Hii ya jeshi kuomba billion sabini kuanzisha benki imekaaje?

Ni sahihi sana, Jeshi la Ujerumani linamiliki night clubs, Jeshi la Croatia linasifika kwa kutengeneza juice ya passion, Jeshi la Canada limepata umaarufu mkubwa sana kwa kutengeneza vitafunio na tambi za paketi. Sioni tatizo kwa jeshi letu kufanya ujasiriamali, muhimu ni kuangalia kusiwe na mgongano wa kimaslahi na usalama wa wananchi.
Zamani tulikuwa na jeshi letu la kujenga Taifa ambalo lilisifika saana kwa kulima mahindi kwa wingi, sikuhizi jeshi letu linasifika kwa kupiga raia wasokuwa hatia.
 
Wakati wa kuanzisha Hospitali kubwa ya Jeshi kuna mijitu ilikuja na mawazo kama hayahaya ohoo kuna haja gani ya Jeshi kuwa na Hospitali wakati Muhimbili ipo,kuna haja gani ya Wanajeshi kuwa Madakitari leo hii ndo wa kwanza kwenda kutibiwa jeshini
 
Wakati wa kuanzisha Hospitali kubwa ya Jeshi kuna mijitu ilikuja na mawazo kama hayahaya ohoo kuna haja gani ya Jeshi kuwa na Hospitali wakati Muhimbili ipo,kuna haja gani ya Wanajeshi kuwa Madakitari leo hii ndo wa kwanza kwenda kutibiwa jeshini
Acha hizzo wewe hospitali ni ya muhimu kuliko hiyo benki italeta mgongano wa kimaslahi na raia, Hivi wewe unajua habari ya meremeta walikabidhiwa wakina nani? si jeshi walikuwa na mgodi wanachimba dhahabu? meremeta iko wapi?
 
eh!! Hii kali...., hyo migodi ya dhahabu ya jeshi iko wapi? Wanachimba kina nani? Hebu tuelezee ww unayefaham mambo...
 
Meremeta huijui wewe walikuwa wanachimba kina nani?
 
mm hata siujui huo mgodi wa meremeta..., uko wapi? Nani walikua/wanachimba hyo dhahabu? Unamilikiwa na nani?
 
Meremeta ulikuwa mgodi unaonilikiwa na jwtz ambao ulileta kasheshe bungeni na kuundiwa tume.
Malipo ya dola milioni 132 (wastani wa Sh205.9 bilioni kwa viwango cha sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1,560 dhidi ya Dola ya Marekani) ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Ned Bank ya Afrika Kusini ikiwa ni malipo ya mkopo wa Dola 10 milioni, uliokuwa umechukuliwa na Kampuni ya Meremeta Ltd, wALIKUWA WANASEMA KWAAJILI YA MRADI WA NYUMBU ANAYEJUA ZAIDI ATAONGEZEA.
 
Kama jeshi itatoa pesa kwenye miradi yake poa lakini kama wanataka kupewa pesa kutoka serikalini hapana!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom