Hili jambo limeniumiza sana

Hili jambo limeniumiza sana

Pole sana,

MSAMEHE, KISHA SONGA MBELE ACHANA NAE, NIKIWA NA MAANA KAA NAE MBALI KABISA.

hapo umeongea huo msamaa ni bas tu kujistukia ila pale kwenye kustresika ndio ulikuwa uhalisia wake akae mbali na huyo mama ni mwanga tu yaani aweke unafiki pembeni mama aendelee na yake na mtoto afanye yake
 
Ni kweli maneno hayo yanaumiza sana wala si rahisi kwa mtu yeyote asikie neno au jambo baya anaambiwa hususani mzazi/wazazi.

Kwanza nianze kwa kukupa pole mno maana hiyo ni moja ya changamoto katika maisha ya mwanadamu.
Kwa ushauri wangu ambao kidogo itakuweka sawa kisaikolojia, ni kwamba unapaswa kuvumilia na hali ambayo unayo kwa sasa na vizuri ukaenda kwa mama yako mzazi mkawa na maongezi yenu binafsi tena ya kina.
Onesha furaha pindi unapoenda kuongea na mama yako, hata kama bado unaumia lakini ni vyema uachie tabasamu pindi upo na mama yako,

Anza kuongea naye kwa udadisi wa kina ili kujua zaidi chanzo cha yeye kusema na kuonesha kitendo cha kutaka wewe ungetangulia kuaga dunia.
Pia naamini utakuwa na hisia kali pale mtakapo kuwa na maongezi wenu unaweza kumhoji kwa maswali haya,

1. Mama unajua nakupenda na nimetimiza wajibu wangu wa kukupenda wewe kama mwanao, na ni haki yako kupendwa zaidi neno upendo, lakini kwa jambo ambalo limetokea msibani mpaka kwenye mazishi kusema kuwa " bora ningekufa mimi na isiwe mdogo wangu" ulikuwa na maana gani hasa kuongea maneno mazito tena mbele za watu, huoni ya kwamba nimedhalilika na kuonesha tatizo/ utofauti katika familia yetu....??

2. Ni kitu gani hasa nimekukosea mama yangu mpaka ukaamua kufikia kutamka maneno mazito kama hayo, au nimekukwaza kwa jambo gani mama yangu, najua thamani ya upendo wako na napenda uwe na amani moyoni, nitaacha kufanya jambo ambalo limekukera, ( atoe sababu za msingi kama anazo na wewe uzipitie kwa makini ukiridhia nazo acha kabisa )

Aghalabu wazazi wanapenda watoto wao kwa namna moja ama nyingine lakini si mbaya na wewe ukamwambia maoni yako juu ya maamuzi yako uliyofikia.
( mfano )
Mueleze kuhusu mahusiano yako, mambo yako ambayo unataka yaende vipi kwa misingi yako/ sababu zako, msimamo wako katika mambo yako kwa ujumla,

Mweleze nafasi uliyonayo kwa sasa ni kuamua maisha yako yaende vipi, wala mwingine hana haki ya kukulazimisha zaidi ya ushauri/maoni.
Mueleze mama yako mzazi kila kitu akifahamu kuhusu misimamo yako na haki zako, endapo atakuewelewa haina shida,

Pia kama hutopenda kuwa na mambo mengi na kuzuia jambo hili lisiwe kubwa katika familia na hata kwa ndugu zenu, fanya jambo gumu kidogo.

Mfuate mama yako mzazi ikiwemo na ndugu kama wataweza kufika uwaambie kuwa umeamua kumsamehe mama yako kwa yote yaliyo tokea na awe na amani moyoni, kisa Fanya mambo yako mengine, kwa hakika mama yako kama mtu mzima ataweza kufikiria vyema atakuwa karibu na wewe maana hawezi kuwa mpweke kwa sasa.

Fanya kama hakuna kilichotokea na ufanye mambo mengine ya muhimu, kwa haya ni maisha tu yanapita na yana mwisho wake wala usiumie sana na jaribu kutowaza sana suala hili angalau kidogo upunguze maumivu.

Pole sana kwa msiba, pole mno kwa mazito yaliyokukuta, nakutakia maisha mema....
 
Msamehe mama yako hakuna Aliye Kama Mama.

Hivyo, jitie nguvu na ubadilike maana wewe ni Mmmmmmmmh, nitarudi tena toleo lijalo.
Ila tabia yako ni mbaya sana, hebu ona picha uliyoweka tu hapa JF hata kama siyo wewe ila inaogopesha.
 
Halafu kitu kingine hapo ndugu ni kwanini alikuwa anampenda ndugu yako umesema hataki mahusiano yako na mpenzi wako ulijaribu kumuuliza ni kwanini hamtaki unajua pia wazazi hupenda mtoto anaye msikiliza japo naye kulia kwakutàmka ni bora ungekufa wewe sio vizuri tuliza pressure na umsamehe tu maana umebaki wewe na yeye baba kafariki na mdogo wako pia, pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama ni Mungu wa Pili katika dunia hii. Hakuna kitu kibaya kama kumchukia Mama. Unachopaswa kufahamu kuwa hakuna mwanadanu aliyekamilika. Hivyo uambie moyo wako kuwa huyu ni mama yangu na vyovyote itakavyokuwa atabaki kuwa mama yangu. The rest mwachie Mungu. Hata kama utaamua kumchukia haitasaidia. Nakusihi mlipe kwa wema hadi ajue kama wewe unampenda hata kama yeye hakupendi. Ukifanya hivyo Mungu ipo siku atakufanyia wepesi katika mambo yako na familia yako kwa ujumla.

Wahenga wakisema: mpe mchawi akulelee mwanao...
Hapana...
Mungu hana madaraja....
 
Kuna tatizo lingine zaidi ya huyo mpenzi wako.
Je? Huko nyuma uliwahi fanya tukio kubwa la kumuuiza.
 
Habari zenu jamani

Katika familia yangu tumezaliwa wawili Mimi nikiwa ndiye mtoto wa kwanza alafu akafwata midogo wangu ambaye tayari ni marehemu mwezi sasa umepita.....nimebaki Mimi na mama yangu baba alishafariki miaka imepita.

Kabla ya mdogo wangu kufariki alikuwa ni kipenzi cha mama sana hilo halikuwa linanisumbua niliona kawaida sana pia hiyo ilitokana na mahusiano ya mpenzi niliekuwa nae mama hakumpenda sana jambo hilo lilifanya Mimi na mama yangu tusiwe na maelewano.
Kitu kilichokuja kuniumiza na nimuone mama tofauti ni siku mdogo wangu alipofariki mama alikuwa akilia wa nguvu na huku akilitaja jina la mdogo wangu na Mimi.......nanukuu( BORA USINGEONDOKA WW KIPENZI CHANGU ANGEONDOKA DADA YAKO (yani mimi)INGEKUWA AFADHARI.
Maneno hayo halikuwa akiyarudia kuanzia mwanzo wa msiba mpaka anazikwa jambo hili liliwashangaza wengi na liliniumiza sana mpaka Leo nikikumbuka Yale roho inaniuma sana nashindwa hata kumuangalia mama yangu naishia kulia.
Pengine nimemkosea mama yangu sana lkn sikutegemea kama anaweza kuombea Mimi kufa imeniumiza sana.
Amekuja leo na baadh ya ndugu akiomba msamaha sijasema chochote nimeishia kulia.nataman niende mbali kwasababu nimejua Mimi si chochote kwake.

Mwenye ushauri au mawazo yoyote kisaikolojia siko sawa.
Tafuta mwanaume mwenye pesa,mama atashika adabu.
 
Dah! Pole sana na una kila sababu ya kuumia na kushangazwa na kilio cha mama yako kuombea kwamba ungekufa wewe badala ya nduguyo. Kwa sababu amegundua kosa lake na kuja kukuomba msamaha basi msamehe tu lakini kamwe huwezi kusahau hiki kilio chake cha kustaajabisha sana cha mzazi kuomba motto aliye hai ndiye angekufa badala ya huyo marehemu, pole sana.

Habari zenu jamani

Katika familia yangu tumezaliwa wawili Mimi nikiwa ndiye mtoto wa kwanza alafu akafwata midogo wangu ambaye tayari ni marehemu mwezi sasa umepita.....nimebaki Mimi na mama yangu baba alishafariki miaka imepita.

Kabla ya mdogo wangu kufariki alikuwa ni kipenzi cha mama sana hilo halikuwa linanisumbua niliona kawaida sana pia hiyo ilitokana na mahusiano ya mpenzi niliekuwa nae mama hakumpenda sana jambo hilo lilifanya Mimi na mama yangu tusiwe na maelewano.
Kitu kilichokuja kuniumiza na nimuone mama tofauti ni siku mdogo wangu alipofariki mama alikuwa akilia wa nguvu na huku akilitaja jina la mdogo wangu na Mimi.......nanukuu( BORA USINGEONDOKA WW KIPENZI CHANGU ANGEONDOKA DADA YAKO (yani mimi)INGEKUWA AFADHARI.
Maneno hayo halikuwa akiyarudia kuanzia mwanzo wa msiba mpaka anazikwa jambo hili liliwashangaza wengi na liliniumiza sana mpaka Leo nikikumbuka Yale roho inaniuma sana nashindwa hata kumuangalia mama yangu naishia kulia.
Pengine nimemkosea mama yangu sana lkn sikutegemea kama anaweza kuombea Mimi kufa imeniumiza sana.
Amekuja leo na baadh ya ndugu akiomba msamaha sijasema chochote nimeishia kulia.nataman niende mbali kwasababu nimejua Mimi si chochote kwake.

Mwenye ushauri au mawazo yoyote kisaikolojia siko sawa.
 
Habari zenu jamani

Katika familia yangu tumezaliwa wawili Mimi nikiwa ndiye mtoto wa kwanza alafu akafwata midogo wangu ambaye tayari ni marehemu mwezi sasa umepita.....nimebaki Mimi na mama yangu baba alishafariki miaka imepita.

Kabla ya mdogo wangu kufariki alikuwa ni kipenzi cha mama sana hilo halikuwa linanisumbua niliona kawaida sana pia hiyo ilitokana na mahusiano ya mpenzi niliekuwa nae mama hakumpenda sana jambo hilo lilifanya Mimi na mama yangu tusiwe na maelewano.
Kitu kilichokuja kuniumiza na nimuone mama tofauti ni siku mdogo wangu alipofariki mama alikuwa akilia wa nguvu na huku akilitaja jina la mdogo wangu na Mimi.......nanukuu( BORA USINGEONDOKA WW KIPENZI CHANGU ANGEONDOKA DADA YAKO (yani mimi)INGEKUWA AFADHARI.
Maneno hayo halikuwa akiyarudia kuanzia mwanzo wa msiba mpaka anazikwa jambo hili liliwashangaza wengi na liliniumiza sana mpaka Leo nikikumbuka Yale roho inaniuma sana nashindwa hata kumuangalia mama yangu naishia kulia.
Pengine nimemkosea mama yangu sana lkn sikutegemea kama anaweza kuombea Mimi kufa imeniumiza sana.
Amekuja leo na baadh ya ndugu akiomba msamaha sijasema chochote nimeishia kulia.nataman niende mbali kwasababu nimejua Mimi si chochote kwake.

Mwenye ushauri au mawazo yoyote kisaikolojia siko sawa.

Ni muhimu aseme sababu ya hayo maneno... Mama ni Mungu ni nani,nonsense.... ni muuaji... atoe sababu.... kaa naye mbali huyo asije kukuua
 
Kwa kweli inauma sana na polee sana,naamini kuna mahali umemkosea mama yako au pengine ulikuwa haumjali wala kuwa naye karibu ,wamama wengi ambao ni watu wazima ambao wamefiwa na waume zao,mara nyingi watoto uwa faraja yao.cha msingi muombe mama radhi na ujue tofauti zilikuwa wapi na uziweke sawa.kukimbia mji/mkoa hakuwezi kukusaidia kitu,kumbuka alikubeba miezi tisa tumboni,kwaiyo utarudi tuh kwake.onyo;punguzeni kiburi Kwa wazazi wenu!achane maisha ya kuiga.mama ndio Mungu wako wa pili.
 
Mama ni Mungu wa Pili katika dunia hii. Hakuna kitu kibaya kama kumchukia Mama. Unachopaswa kufahamu kuwa hakuna mwanadanu aliyekamilika. Hivyo uambie moyo wako kuwa huyu ni mama yangu na vyovyote itakavyokuwa atabaki kuwa mama yangu. The rest mwachie Mungu. Hata kama utaamua kumchukia haitasaidia. Nakusihi mlipe kwa wema hadi ajue kama wewe unampenda hata kama yeye hakupendi. Ukifanya hivyo Mungu ipo siku atakufanyia wepesi katika mambo yako na familia yako kwa ujumla.

Wahenga wakisema: mpe mchawi akulelee mwanao...
That's true ushaur mzur sana

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Habari zenu jamani

Katika familia yangu tumezaliwa wawili Mimi nikiwa ndiye mtoto wa kwanza alafu akafwata midogo wangu ambaye tayari ni marehemu mwezi sasa umepita.....nimebaki Mimi na mama yangu baba alishafariki miaka imepita.

Kabla ya mdogo wangu kufariki alikuwa ni kipenzi cha mama sana hilo halikuwa linanisumbua niliona kawaida sana pia hiyo ilitokana na mahusiano ya mpenzi niliekuwa nae mama hakumpenda sana jambo hilo lilifanya Mimi na mama yangu tusiwe na maelewano.
Kitu kilichokuja kuniumiza na nimuone mama tofauti ni siku mdogo wangu alipofariki mama alikuwa akilia wa nguvu na huku akilitaja jina la mdogo wangu na Mimi.......nanukuu( BORA USINGEONDOKA WW KIPENZI CHANGU ANGEONDOKA DADA YAKO (yani mimi)INGEKUWA AFADHARI.
Maneno hayo halikuwa akiyarudia kuanzia mwanzo wa msiba mpaka anazikwa jambo hili liliwashangaza wengi na liliniumiza sana mpaka Leo nikikumbuka Yale roho inaniuma sana nashindwa hata kumuangalia mama yangu naishia kulia.
Pengine nimemkosea mama yangu sana lkn sikutegemea kama anaweza kuombea Mimi kufa imeniumiza sana.
Amekuja leo na baadh ya ndugu akiomba msamaha sijasema chochote nimeishia kulia.nataman niende mbali kwasababu nimejua Mimi si chochote kwake.

Mwenye ushauri au mawazo yoyote kisaikolojia siko sawa.
Nivigumu kufahamu umuhimu wako ila kwasasa ataujua kwani alicgo kipenda hakipo tena bac ww kama ww inakupasa uzdishe mapenzi kwa mama yako ili pia afahamu umuhimu wako japo kuna siri nzito hapo kat ya mama yako na huyo mdogo wako ambaye aliye fariki.
 
Kinachotuumiza katika mapendo ni kutaka kuona ama kuamua mapendo yatoke wapi. Angalia waliokuzunguka, umezungukwa na upendo mwingi wa kutosha. Isitoshe Yuko Mungu anaesema kabla ya kuwekwa kwa misingi ya dunia alikujua. Yaani akishakupenda Yeye Haijalishi kama mama anakupenda ama la. msamehe mama yako, ana matatizo yake ambayo Wewe hujahusika Nayo. Halafu mhurumie ili auone upendo wa agape ulio ndani yako, usio na sababu wala mipaka. Msaidie amuone Mungu kupitia Wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom