Hiki ndicho kilichomkuta Dkt. Wilbroad Slaa

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
ESTA 1

Malkia Vashti aasi amri ya mfalme Ahasuero

1Mfalme Ahasuero, alipotawala ufalme wake ulikuwa mikoa 127, toka India hadi Kushi. 2Kiti chake cha enzi kilikuwa katika mji mkuu Susa. 3Mnamo mwaka wa tatu wa utawala wake, mfalme Ahasuero aliwaandalia karamu viongozi na watumishi wake wa serikali, wakuu wa majeshi ya Persia na Media, watu maarufu na wakuu wa mikoa. 4Basi, kwa muda wa miezi sita, Ahasuero akaonesha utajiri wa ufalme wake mtukufu, na fahari ya utawala wake.

5Muda huo ulipomalizika, mfalme aliwaandalia karamu watu wote wa mji mkuu wa Susa, wakubwa kwa wadogo. Karamu hiyo iliyochukua muda wa siku saba, ilifanyika uani, katika bustani ya ikulu. 6Mahali hapo palikuwa pamepambwa kwa mapazia ya pamba ya rangi nyeupe na vitambaa vya rangi ya buluu. Mapazia hayo yalikuwa yamefungiwa pete za fedha kwa kamba za kitani safi za zambarau, na kuninginizwa kwenye nguzo za marumaru.

Makochi ya dhahabu na fedha yalikuwa yamewekwa kwenye sakafu iliyotengenezwa kwa vijiwe vya rangi, marumaru, lulumizi na mawe ya thamani. 7Watu walipewa vinywaji katika vikombe mbalimbali vya dhahabu, naye mfalme alikuwa mkarimu sana wa divai ya kifalme. 8Kila mtu alikunywa akashiba; mfalme alikuwa ametoa maagizo kwa watumishi wa ikulu wamhudumie kila mtu kadiri ya mahitaji yake.

9Wakati huo huo, malkia Vashti naye aliwaandalia akina mama karamu ndani ya ikulu ya Ahasuero.

10Siku ya saba ya karamu hiyo, mfalme Ahasuero, akiwa amejaa furaha kutokana na divai aliyokuwa amekunywa, aliwaita matowashi saba waliomhudumia yeye binafsi: Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi. 11Aliwaamuru hao wamlete kwake malkia Vashti, akiwa amevaa taji yake ya kimalkia. Malkia huyo alikuwa na sura ya kuvutia sana, hivyo mfalme alitaka kuwaonesha wageni wake na viongozi uzuri wake. 12Lakini matowashi hao walipomweleza malkia amri ya mfalme, Vashti alikataa kutii. Jambo hilo lilimwudhi sana mfalme, akawa anawaka hasira moyoni.

13Ilikuwa desturi ya mfalme kupata mawaidha kutoka kwa wenye hekima, hivyo aliwaita wanasheria na mahakimu ili wamshauri la kufanya. 14Washauri wake wa kawaida walikuwa Karshena, Shethari, Admatha, Tarshishi, Maresi, Marsena na Memukani – viongozi saba wa Persia na Media waliokuwa na vyeo vya juu kabisa katika utawala wake. 15Aliwauliza hivi: “Je, kulingana na sheria, afanyiwe nini malkia Vashti? Maana, nimewatuma matowashi wangu kwake, lakini yeye amekataa kuitii amri yangu, mimi mfalme Ahasuero!”

16Hapo Memukani akamwambia mfalme na viongozi wake, “Licha ya kumkosea mfalme, malkia Vashti amewakosea viongozi na kila mtu katika mikoa ya mfalme Ahasuero! 17Tendo hili la malkia Vashti litajulikana na wanawake wote, nao watawadharau waume zao, wakisema: ‘Mfalme Ahasuero aliamuru malkia Vashti aje kwake, lakini yeye akakataa.’ 18Leo hii, mabibi wa Persia na Media ambao wamesikia alivyofanya malkia Vashti, watakuwa wanawaeleza viongozi wako; hivyo dharau na chuki vitajaa kila mahali. 19Basi, ukipenda, ewe mfalme, toa amri rasmi Vashti asije tena mbele yako.

Amri hiyo na iandikwe katika sheria za Persia na Media, ili isiweze kubadilishwa. Kisha, cheo chake cha umalkia, apewe mwanamke mwingine anayestahili zaidi yake. 20Amri hiyo itakapotangazwa katika eneo lote la utawala wako, kila mwanamke atamheshimu mume wake, awe tajiri au maskini.”

21Wazo hilo lilimpendeza sana mfalme na viongozi wake, akatekeleza kama alivyopendekeza Memukani. 22Basi, akapeleka barua kwa kila mkoa kwa lugha na maandishi yanayoeleweka mkoani: Kwamba kila mwanamume awe bwana wa nyumba yake, na kuitangaza habari hii kwa lugha yake.

Swali:
Hivi TEC haiwezi kumpigania Dr. Slaa Holy See ili apewe hadhi ya Balozi wa Vatican asiye na kituo cha kazi ili akamalizie muda wake anapojiandaa kuanza maisha mapya ya Uburuda kwa mujibu wa umri wake.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Huyo huyo aliyeasi upadre na kuoa au unataka afanye mara ya pili Uasi kama Malkia Vashti?

Amekataliwa Duniani na mbinguni,mwambieni Babu yenu atulie amalizie uzee wake.
Katoliki haiko hivyo kama Lutheran na Suni na Shia na Ibadi.

Katoliki Papa anamrejeshea Upadri wake wakati wowote akiwa tayari na kutekelezewa hatua za kinidhamu zinazomtengenezea toba na MUNGU.

Wakatoliki wanaamini upako wa mafuta ya huduma ya Upadre Papa hana mamlaka ya kuufuta kwa sababu ni nadhiri ya milele.

Ndiyo maana Padre akifanya kosa anaweza hata kufungwa na akimaliza kutumikia adhabu akitaka anarejeshewa Upadri wake hadi mauti. (Nadhiri za milele)

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Katoliki haiko hivyo kama Lutheran na Suni na Shia na Ibadi.

Katoliki Papa anamrejeshea Upadri wake wakati wowote akiwa tayari na kutekelezewa hatua za kinidhamu zinazomtengenezea toba na MUNGU.

Wakatoliki wanaamini upako wa mafuta ya huduma ya Upadre Papa hana mamlaka ya kuufuta kwa sababu ni nadhiri ya milele.

Ndiyo maana Padre akifanya kosa anaweza hata kufungwa na akimaliza kutumikia adhabu akitaka anarejeshewa Upadri wake hadi mauti. (Nadhiri za milele)

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Nyie mnaokataa kuzika watu 🤣🤣

Sasa mtu ni Babu hata akiwa padre atafanya lipi jipya keshachoka?

Wapi Mushumbishi kutetea mume wake? 🤣🤣🤣🤣
 
Labda Nchi ya Vatican maana Kwa kuvuliwa Ubalozi hakuna mafao na stahiki tena za Balozi mstaafu
Akija rais mwingine atamrudishia hadhi ya ubalozi, hivyo ndivyo Tz inavyofanya kazi. Nadhani hadhi ya ubalozi ilindwe kisheria kama ya Majaji kwamba ukiishamteua basi huwezi kumuondolea hadhi hiyo ili kulinda heshima ya nchi isitwezwe kimataifa.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Nyie mnaokataa kuzika watu

Sasa mtu ni Babu hata akiwa padre atafanya lipi jipya keshachoka?

Wapi Mushumbishi kutetea mume wake?
Nadhani unahitaji kujuwa mfumo wa Ukatoliki vizuri.

Mushumbuzi ilikuwa ndoa ya kimkataba kwa matakwa ya Katiba ya JMT kwamba rais lazima awe na mwenza. Ndiyo maana alipokosa urais akaachana na Mushumbuzi na Mushumbuzi wala hakwenda kudai haki zake Mahakamani za kuachwa kama mke.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Wapi Mushumbishi kutetea mume wake? 😂😂😂😂

Jamaa anakataliwa kuanzia kwenye familia Hadi Vatican,laana inamtafuna 🤣🤣🤣🤣
Wenzako wamevurugwa hapo Lumumba 😂😂🐼

Katibu mkuu mstaafu wa TEC ni zaidi ya Vyama Vyote vya Siasa ukiviweka pamoja 😂

Three The Hardway Dr Slaa, Mwabukusi na Mdude 🔥🌟🔥

Mbeya Moja hiyooooo!
 
Back
Top Bottom