Hii ya Police Traffic Arusha imakaaje?

Hii ya Police Traffic Arusha imakaaje?

MikeGolles

Member
Joined
Mar 31, 2012
Posts
73
Reaction score
9
Wadau naombeni msaada! Hii ya traffic police inanipa shida kidogo kuielewa! Nimekwenda kulipa sumatra ukaguzi wa gari unafanyika kwa elfu 10, na ukienda kwa ajili ya loss report charge yake ni elfu 5, ambazo kwa taratibu za police hasa Arusha zinatakiwa zilipwe kwa mhasibu wa police!

Taratibu mpya ni kwamba utakwenda kwa mhasibu atakupa bank sleep ambazo utakwenda kulipa NMB !

Majuzi nimekwenda kukaguliwa gari police kwa ajili ya kupata sumatra lakini taratibu nilizopitia nikama nilivyoeleza! Unapitia traffic then wanakuelekeza kwa mhasibu then NMB halafu unarudi kwa mhasibu unampa bank slip na yeye anakupa stakabadhi ya serikal ambayo utakwenda nayo kwa vehicle inspector atakagua gari husika na atakujazia form ambayo utaipeleka ofisi za sumatra!

Traffic Arusha wanasimama barabarani kwa kundi hadi la police 20 na wanatoza penalt magari hadi zaidi ya makosa matatu kwa gari moja, ambayo kwa mujibu wa sheria ni itakuwa ni 90,000 na kuendelea!

Tatizo langu lipo hapa , kama watahitaji loss report ya tsh 500 ilipwe bank! na bank slip ipelekwe kwa mhasibu ili upewe stakabadhi ya serikali! inakuwaje hizi nyingi zilipwe barabarani bila mhasibu but just police form as they call it notification? Je hivi ndivyo pesa za serikali zinakusanywa!

Traffic act zinatungwa na bunge na motor vehicle lisence haiko kwenye trafik act kama ikiisha muda wake, sababu TRA watakuadhibu wenyewe cha ajabu traffic Arusha wakucharge penalt ya motor vehicle! Je sheria za nchi hii zinaruhusu mtu aadhibiwe mara 2?

Wadau nisaidieni kama sheria za nchi hii zinaruhusu uadhibiwe na police na pia Sumatra ?

Naombeni mnijibu wakuu!
 
Sijali kama nikilipa penalt na kiadhibiwa kwa mujibu wa sheria lakini mimi sio mkwepa kodi na ninalipa kila kodi on time lakini hii imetokea maana nilificha document ambazo ninajua police hawzihitaji na haziwahusu!
 
Sasa matatizo yako ya maisha unatuletea hapa ya nini?
Chriss angalia mada za kuchangia kishabiki na mada za kuchangia kiungwana. Huu ni ufafanuzi wa hali halisi huko barabarani na wala hauna uhusiano wowote na ushabiki unaotaka kuuleta hapa, ama mwenzetu huishi hapa nchini nini? Jiheshimu tu ili heshima yako ipande.
 
Tindo usimshangae Lukosi yeye haishi hapa nchini yuko Uingereza ni kuli wa kubeba maboksi kwenye maduka!so haelewi chochote!
 
na we nani kakulazimisha kuchangia ka huna cha maana kaa kimya si lazima kila uzi uongee
 
Ndugu bottom line nu kwamba malipo yeyote lazima upewe stakabadhi or cash receipt na kwa serikali ni ile nyembamba ya rangi nyekundu hivi. sijui wanaita exchequer receipt. so notification sio stakabadhi. ukiandikiwa ile anatakiwa akupe risiti kama utatoa hela pale. otherwise unaibiwa.
 
Hizo police notification books zipo kibao zinatengenezwa mjini kwa mshkaji, ila traffic ameamriwa na bosi wake kukamata angalau makosa matatu, yaani sikuhizi wanakamata mpaka wakwe zao
 
notification inakuwa ktk karatas ya njano kama unapewa nyekundu hizo sio ndugu yangu
 
Sasa matatizo yako ya maisha unatuletea hapa ya nini?

mkuu siasa zisikuaribie akili zako,we ni kichwa sana kwa namna nilivyopata taarifa zako ila akili zako huzitumii ni kwasabab tu ya siasa,shabikia siasa lakin akili ndo iipeleke siasa..,Achana na ushabiki wa kisiasa,mkuu plz achana na ushabiki wa kisiasa.!! iruhusu akili yako ifanye kazi.,utadharauliwa na jamii bure.,like u bro.!!!!
 
Mpuuzeni huyu chris mkosi.
katika vitu ambavyo siwaelewi police ni pamoja na hiyo ya kulipia bank.nafikiri ni uvivu na rushwa ndo vinafanya waone losereport ni usumbufu kwao.kama vipi hata kulipia faini hela iende bank.
 
Sasa matatizo yako ya maisha unatuletea hapa ya nini?
Umemuelewa lakini?
Jamaa ameuliza ktu ambacho nami niliwahi kuwapa somo Traffic wa Kia nashukuru walinielewa.. Adhabu ya kutolipa Kodi ya matumizi ya Barabara ni Fine inayotozwa moja kwa moja pale unapoenda kulipia Road Licence TRA. Chaajabu Traffic akikukamata wakati anasimamia Traffic Act anakuadhibu kwa kosa hili ambalo kimsingi halipo kwenye Traffic Act, lakini pia adhabu yako ipo pale tu utapoenda kulipia. Hili ni tatizo kwa watanzania wote na ninaamini ni kutokana na kukosa Elimu.
Lakini kwa jibu lako wewe sio kukosa Elimu bali ni kutokana na Ujuha ulionao. hata ungepata Elimu isingekusaidia. Bora CDM walikutimua mana ni fedheha kua na mwanachama mwenye akili kama wewe..
 
Ndugu bottom line nu kwamba malipo yeyote lazima upewe stakabadhi or cash receipt na kwa serikali ni ile nyembamba ya rangi nyekundu hivi. sijui wanaita exchequer receipt. so notification sio stakabadhi. ukiandikiwa ile anatakiwa akupe risiti kama utatoa hela pale. otherwise unaibiwa.
Ndugu yangu kama una muda mzuri fanya kama mimi, kusanya hizo notification, hakikisha unayempa pesa au fine whatever you call it, ameweka sahihi na majina yake yote. Mpe mda wa kula hizo pesa hata wiki mbili au tatu kisha uende kituoni kwake ukaonane na mhasibu ili kudai risiti yako ambayo ni halali yako. Kitakachotokea ni mhasibu kumpigia simu polisi aiyekukamata kwamba aiwakilishe pesa ili upewe risiti yako, cheki atakavyokubembeleza sasa myamalize maana hatakua nahiyo pesa
 
Umemuelewa lakini?
Jamaa ameuliza ktu ambacho nami niliwahi kuwapa somo Traffic wa Kia nashukuru walinielewa.. Adhabu ya kutolipa Kodi ya matumizi ya Barabara ni Fine inayotozwa moja kwa moja pale unapoenda kulipia Road Licence TRA. Chaajabu Traffic akikukamata wakati anasimamia Traffic Act anakuadhibu kwa kosa hili ambalo kimsingi halipo kwenye Traffic Act, lakini pia adhabu yako ipo pale tu utapoenda kulipia. Hili ni tatizo kwa watanzania wote na ninaamini ni kutokana na kukosa Elimu.
Lakini kwa jibu lako wewe sio kukosa Elimu bali ni kutokana na Ujuha ulionao. hata ungepata Elimu isingekusaidia. Bora CDM walikutimua mana ni fedheha kua na mwanachama mwenye akili kama wewe..
Mimi nilikuwa traffic for five yrs na hilo ni moja ya makosa ambayo nilikuwa nayakamata sana
 
Sasa matatizo yako ya maisha unatuletea hapa ya nini?

M p u m b a vu mjinga wa mwisho wewe, beba boksi zako osha ma ta ko ya wazungu huko huko. Hujui kilichoulizwa wala hutakaa ujue. Ktk hili kaa pembeni kabisaaaa. Hujui chochote hapa duniani wala hutakaa ujue lolote hapa duniani.
 
Back
Top Bottom