Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 297
- 285
Mimi Rashda Zunde, naamini kwamba hatua za serikali za kutafuta kampuni yenye uwezo na uzoefu mkubwa katika uendeshaji wa bandari duniani kwa teknolojia za kisasa kuiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kufanya kazi kwa ufanisi, kuongeza mapato ya nchi na kuchangiza sekta nyingine za kiuchumi, kumefanyika kwa nia ya njema na itazaa matunda mema.
Katika hili, wananchi ni vyema tukasikiliza viongozi wanasemaje kuhusu ubora wa kampuni ya DP World, ambayo imeonesha kuwa na utaalamu, uwezo na uzoefu mkubwa katika uendeshaji wa bandari 190 katika nchi 68 barani Afrika, Asia, Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini.
Tukumbuke pia kuwa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii na Dubai ni kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari nchini, hivyo ni muhimu wananchi wakaona umuhimu wa mageuzi yanayotakiwa ili kuleta tija na ufanisi.
Kutokana na mipango maridhawa ya serikali ya kupaisha ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam, natoa wito wananchi wenzangu kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuacha kuruhusu mgawanyiko wa aina yoyote kuhusu uwekezaji wa bandari huku tukiepuka kujadili itikadi za kisiasa, udini, ukabila, ukanda au vyovyote vile kuhusiana na mradi huo mkubwa wa kitaifa.