Hili basi ni balaa jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili basi ni balaa jamani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Simba Mkali, Feb 15, 2012.

 1. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kuna basi moja linafanya kazi ya kusafirisha abiria kati ya Dar es Salaam hadi Mwanza, linaitwa Muro kila siku linalaza abiria njiani, yaani bovu ile kinoma. Mbaya zaidi linapoharibika hakuna msaada wowote unaotolewa na wahusika, hapo ndipo inapokuwa mwisho wa mchezo, aidha abiria watafute usafiri mwingine au walale kwenye basi (kama ni usiku) hilo hadi kesho yake. Jamani haya si mateso jamani. Kwani linaruhusiwa kutembea au ni la mkubwa. Nani anayejua habari zake atuhabarishe?
   
 2. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwenye red kama ni kweli basi hatari sana.

   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Badilisha aina ya usafiri.
   
 4. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Panda Mohamed Trans au Mombasa Raha..
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwani Mwanza kuna bus hilo hilo moja? Badilisha usafiri mkuu
   
 6. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  muro au princess muro???
   
 7. m

  mnyakyusa JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 248
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwani hamna mabsi mengine???? Unalalamika utadhani ndege ya kwenda Kigoma ambayo iko moja tu ATC
   
 8. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mimi sipandi tena, ila tatizo ni ndugu zetu wengine wa Kitanzania bado wapanda likija kuleta madhara si tutalia wote kama tulivyolia kwenye MV Spice, kwanini tusichukue tahadhari mapema?
   
 9. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Labda nauli yake ni ndogo!
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  na vya bure gharama
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Duh umenikumbusha ndio ilikua mara yangu ya kwanza kwenda Kigoma, ndio nikaambiwa linaenda huko, balaa yaani kahama saa tano usiku ndio tunafika na kum,be linaishia hapo
   
 12. g

  gadi New Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muro hakuna gari pale
   
 13. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wengine mna majibu ya kukera sana, kutoa taarifa imeshakuwasoo..! Ametoa taarifa ili yeyote atakayesafiri kuelekea huko asilipande litamletea usumbufu. Kama yeye akibadili gari akawa anapanda aina nyingine ya bus bila kutoa taarifa sisi tutajuje? Si tutaingia mkenge kama yeye? . Mkuu big up 4 your information.
   
 14. P

  PAFKI Senior Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Jamani sio utani huyo jamaa kawatahadharisha tu,ilisha,ilishanitokea mimi nilikuwa nakwenda KAHAMA liliharibika si chini ya mara nne na tulilala Manyoni,Chalinze walikaza tairi,Kibaigwa ilifungukaka shafti,Bahi ikatoboka rejeta na tukawa tunaenda kama kobe na madumu ya maji ili isichemshe,wakalazimisha tupite usiku saa 9 manyoni watu wakakataa tukasubiri asubuhi wakalitengeneza,Tulifika KAHAMA saa 11 jioni.
  Pale ubungo wanafanya uhuni wanakukatia Alliys ukifika muda wa kuondoka wanakwambia alliys mbovu ndo wanaleta mifupa yao, nilisafiri kwakuwa nililazimika kuondoka siku hiyo na mabasi mengine yalishatoka na kurudisha nauli ingelichukua muda sana.
  KWELI MURO SIO BASI HATA KIDOGO.
   
 15. P

  PAFKI Senior Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Yote ni yaleyale mmiliki wake ni mmoja.
   
 16. mchambuzixx

  mchambuzixx JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 1,294
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  mwanza magari ya uhakika ni haya 1. allys 2.green star 3. darlux 4. princess shabaha 5 akamba...... na ukitaka ufike dar mapema au mwanza mapema by saa2 panda Allys ila nauli 45000 ...yaliyobaki ndugu kama vile mohamed,mombasa, zuber,muro na mengineyo kama unataka kutekwa au kuliwa kiboga maeneo ya usagara wkt unatoka dar panda ila uandae kyjel kabisa kama ww mwanaume
   
 17. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Aksante tutaliepuka... hata ukiliangalia kwa nje limekaa kishari shari vile...
   
 18. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  best line, master line ni bora ulale stendi kuliko kupanda haya mabasi, kulala njiani ni nje nje halafu machafu mpaka kunguni ndani. mabasi mazuri mwanza-dar ni green star 2. lucky star, 3. allly's (yanakwenda kasi sana ni hatari) nikikosa haya huwa na ahirisha safari
   
 19. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante kwa taarifa mkuu,Nilienjoy kusafiri na Allys kwenda mwanza nakurudi na ilikua mara yangu ya kwanza kiukweli huwa sisahau ile safari!
   
Loading...