Waziri Dr. Mwakyembe tuitengeze hii Single ya "SOKA LA VIJANA" hakika tupata views nyingi kuliko nyimbo zote za Diamond YouTube

Wuondruok

Senior Member
Jul 2, 2019
127
250
Heshima kwako Waziri Mwakyembe na Wizara yako nzima katika kuhakikisha tunatoka hapa tulipo.
Wewe binafsi na watanzania wote kwa ujumla tunatamani kuiona bendera ya Taifa letu ikipepea kwenye nyanja ya michezo kimataifa. Lakini kupata hayo mafanikio vilevile tunahitaji kufuata njia stahiki.
Nikiongelea Soka ambao ndo mchezo pendwa hapa kwetu, bado tumesinzia tena usingizi mzito usioeleweka kikomo.
Ndugu Waziri kwa kuliona hilo na matokeo tuliyoyapata Afcon umekuwa mara nyingi ukizumgumzia wingi wa wachezaji wa kigeni ndo unatupoteza, jambo ambalo linazua mijadala kwa sisi tunaoutakia mema mpira wetu.
Hivi ni kweli hii ndo sababu ya sisi kuendelea kuwa kichekesho kwenye soka?
Ndugu Waziri dunia sasa ni Kijiji na yote yanaendelea huko kwa waliondelea wote sisi ni mashahidi
Ni kweli tunahitaji vijana wetu wapate exposure na experience ya mechi za kimataifa? Sasa swali tunalojiuliza hao vijana wako wapi? Hakika Tanzania tumebarikiwa kuwa na vipaji vingi za soka ila KIPAJI bila MAARIFA ni kazi bure. Leo hii tunatoa mfano wa Samatta ila tujiulize kuwa tutategemea bahati kama za akina Samatta mpaka lini? Tusubiri miaka mangapi tupate bahati ya kuwa na akina Samatta 23 waje watusaidie?
Ni wazi kuwa tunataka Short cut ya kufanikiwa kwa njia ambao siyo. Tunataka tuamini kuwa kama tukicheza wazawa watupu basi tutafika mbali? Sasa hao wazawa tunaotaka wacheze wamepewa maarifa yapi ya ziada ya soka ukitoa KIPAJI chao?
Sasa tujiulize tuna ligi ya kutengeneza ushindani kimataifa? Ligi ambayo mshahara, usafiri na malazi ni kizungumkuti itatoa mazao yapi?
Kwakweli kama tunataka tulikwamua soka letu basi ni wazi Serikali inahitajika KUPANDA MBEGU kwenye hili kwa KUANZA na watoto.. Nasema kuwa Serikali inahitajika kwasababu tunajidanganya kusema kuwa vilabu ambavyo hata timu ya kwanza inawashinda ije itengeneze wachezaji wa maana..
Mfano mdogo Yanga imewafanyia watoto usaili kwa ajili ya timu za watoto, ila swali hawa watoto watafundishiwa na kucheza viwanja vipi? Je kweli Yanga wana vifaa vinavyohitajika kwenye kufundishia watoto wafanane kiuwezo na wale wa EDUKICK au itaishia kwenda kuwakimbiza watoto riadha tu?.. Ni wazi tunafahamu uwekezaji kwenye soka hasa la watoto si suala la mzaha kama tunavyolichulia.
Swali lingine sisi kama nchi kupitia TFF je tuna MTAALA wowote kwa hawa vijana au kila mtu afundishe akijuacho?
Je TFF kama wasimamizi wa Soka letu wana MIPANGO yoyote ya MUDA mrefu kwa watoto wa nchi hii?
Kweli wazawa ndo Taifa Stars ila Ligi ni steji ya pili baada ya kuwatengeneza.
Hapo bado hatujaongelea kama kweli tuna ligi ya Vijana tukiachana na huu mfano wa ligi ya Vijana tulionayo.

USHAURI

Serikali yenyewe inaweza Kusimamia hili suala na tukafanikiwa. Kwakuwa tayari TFF imeshapewa kiwanja Kigamboni basi tuhakikishe kituo kinajengwa kikiwa kikamilifu. Vijana wataozalishwa hapa na kuonekana wameiva vizuri wale FIRST CLASS wawe wanatafutiwa timu za nje hasa za ULAYA hata wakicheza kwa mikopo ili wakapate kufunguka zaidi kisoka waje waitumikie TAIFA STARS. Na wale wengine wasambazwe kwenye timu za Africa na humuhumu kwetu. Tukifanya haya kwa miaka 5 mpaka 10 tutakuwa pengine kabisa......Sasa hapo Ndugu Waziri wangu ndo mje na Mkakati wa KUPUNGUZA wachezaji wageni kwakuwa tayari MNA KIWANDA ENDELEVU CHA VIJANA, ambapo mtawapa VILABU TIMEFRAME inayoeleweka na kuwataka kuwa baada ya miaka pengine mitano mtaruhusu wachezaji watano au watatu. Lakini huku kutukurupusha haitotusaidia chochote zaidi kuwa ni SIASA zisizo na msaada kwa Taifa.

Linapokuja suala la GHARAMA za kulea hawa vijana, nchi hii ina utitiri wa makampuni ya MICHEZO YA KUBAHATISHA zaidi ya 100 ambayo hayana msaada kwa vijana zaidi ya kuchota hela kutoka kwa watanzania. Kama wakiwekewa kipengele cha kuchangia kwa lazima pale wanapotaka ku-renew leseni zao au kwa awamu za kila mwezi kwa mwaka mzima hatutokosa pa kuanzia. Kwasababu nakumbuka hata Abass Tarimba wa SPORTPESA aliwahi sema kuwa Serikali inabidi iangalie njia ambayo haya makampuni ya Bahati Nasibu yatasaidia Michezo. Kwahiyo hili wazo siyo kitu cha ajabu wala kigeni kwakuwa ni mawazo yanayoishi akilini mwa watu.
Hapa nimekumbuka na TFF kuingia mkataba na Shule ya Dodoma kukuza watoto, hivi hii shule ina vifaa na walimu aina gani watakaofanya kazi hii? Hiyo shule mbona hatujaona zao lolote la michezo nikitoKEa hapo? Tunarudi kule kule tulikofeli kwa kukimbia majukumu na kutafuta shortcut ambayo hata Malinzi na Alliance hawakutafikisha popote kwenye AFCON U17


Naonavyo Serikali mnataka kujitoa kwenye nafasi yenu. Mnataka vilabu vitengeneze vijana sawa, sasa hao vijana wanatengenezwaje bila hivyo vilabu kuwa na misuli ya pesa.. na kila mtu anafahamu kuwa huu ukosefu wa fedha kwa hivi vilabu hausababishwi na wao wenyewe bali mfumo wenyewe wa michezo wa nchi yetu haupo rafiki kwa michezo......hapo tutaendelea kuota kama tunataka Ndanda FC na Lipuli FC watutengenezee watu wa kuitoa Tanzania kweli hili shimo..

MAWAZO YANGU NI HAYO.....
 
  • Thanks
Reactions: Auz

Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
6,646
2,000
Mpira ni vipaji na kupata vipaji ni majaliwa kuna nchi wana kila kitu kuhusu mpira lakini tatizo vipaji
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom