Hiki kimsemo cha kumuita kila mtu 'kaka' kinaboa

Hiki kimsemo cha kumuita kila mtu 'kaka' kinaboa

Pole sana babuu...unajua nibi babu wewe haeajua nini babu..istoshe hawajui kua wewe ni babu
 
Hahahah,nilimtokea mdada fulani mlokole kesho yake anaanza kuniita "kaka" daah nilichukia sana
Mkuu labda hujawafahamu hawa akina dada, kuitwa kaka kusikukatishe tamaa! siku hizi ni code yao hiyo,mi kuna sehemu naitwa kaka halafu kama kawaida.
 
Mimi hata konda namuita kaka. Nikipanda tu daladala wakati wa kushuka, nasema "kaka naomba unishushe palee"

haya babu tumekusikia au na babu inakuboa??
 
Nilidhani ninaekeleka ni mimi tu,kumbe tupo wengi…
Unakuta jitu zima linakuzidi umri afu linakuita kaka daaah
 
JF,

Kuna misemo tofauti tofauti imekua ikiibuka katika baadhi ya vipindi.

Kimsemo kimoja wapo ni hii cha "kaka" ujue sijui ni kutokana na kuzoea kiswanglishi au vipi?.

Bora mtu aniite blaza kuliko aseme kaka sijui najisikiaje afu bora angalau awe mdogo au mwanamke angalau sioni shida.

Sasa mtu ni age-mate au amekuzidi anakupigia sim au mnaonge anasema "habari kaka" yaani katika kila kitu kaka
Aah! naboreka na nibora aseme kaka flani labda.

Sasa kaka kaka kaka wakati kaka zenyewe hawamaanishi wanaongea kama kimsemo au kafasheni "

INANIBOA

SIJUI WADAU WENGINE MNAONAJE
Mtu kukuita kaka haina maana eti umemzidi umri laa hasha bali ni sawa na kusema ndugu kwakingereza ni sawa na brother
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Bora tu uendelee kuitwa kaka
Nairobi jamaa tena mtu mzma
Kabsa anakusalimia kwa
Kukuambia mambo
Na hapo n

Wanaume kwa wanaume mnasalimiana
Mambo[emoji2] [emoji2]
Ha ha ha
 
Kama halikubadilishi jinsia uliyo nayo sidhani kama linakuwa na ubaya.

Kubali tu kaka hakuna jinsi au uwe unawaambia jina ambalo unalipenda na unaona wakikuita nafsi yako itaburudika.
At leat uitwe jina lako
 
Tena shukuru sana weye huko mombasa wenyewe hutamka mambasa vidume husalimiana mambo shoga angu ndo utajua kaka ni heshima kubwa na kujali we huoni hata mabibi ukiwaamkia wanakujibu marahaba baba hata kama hakujui nayo ni dharau?
Duuuh
 
Hakuna jambo huwa silipendi Mwanaume mwenzangu anisalimie mambo na pia sijawahi kumsalimia MTU wa jinsia yangu "eti mambo!"...

Huwa naona salamu ya mambo ni kama ya kina Dada tu.
Akisema " mambo!? Na akisema " mambo VIP"!?
Ya kike n ipi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom