Hii ya jeshi kuomba billion sabini kuanzisha benki imekaaje?

Mifano mingi je kuna biashara gani jeshi inafanya kwa faida ya kupewa bank!!. Kama ni kwa wanajeshi basi wande bank za kawaida kuna tatizo gani? Tanzania ni nchi masikini sasa badala ya kuachia mashirika binafsi yafanye kazi tunataka wananchi wachukue pesa za kuanzisha bank za kifisadi za jeshi!. Jeshi la Tanzania linafanya nini kwanza kwa taifa zaidi ya kutumia pesa tu!!!
 
Jeshi la nchi masikini badala kufikiria vitu vya kuzalisha wanafikilia kufanya biashara ya huduma utafikiri ni nchi iliyoendelea. Nchi hii inahitaji manufacturing ili kuinuka toka uchumi mdogo kwenda uchumi wa kati.

Kamwe hatutakaa tutoke kwenye huu umasikini kama tunawaza kufungua benki wakati hakuna tunachozalisha.

Uyoga wabenki uliopo hapa nchini si kwa ajili ya watanzania bali umewafata wawekezaji kutoka nchini kwao. Hatutafika popote kwa uchumi wa uyoga wa mabenki!

Jeshi la weza kuwa na miradi yake lakini siyo bank!
 
Hii ya jeshi kuomba billioni sabini kuanzisha benki iko vipi hii? leo wameomba hizzo billioni sabini kesho hawatotuomba uhuru wetu kweli?
<br />
<br />
Nakubaliana nawe mkuu, Jeshi letu linatakiwa kugharamiwa na kodi zetu na jukumu lao ni Ulinzi wa Wananchi, na uokozi yanapotakiwa kufany hivyo. Kitendo cha kuwa na Benki yao, kitawafanya washindane na raia kufanya biashara, na kwa kuwa wana nguvu ya ziada, uwezekano wa kuwaonea raia wanaopaswa kuwalinda. Sio wazo zuri kabisa, wanaweza kufanya biashara kama vikosi maalum vya kuzalisha mali tu.
 
Mbona inasemekana mwenzao Shimbo anazo zaidi ya hizo? Siawachangie tu waanzishe watakacho?
 
UKiona Jeshi linaanza kuwa kikundi cha kusaidiana katika shida na furaha na majambazi yanarindima mitaani ujue kuna shida na angalia mshale wako wa saa
 
Mbonaq viongozi wao akina Shimbo , Mboma ni matajiri acha nao wafuate huko huko ila najua hii ni njia ya kuwazima wadogo wasiwe na plan B kwenye maamuzi fulani .
 
Hii habari ni ya zamani sana wakati jeshi linaadhimiasha miaka ya kuzaliwa kwake. Mwmunyange alipropose mpango wa kuanzisha JESHI SACCOS ili kusaidia wanajeshi kupata sehemu ya kuomba mikopo bila bureaucracy. Sidhani kama ina tatizo lolote.

Mkuu usihangaike na hawa wadandiaji wa hoja wasiojua wanachoongea. Hivi kuna shida gani kwa wanajeshi kutafuta njia za kuinua vipato vyao kihalali? Mnataka waibe risasi na mabomu wakauze ili waendeshe maisha yao na familia zao?
 
Mimi binafsi napinga jeshi kuwa wajasiliamali kazi yao ni kulinda raia na mipaka ya nchi watahudumiwa kwa kodi zetu, watakaa kambini na jeshi lazima liwe la mkataba iwe ni sehemu ya kujitolea wananchi kulinda nchi yao wenyewe wakimaliza jeshi wapewe mafao manono yatakayowasaidia kufanya ujasiliamali na kujenga nyumba kwa ajili ya familia zao, Isichukuliwe kama ajira bali wito wa kizalendo wa kulinda na kutetea taifa.
 
UKiona Jeshi linaanza kuwa kikundi cha kusaidiana katika shida na furaha na majambazi yanarindima mitaani ujue kuna shida na angalia mshale wako wa saa
Kweli mkuu hilo ni tatizo inabidi tuliangalie. mwanajeshi akili yake lazima ielekezwe kwenye ulinzi ni wajibu wetu kuliangalia jeshi letu na ni lazima wajue jeshi sio chombo cha kutajirikia bali ni chombo cha kujitolea kwaajili ya ulinzi wa taifa, Jeshi sio ajira ni wito, jeshi lisiwe la starehe sana au la shida sana.
 
ninadhani ni sahihi sana kupatiwa mtaji wa kundesha benki itakayokuwa na maslahi kwa wanajeshi wote na sio wachache
 
Kweli mkuu hilo ni tatizo inabidi tuliangalie. mwanajeshi akili yake lazima ielekezwe kwenye ulinzi ni wajibu wetu kuliangalia jeshi letu na ni lazima wajue jeshi sio chombo cha kutajirikia bali ni chombo cha kujitolea kwaajili ya ulinzi wa taifa, Jeshi sio ajira ni wito, jeshi lisiwe la starehe sana au la shida sana.

Unataka wewe pekee ndiyo uishi na wale wananjeshi na familia zao wawe wasindikizaji. Wito sawa, wanaishije? Wanasomeshaje? Wanasaidiaje wanaowategemea?
 
mkuu wewe unaishi dunia gani? Jeshi ni ajira kama zilivyo ajira zingine. wanategemewa na ndugu kibao kwa ajili ya kuendeleza the so called extended family. wake up woman/man

Aliyeshiba hajui mwenye njaa!
 
Haiwezekani mimi nimepata kazi tuu, nilishe hadi watoto wa mjomba hapa ndipo ufisadi unapoanzia kila mtu ajitegemee kama katiba ya jamhuri ya muungano inavyosema, jeshi liwe la mkataba miaka mitano mitano, wachache sana wenye taaluma zao ndio wabaki, baada ya hapo wakafanye kazi nyingine.
 
benki itakayoanzishwa inalenga zaidi kumsaidia mwanajeshi na si jeshi kama jeshi..., kwa mfano.., mwanajeshi ana familia, anapenda watoto waende shule nzuri, ajenge, aanzishe biashara, basi anaomba mkopo ambao utakua na masharti nafuu.......

Kwa idadi ya wanajeshi nchini..., nusu yao tu wakiwa wateja wa benki hii..., benki itajiendesha kwa faida at the same time itatimiza lengo la kuwasaidia walengwa

hakuna lolote hapo. Dawa ni kuboresha mishahara kama kweli pesa ipo........ Wasitudanganye wanataka sehemu ya kuchota pesa ya uchaguzi 2015 hao. kama ni hivyo basi serikali pia itoe Billion 70 kwa ajili ya benk ya waalimu, Billion 70 kwa manesi, Billion 70 kwa madereva, Billion 70 kwa akina mama ntilie ....... ili wote tuwe na benki za kutuwezesha kusomesha watoto wetu!!!
 
Mkuu umesema jambo la msingi sana!

UKiona Jeshi linaanza kuwa kikundi cha kusaidiana katika shida na furaha na majambazi yanarindima mitaani ujue kuna shida na angalia mshale wako wa saa
<br />
<br />
 
Mimi sioni kama ni kitu kibaya kwa wajeshi wetu kutafuta njia ya kujiongezea kipato kama raia wengine wowote wa Taifa hili la Tanzania kwani ni haki ya msingi kabisa ya raia,lakini mashaka yangu yapo hapo katika hilo la kuanzisha benki,kwa mtazamo wangu nadhani hilo halipaswi kuwa la kwanza kwani jeshi letu hivi sasa limejaza vijana wasomi wa taaluma mbali mbali nadhani wangefanya mpango wa kuanza na manufacturing industries then wanaweza kuwa na benki.Lakini swala la kuwa na benki ambayo mzunguko wake wa pesa utategemea pato lile lile la serikali kutoka kwa wananchi wake nadhani hapo watakuwa si tu kwamba hawaisaidii Tanzania yao bali hata wao wenyewe watakuwa wapo katika biashara ya upatu tu,kwani kiasi hicho hicho walichoomba kama mtaji wa benki ndicho kitakachokuwa kinazunguka ndani ya jeshi kwa faida hafifu itakayokuwa inatokana na riba kwa wakopaji.
 
Haifai jeshi kujiingiza kufanya shughuli za ujasiliamali, shughuli pekee ambayo jeshi inaweza kufanya ni viwanda kwaajili ya jeshi lenyewe kwa mfano wanaweza kuanzisha kiwanda cha kutengeneza sare za jeshi, mabuti na vitu vingine muhimu kwa jeshi, Wnaweza kuwa na mashamba yao na lunch zao za mifugo hiyo iko ok! hata hivyo bidhaa wanazopata kutoka madukani kwao ni bei rahisi kwa mfano mabati, cement na nk, Wakijiingiza kwenye biashara ndogondo, wakishaanzisha vikundi vya kusaidiana katika shida na raha hilo ni tatizo, mwanajeshi lazima akabiliane na fatique ni lazima akili yake yote iwe kwenye ulinzi , lazima jeshi liwe la watu waliojitolea na waliosukumwa na uzalendo kwenda jeshini sio kufuata pesa hapo ndipo tutakapo kuwa na jeshi imara, mwanajeshi anayepigana kwa pesa hawezi kupigana kwa moyo wake wote.
 
Back
Top Bottom