kilalile
JF-Expert Member
- Jun 4, 2012
- 1,594
- 2,207
Wapo baadhi ya wazazi wasiojitambua huelekeza mapenzi yao kwa mtoto mmoja kati ya wengi aliozaa bila kificho, na wakati mwingine huonyesha chuki kwa mtoto mmoja kati ya wengi aliozaa bila kificho.
Cha ajabu, mtoto anaependwa na mzazi kisha akajua yeye anapendwa sana huwa hawanaga mwisho wa kupendeza. Na pale inapotokea mtoto asiyependwa kuja kupata mafanikio, hujikuta hakumbuki nyumbani kwao kwa lolote. Jamii inayomzunguka humuona wa ajabu sana kwa kutokumbuka kwao. Jamii inachopaswa kuelewa ni kuwa mapenzi ya mzazi na mtoto hujengwa katika kile kipindi ambacho mtoto ni tegemezi, akivuka hapo bila kuwa na mapenzi nawe, imekula kwako, uwe mzazi au mlezi.
Kinachobaki ni huruma ya mtoto ya kuzaliwa.