA KUFUZU kucheza soka
  2. Kwamba kwa kuwa tumeshindwa mguuni walau tumefikiriwa mdomoni
  3. Kwamba huenda soka letu ni la maneno zaidi na ndio maana tunaambiwa wacha maneno weka MUZIKI
  4. Kwamba Waziri anakabidhi bendera ya TAIFA la Tanzania kwa Diamond kwa kuwa anakwenda KUWAKILISHA TAIFA nalo ni la kupongezwa pia maana tutapata kodi
  5. ...........................................................ongeza.
  6. Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, akimkabidhi bendera msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,193
2,000
Maneno ya ridhiwan kikwete
1484191346650.jpg
 

princess ariana

JF-Expert Member
Aug 19, 2016
6,165
2,000
Sema hivi!
Bendera tumeshindwa Kuwakabidhi Michezo(Taifa Stars)

tumemkabidhi Diamond, Balozi wa Burudani(Bongo Fleva)

Aibu iliyoje kwa Taifa Stars
 

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,348
2,000
kule huendi kwa mwaliko.. bali unaenda kwa jasho..

africa mashariki yote... ameenda uganda tu kucheza mpira baada ya jasho kubwa kumtoka...

starz wazee wa excuses walitolewa mapemaaaa...

hata diamond jasho lake ndio limempa mwaliko wa kuimba kule
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,743
2,000
Dayamondi hajapelekwa Bali kaenda kwa juhudi zake usitake kuchukua credits kwa jasho la mtu mwingine. Hata Kiba akikaza sana na kuwa international anaweza kuombwa

Bendera ya Tanzania ni haki ya mtanzania yeyote sio taifa stars pekee hata wewe unaweza pewa bendera ya Tz

Taifa stars kama ilishindwa kufanya vizuri kipindi cha Kikwete haiwezi fanya vizuri tena
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom