Hii ya Tabora imenishangaza sana

Hii ya Tabora imenishangaza sana

tamimusalim

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2014
Posts
1,822
Reaction score
501
Nimeshangazwa na umati mkubwa wa raiya pamoja na wanajeshi wa jeshi la jwtz kukusanyika kwa wingi kushuhudia tukio ambalo ukweli linasikitisha ,tukio lenyewe ni bank ya exim walikuwa wanatoa msaada wa kitanda tena kimoja cha kujifungulia wajawazito, kilichonishangaza umati kama ule kushuhudia msaada wa kitanda tena kimoja kweli hari hii inasikitisha sana, tena hata star tv wamelitoa hilo tukio katika taarifa ya habari saa mbili usiku, naiyomba tuu bank hii vitu vidogo vidogo kama vile muwe mnavitoa tu kimya kimya sio lazima mpaka jeshi na saluti juu, mnadhalilisha watu
 
Sasa wanaonyesha shukrani mkuu acha kujilinganisha.aisee
 
Hii taarifa yako nimejikuta najishangaa kwanini nami nimeshangaa kitanda kimoja tu kimewakusanya umati mkubwa hivyo (kwa mujibu wa maelezo yako).

Ila nimepata jibu "na wao hao JWTZ na raia wanaishangaa Exim Bank kutoa "kakitanda kamoja tu".
 
Hiyo stanbic si ndio watu walichota pesa kwa maroba?wanachoshindwa kununua hata vitanda elfu moja ni nini?
 
Hii taarifa yako nimejikuta najishangaa kwanini nami nimeshangaa kitanda kimoja tu kimewakusanya umati mkubwa hivyo (kwa mujibu wa maelezo yako).

Ila nimepata jibu "na wao hao JWTZ na raia wanaishangaa Exim Bank kutoa "kakitanda kamoja tu".
nina rafiki yangu mkenya niko nae hapa kwangu amenitembelea ameshangaa sana tanzania kitanda kimoja umati kama anakuja rais najeshi juu jamani,na saruti nyingi tuuu
 
nina rafiki yangu mkenya niko nae hapa kwangu amenitembelea ameshangaa sana tanzania kitanda kimoja umati kama anakuja rais najeshi juu jamani,na saruti nyingi tuuu

Mkuu, sijakusudia kucheka!

Kwamba tu maskini kufikia kiwango hicho?Kitanda kimoja kikusanye umati wa watu tena kiitifaki kabisa...? Msimuliaji wako pengine ametia chumvi katika habari yake.
 
Mkuu, sijakusudia kucheka!

Kwamba tu maskini kufikia kiwango hicho?Kitanda kimoja kikusanye umati wa watu tena kiitifaki kabisa...? Msimuliaji wako pengine ametia chumvi katika habari yake.
Yaani itifaki full, yaani hawa wahindi wametuzarau sana sio chumvi kwani taarifa ya habari saa mbili ulitazama kituo gani ungetazama star Tv ungeona mambo,kitanda tena kimojaaaa
 
Yaani itifaki full, yaani hawa wahindi wametuzarau sana sio chumvi kwani taarifa ya habari saa mbili ulitazama kituo gani ungetazama star Tv ungeona mambo,kitanda tena kimojaaaa

Mbavu zangu, hujazitendea haki!
 
Mkuu, sijakusudia kucheka!

Kwamba tu maskini kufikia kiwango hicho?Kitanda kimoja kikusanye umati wa watu tena kiitifaki kabisa...? Msimuliaji wako pengine ametia chumvi katika habari yake.

Zawadi haina ukubwa jamani. Shukuruni kwanza, bank imefanya hivyo kama njia ya kukufungulieni mengi makubwa baadaye.
Mbona Mh. James Ruge hakukumbuka hata wale wazee wasio na pa kulala akawapa nao ka 80 m? Kutoa ni moyo si utajiri. Wacha wapigiwe masaluti ni haki yao.
Aksante sana sana Exim bank kwa moyo wa kutoa. Mkiokota tena kingine huko kwenu wawekezwaji mtuletee hata kama akijifungulia mama mmoja kikavunjika. Yote ni misaada tu.
 
Nilipokuwa nafanya kazi katika moja ya wilaya za mkoa wa Mtwara nilishuhudia NMB wakitutia hasara kwa kutufadhili vyandarua sitini lakini sisi tuliandaa shughuli ya mapokezi kwa zaidi dhamani ya msaada huo.
Kilichofanyika ni kwamba mwakilishi wa NMB makao makuu Bi Shayrose Banji alitufanya tuamini kwamba msaada ule ulikuwa ni mwanzo tu kwani kungekuwa na misaada zaidi.Lakini hakuna misaada zaidi tuliipata baada ya hapo.
Kwa hiyo tuliandaa vikundi vya ngoma kwa ajili ya kutumbuiza kwenye shughuli hiyo.Nilipopiga hesabu nikagundua kuwa pesa tuliyotumia ingeweza kununua vyandarua zaidi ya vile tulivyopewa ambavyo vilikuwa kama vya thamani ya laki tatu wakati huo.
 
watz hamkosagi la kusema. msiposhukuru kwa kidogo hata kikubwa hamtokipata! unashangaa kitanda kimoja wewe umewahi kupeleka nini?
 
Zawadi haina ukubwa jamani. Shukuruni kwanza, bank imefanya hivyo kama njia ya kukufungulieni mengi makubwa baadaye.
Mbona Mh. James Ruge hakukumbuka hata wale wazee wasio na pa kulala akawapa nao ka 80 m? Kutoa ni moyo si utajiri. Wacha wapigiwe masaluti ni haki yao.
Aksante sana sana Exim bank kwa moyo wa kutoa. Mkiokota tena kingine huko kwenu wawekezwaji mtuletee hata kama akijifungulia mama mmoja kikavunjika. Yote ni misaada tu.

Nimekusoma vizuri. Kweli zawadi ni zawadi.

Hata hivyo kuna zawadi nyingine unapopewa lazima ujipime. Exim Bank, wanatoa kitanda kimoja?
 
Back
Top Bottom