Mantiki inakataa kabisa.
Hivi katibu wa Mbunge (let say it is true ni katibu wake, am not sure, sijasoma habari) ana uhusiano gani na Mbunge ktk mambo binafsi? Je, Katibu wa Mbunge aktoka ofisini ni jukumu Mbunge kujua kama anafanya nini? Wapi? na Nani?. Jina la Lema hapo linaingiaje?. Hivi kesho akimpiga mke wake, akiiba tunamhusisha mwajiri wake Lema tena?
Pili, Ninasikitika kwamba habari hizo zimeandikwa ktk gazeti ambalo si la udaku. Je, Mjomba, shangazi, marafiki zake, majirani, nk mmoja wao akiiba, kichwa cha habari lazima kianze na jina Lema?
Tatu, kwanini habari hizi zianze kwa kasi tangu yeye aliposoma maoni ya upinzani yaliyoichafua sana Serikali ya CCM hasa jeshi la polisi kwa kuua raia bila sababu huku wakishindwa kukanusha hoja ya Lema? Kwanini leo?
Kila ninapowaza mantiki inakataa kabisa. Iko siasa ya hatari ya ccm nyuma jambo hili ambayo inaweza kuvuruga amani yetu. Sitashangaa kesho wakisema Dr Slaa, Mbowe, Mnyika Wenje nk ana hili na lile.