Hili jambo limeniumiza sana

Hili jambo limeniumiza sana

Mama si mungu na hawezi kuwa mungu wala mzazi yeyote hawezi pata nafasi ya umungu kwa namna yoyote
hekima ya mungu haipimiki hata kidogo na mungu hawezi fanya makosa ya dhihaka namna hiyo, mungu hafikiriki
mama yako ana makosa sana na imeniuma kwa kweli
Inaumiza sana kila Mara naishia kulia tu
 
doh! pole sana asee
tulia fanya uchunguzi simple tu ujue shida ni nini mpka atamke vile labda alkua too emotional au kuna kitu kingine
all in all pole sana unaweza sameh pia maisha yakaendelea japo ni ngumu
Ata akitulizwa alikuwa akiendelea kutoa maneno Yale makali naona alikuwa ameadhimia
 
Mama ni Mungu wa Pili katika dunia hii. Hakuna kitu kibaya kama kumchukia Mama. Unachopaswa kufahamu kuwa hakuna mwanadanu aliyekamilika. Hivyo uambie moyo wako kuwa huyu ni mama yangu na vyovyote itakavyokuwa atabaki kuwa mama yangu. The rest mwachie Mungu. Hata kama utaamua kumchukia haitasaidia. Nakusihi mlipe kwa wema hadi ajue kama wewe unampenda hata kama yeye hakupendi. Ukifanya hivyo Mungu ipo siku atakufanyia wepesi katika mambo yako na familia yako kwa ujumla.

Wahenga walisema: mpe mchawi akulelee mwanao...
Ushauri mzuri kweli nadhani ataufanyia kazi ipasavyo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Dada yangu ila nachokuomba jaliribu kutafuta muda mzuri umkalishe mama umuulize niwapi ulimkosea iliumuombe msamaha na wewe pia urudishe moyo umpende mama kwasababu ndo ndugu yako pekee wakaribu ulienae ndo mzazi wako pekee aliebaki miezi tisa uko tumboni mwake ,kifuachake ndo ulipata chakula chako ujui mangapi alipitia kukikisha unakua salama muda wote ilijinyima aliumia kwa ajili yako simaanishi humpendi la hasha ila namaanisha umsamehe mama nakutakia malidhiano mema na mama.....amina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siri kubwa sana hapo. Mungu sio Athuman au John. Mama kamkufuru Mungu. Ngumu lakini msamehe, ikibidi akuleze chuki yake kwako chanzo nini?
Nashindwa hata kumuangalia usoni ila itabidi nakae chini nimuulize kitendo cha yeye kufikia kuniombea Mimi kufa.
 
Ni kweli maneno hayo yanaumiza sana wala si rahisi kwa mtu yeyote asikie neno au jambo baya anaambiwa hususani mzazi/wazazi.

Kwanza nianze kwa kukupa pole mno maana hiyo ni moja ya changamoto katika maisha ya mwanadamu.
Kwa ushauri wangu ambao kidogo itakuweka sawa kisaikolojia, ni kwamba unapaswa kuvumilia na hali ambayo unayo kwa sasa na vizuri ukaenda kwa mama yako mzazi mkawa na maongezi yenu binafsi tena ya kina.
Onesha furaha pindi unapoenda kuongea na mama yako, hata kama bado unaumia lakini ni vyema uachie tabasamu pindi upo na mama yako,

Anza kuongea naye kwa udadisi wa kina ili kujua zaidi chanzo cha yeye kusema na kuonesha kitendo cha kutaka wewe ungetangulia kuaga dunia.
Pia naamini utakuwa na hisia kali pale mtakapo kuwa na maongezi wenu unaweza kumhoji kwa maswali haya,

1. Mama unajua nakupenda na nimetimiza wajibu wangu wa kukupenda wewe kama mwanao, na ni haki yako kupendwa zaidi neno upendo, lakini kwa jambo ambalo limetokea msibani mpaka kwenye mazishi kusema kuwa " bora ningekufa mimi na isiwe mdogo wangu" ulikuwa na maana gani hasa kuongea maneno mazito tena mbele za watu, huoni ya kwamba nimedhalilika na kuonesha tatizo/ utofauti katika familia yetu....??

2. Ni kitu gani hasa nimekukosea mama yangu mpaka ukaamua kufikia kutamka maneno mazito kama hayo, au nimekukwaza kwa jambo gani mama yangu, najua thamani ya upendo wako na napenda uwe na amani moyoni, nitaacha kufanya jambo ambalo limekukera, ( atoe sababu za msingi kama anazo na wewe uzipitie kwa makini ukiridhia nazo acha kabisa )

Aghalabu wazazi wanapenda watoto wao kwa namna moja ama nyingine lakini si mbaya na wewe ukamwambia maoni yako juu ya maamuzi yako uliyofikia.
( mfano )
Mueleze kuhusu mahusiano yako, mambo yako ambayo unataka yaende vipi kwa misingi yako/ sababu zako, msimamo wako katika mambo yako kwa ujumla,

Mweleze nafasi uliyonayo kwa sasa ni kuamua maisha yako yaende vipi, wala mwingine hana haki ya kukulazimisha zaidi ya ushauri/maoni.
Mueleze mama yako mzazi kila kitu akifahamu kuhusu misimamo yako na haki zako, endapo atakuewelewa haina shida,

Pia kama hutopenda kuwa na mambo mengi na kuzuia jambo hili lisiwe kubwa katika familia na hata kwa ndugu zenu, fanya jambo gumu kidogo.

Mfuate mama yako mzazi ikiwemo na ndugu kama wataweza kufika uwaambie kuwa umeamua kumsamehe mama yako kwa yote yaliyo tokea na awe na amani moyoni, kisa Fanya mambo yako mengine, kwa hakika mama yako kama mtu mzima ataweza kufikiria vyema atakuwa karibu na wewe maana hawezi kuwa mpweke kwa sasa.

Fanya kama hakuna kilichotokea na ufanye mambo mengine ya muhimu, kwa haya ni maisha tu yanapita na yana mwisho wake wala usiumie sana na jaribu kutowaza sana suala hili angalau kidogo upunguze maumivu.

Pole sana kwa msiba, pole mno kwa mazito yaliyokukuta, nakutakia maisha mema....
Ahsante sana kwa ushauri nitajitahidi kufanya hivyo
 
Halafu kitu kingine hapo ndugu ni kwanini alikuwa anampenda ndugu yako umesema hataki mahusiano yako na mpenzi wako ulijaribu kumuuliza ni kwanini hamtaki unajua pia wazazi hupenda mtoto anaye msikiliza japo naye kulia kwakutàmka ni bora ungekufa wewe sio vizuri tuliza pressure na umsamehe tu maana umebaki wewe na yeye baba kafariki na mdogo wako pia, pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakumpenda kutokana na kabila pia alitaka niwe na mahusiano na kijana wa rafiki yake jambo ambalo sikulihafiki.
 
Dah! Pole sana na una kila sababu ya kuumia na kushangazwa na kilio cha mama yako kuombea kwamba ungekufa wewe badala ya nduguyo. Kwa sababu amegundua kosa lake na kuja kukuomba msamaha basi msamehe tu lakini kamwe huwezi kusahau hiki kilio chake cha kustaajabisha sana cha mzazi kuomba motto aliye hai ndiye angekufa badala ya huyo marehemu, pole sana.
Inauma sana
 
Hata hasingetamka kwa kinywa angetamka moyoni, believe me wazazi wengi hutamka hivyo moyoni.
Kikubwa ni wewe kujitazama na kujirekebisha kasoro zinazokuweka mbali na mama yako. Mama yako kutokupenda kulianza ulipokuwa mkubwa ulikuwa ukifanya machukizo machoni pake,hukumpa kipaumbele Kama mama, angekuwa hakupendi tangu mwanzo angeku- destroy tangu mimba yako ilipotungwa au tangu ulipoigusa dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachotuumiza katika mapendo ni kutaka kuona ama kuamua mapendo yatoke wapi. Angalia waliokuzunguka, umezungukwa na upendo mwingi wa kutosha. Isitoshe Yuko Mungu anaesema kabla ya kuwekwa kwa misingi ya dunia alikujua. Yaani akishakupenda Yeye Haijalishi kama mama anakupenda ama la. msamehe mama yako, ana matatizo yake ambayo Wewe hujahusika Nayo. Halafu mhurumie ili auone upendo wa agape ulio ndani yako, usio na sababu wala mipaka. Msaidie amuone Mungu kupitia Wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante sana ubarikiwe
 
Back
Top Bottom