Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 60
- 1,237
Jana wakati wa ibada ya kumuingiza kazini Askofu Malasusa nilishangaa kuona tena Rais Samia akiingia na jukwaa lake la kimamlaka pamoja na kiti chake cha kimamlaka licha ya kwamba tulishawahi kuonya huko nyuma kuwa ni makosa. Kanisani au msikiti ni sehemu za ibada takatifu na wala hatupaswi kuingia na vyeo hata kama tumealikwa maana pale mkuu ni mmoja tu Mungu Mwenyezi.
Kwa bahati mbaya sasa madhabahu ya kanisa yamegeuzwa majukwaa ya kimamlaka ya serikali kiasi kwamba Rais anafika hapo na kutoa tamko au amri za kiserikali kinyume kabisa na kanuni za kikristo.
Mfalme Suleiman pamoja na kwamba yeye ndiye aliyejenga hekalu la Mungu pale Jerusalem lakini hakuwahi kuingia na ufalme wake hekaluni. Mfalme Suleiman aliingia hekaluni na kusali kama muumini wa kawaida.
Mwaka 734 - KK mfalme Uzia alipigwa ukoma na Mungu baada ya kulazimisha kupanda madhabahuni wakati anajua hakuwa na hiyo mamlaka ya kimungu isipokuwa wana wa haruni na walawi wengine. Pamoja na kwamba mfalme Uzia alionywa kwamba alikuwa anafanya makosa alipuuza maonyo hayo kisha kupanda madhabahuni. Mfalme Uzia alipigwa ukoma mpaka kifo chake huku akikaa peke yake katika nyumba ya kutengwa kama ilivyokuwa desturi zamani za kale mtu mwenye ukoma kutengwa.
Leo baada ya miaka 2700+ kupita baada ya tukio la mfalme Uzia tunaona Rais Samia anaingia kanisani na mamlaka yake ya kiserikali hata mbele ya madhabahu. Kwani kulikuwa na ubaya gani Rais angeingia kama muumini mwingine akakalia viti kama waalikwa wengine?
Kuingia na jukwaa la kimamlaka maana yake unaingia na mamlaka yako kanisani kitu ambacho ni kosa kubwa sana kwani kanisani pana mamlaka zake za kimungu. Tulijaribu kuonya Rais alipoingia na kiti cha kimamlaka katika kanisa la Roma mwaka jana lakini tunaona jambo hili linajirudia. Najua mliomwalika hamuwezi kukemea au kukataza jambo hili kwa sababu labda mnamuogopa au anatoa michango mingi kwenu au anawapa misamaha ya kodi lakini sisi wengine tutakemea maana Yesu Kristo alitusisitiza kuhubiri kweli.
Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.