Kwanza tuondoe mitazamo ya kwamba heti lugha ya Kiswahili haikidhi haja kutokana na kuwa na misamiati michache. Halafu 'kuchocha' ni neno linaloweza kutumika kuwa mbadala wa hilo neno la kiingereza,kwa maana kinachoangaliwa katika mazungumzo ni dhana gani inalengwa wakati huo,. Lakin sisi wenye lugha yetu kwanza tumekuwa wavivu wa kutafuta miamiati mipya kutokana na kujenga mitazamo mibovu katika lugha yetu. Pia tukumbuke katika kuunda misamiati ya lugha kuchukua misamiati kutoka katika lugha nyingine kunaruhusiwa ilimradi tu dhana lengwa iwe sahihi. Hata hicho kiingereza kinachoonekana kuwa ni lugha bora,mbona kina misamiati mingi inayotoka katika lugha zingine.?
KISWAHILI NDIO LUGHA TAMU NA ADHIMU DUNIANI KOTE.