Hiki ndicho cheti changu cha form four

Ndo unaturingishia wenye div 4 zetu za 33 eeee!!??[emoji53][emoji53][emoji53]
 
Kusoma ni kipaji, si kila mtu lazima apate division one. Kuna professor nilitaka niupate wasifu wake Wikipedia sijaupata(hawamtanbui) Ila Lulu yupo Wikipedia.
Halafu wewe ulikuwa ukisoma kwa kushindana na si kwa malengo, badala yake mwanasiasa Msukuma STD seven anakupangia kiasi cha mafao yako mara ukistaafu huku yeye within 5 yrs ya ubunge wake anaondoka na more than 200 TZS.
 
Kwenye huu uzi kila mtu aliyefeli shule anadai maisha ya mtaani kayapatia........huku ukute akitafuta hela kwa bidii akalipe ada ya mwezi ujao, mtoto wake nae akapate cheti kama hiko, sa ujiulizi kwa nini asimpe tu mbinu huyo mwanae za kuyapatia maisha ya mtaani......... Wabongo kwa unafiki siwawezi .......bora hata Mimi vyeti vya lasaba havina maksi maana ningeumbuka
 
Mkeka huo ndio unaonesha ulichagua masomo ya sayansi, tofauti na unavyotuaminisha

By the way hongera (Kama cheti ni genuine na ni chako)

Uko wapi siku hizi mkuu
 
Hongera sana Mkuu,kuna vilaza humu vinarusha madongo,ukiona Mtu anadharau Elimu anailinganisha na magari anayomiliki,jiongeze kichwani na usimjibu kabisa.
 
Siamini sana matokeo ya darasani, maana ya kuona jamaa ana kama hizo shoga maarufu sana
 
Kusoma na kufaulu ni jambo moja, kutusua kwenye maisha ni jambo jengine kabisaaaa
 

Naomba nikuhakikishie kuwa hapa asilimia 90 ya maisha yako tayari umeshayanyoosha, ila tu kama utamalizia vizuri asilimia 10 iliyobaki! Hongera sana
 

Naiona One ya pointi 8 hapo mkuu ulitisha sana. Vilaza wengine unaweza kuta hata one point 8 hapo inakokotolewa vipi hawajui🤣
 
Cha form six na chuo kiko wapi??
 
Mkuu tumia akili yako uliyo barikiwa kujifunza Maarifa mpya kila uchao ....kwa kuanza piga msuli wa forex hakika ukiielewa akili yako itakufanya uwe billionaire!
 
Mkuu tumia akili yako uliyo barikiwa kujifunza Maarifa mpya kila uchao ....kwa kuanza piga msuli wa forex hakika ukiielewa akili yako itakufanya uwe billionaire!
Siku zote napenda kujaribu vitu vipya. Maisha ni kujifunza kila siku
 
Mkeka huo ndio unaonesha ulichagua masomo ya sayansi, tofauti na unavyotuaminisha

By the way hongera (Kama cheti ni genuine na ni chako)

Uko wapi siku hizi mkuu
Nimeajiri lakini pia najiendeleza kielemu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…