Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,399
- 40,295
Kumekuwa na matangazo mengi ya kutafuta wenza/wachumba siku za karibuni kupitia majukwaa mbalimbali. Sifa zinazoainishwa kwa muhitaji, mojawapo ni kipengele cha kazi; atasema anataka mwenza aliyejiajiri au aliyeajiriwa.
Kwa mtazamo wangu, katika mazingira hayo, mi naona muhitaji anayetafuta mwenza anaitaji mwenza wa kumuhudumia kiuchumi au wa kumsaidia kiuchumi; kwa sababu mapenzi asilia, au ya kweli hayaangalii muonekano wa mtu, wala kazi ya mtu, bali yanatokea tu kutoka moyoni (kunakuwa na msukumo) wa kumpenda mtu fulani.
Lakini nyakati hizi, pesa ndio imekuwa kivutio namba moja kwenye mapenzi na hatimaye kuleta mapenzi feki. Unakuta mtu yupo kwenye mahusiano, na wakati huo huo anakuwa na mahusiano mengine nje kutokana na tamaa ya pesa.
Je, mahusiano yako wewe yako katika muundo huo?