Jinsi neno pesa linavyovuruga akili za watu katika mapenzi na ndoa

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Neno pesa limekuwa likitumika vibaya na watu wengi hususani jinsia ya kiume kuyatazama mahusiano, mapenzi na ndoa, kwamba bila pesa hakuna udhati wa mapenzi. Pia neno pesa linatumiwa kuonyesha mwanamke yeyote mbele ya pesa ni kama bidhaa, hawezi kukataa na hata kama X basi akipewa pesa atarudi bila kuhoji.

Watu wameenda mbali na kusema:
1. Nguvu za kiume ni pesa.
2. Mwanaume mwenye kibamia hana pesa.
3. Kupata mwanamke mzuri ni pesa.
4. Mapenzi ya dhati ni pesa.

Huu ni mtazamo unaotazama upande mmoja wa waliyonacho na kiuchumi, lakini uhalisia ukoje?

Mapenzi huwa ni hisia na suala la pesa huwa ni nyenzo ya kurahisisha mahitaji, kwa wanaotazama mapenzi ni pesa ni kundi kubwa lililo na mtazamo kuwa mapenzi ni kugonoka na Ndoa ni kugonoka, hivyo hawana kingine ambacho kinawasukuma kuanzisha mahusiano zaidi ya ngono.

Sio kweli kuwa hakuna matajiri wanaoteseka na mapenzi, waliotendwa, wanaotapeliwa, wanaochunwa, wanaotafuta mitaji kupitia sehemu zao za siri kama madada poa lakini wana watu wanaowapenda kimapenzi tena kwa dhati.

Utajifunza kupitia talaka nyingi zilizotokea kwa matajiri wa nje na ndani ya nchi, wafanyabiashara wakubwa nje na ndani, wasanii wakubwa ndani na nje ya nchi.

Kuna haja ya watu kuacha kuitumia Pesa kama kisingizio cha kukosa mapenzi kumbe:

1. Hujui kutongoza.
2. Hujiongezi katika mapenzi.
3. Unapenda mteremko.
4. Hauko romantiki.
5. Hauishi katika jinsia yako.
6. Umeendekeza ngono kichwani.
7. Kujikweza kupita uwezo wako.
8. Kuweka unyanyasaji wa kijinsia akilini.
9. Uigaji wa maisha na misemo.
10. Ubinafsi.

Maswali matatu ya kujiuliza?

1. Nini lengo la kuanzisha mahusiano ya mapenzi na ndoa?
2. Unaweza kutimiza kila anachohitaji mpenzi wako?
3. Ni pesa au hisia zinazokusukuma kumtamani na mwisho kumpenda mtu?

Jifunze na tafakari: Mara nyingi mahusiano yenye hali ya kawaida au hali mbaya kiuchumi, huwa yanajengwa na umoja, kupeana moyo, kuaminiana na juhudi kubwa ya kutafuta kwa pamoja na ni mara chache kutokea migogoro ya kihisia.

Ila pindi pesa inapopatikana na kuwa siyo tatizo kwa watu hawa, tatizo la hisia huanza, kila mmoja huwaza kutimiziwa haja zake za kihisia na siyo tena kutafuta pesa kuukabili ugumu wa maisha.

Na mmmuhumba
#mnogeshe umpendae#
#imarika katika mahusiano#
#acha uoga wa maisha#
 
Kutongoza ni uamuzi, kuna watu ni saundi mlima hawana hofu na kuna watu wenye pesa hawawez kutongoza. Hujawahi kutana na wajanja wa kuhonga alafu kutongoza hawawezi.
 
Ni kweli mkuu ila nisaidie kuyafundisha haya manyumbu mpaka yaelewe.
 
Neno pesa limekuwa likitumika vibaya na watu wengi hususani jinsia ya kiume kuyatazama mahusiano, mapenzi na ndoa, kwamba bila pesa hakuna udhati wa mapenzi. Pia neno pesa linatumiwa kuonyesha mwanamke yeyote mbele ya pesa ni kama bidhaa, hawezi kukataa na hata kama X basi akipewa pesa atarudi bila kuhoji.

Watu wameenda mbali na kusema:
1. Nguvu za kiume ni pesa.
2. Mwanaume mwenye kibamia hana pesa.
3. Kupata mwanamke mzuri ni pesa.
4. Mapenzi ya dhati ni pesa.

Huu ni mtazamo unaotazama upande mmoja wa waliyonacho na kiuchumi, lakini uhalisia ukoje?

Mapenzi huwa ni hisia na suala la pesa huwa ni nyenzo ya kurahisisha mahitaji, kwa wanaotazama mapenzi ni pesa ni kundi kubwa lililo na mtazamo kuwa mapenzi ni kugonoka na Ndoa ni kugonoka, hivyo hawana kingine ambacho kinawasukuma kuanzisha mahusiano zaidi ya ngono.

Sio kweli kuwa hakuna matajiri wanaoteseka na mapenzi, waliotendwa, wanaotapeliwa, wanaochunwa, wanaotafuta mitaji kupitia sehemu zao za siri kama madada poa lakini wana watu wanaowapenda kimapenzi tena kwa dhati.

Utajifunza kupitia talaka nyingi zilizotokea kwa matajiri wa nje na ndani ya nchi, wafanyabiashara wakubwa nje na ndani, wasanii wakubwa ndani na nje ya nchi.

Kuna haja ya watu kuacha kuitumia Pesa kama kisingizio cha kukosa mapenzi kumbe:

1. Hujui kutongoza.
2. Hujiongezi katika mapenzi.
3. Unapenda mteremko.
4. Hauko romantiki.
5. Hauishi katika jinsia yako.
6. Umeendekeza ngono kichwani.
7. Kujikweza kupita uwezo wako.
8. Kuweka unyanyasaji wa kijinsia akilini.
9. Uigaji wa maisha na misemo.
10. Ubinafsi.

Maswali matatu ya kujiuliza?

1. Nini lengo la kuanzisha mahusiano ya mapenzi na ndoa?
2. Unaweza kutimiza kila anachohitaji mpenzi wako?
3. Ni pesa au hisia zinazokusukuma kumtamani na mwisho kumpenda mtu?

Jifunze na tafakari: Mara nyingi mahusiano yenye hali ya kawaida au hali mbaya kiuchumi, huwa yanajengwa na umoja, kupeana moyo, kuaminiana na juhudi kubwa ya kutafuta kwa pamoja na ni mara chache kutokea migogoro ya kihisia.

Ila pindi pesa inapopatikana na kuwa siyo tatizo kwa watu hawa, tatizo la hisia huanza, kila mmoja huwaza kutimiziwa haja zake za kihisia na siyo tena kutafuta pesa kuukabili ugumu wa maisha.

Na mmmuhumba
#mnogeshe umpendae#
#imarika katika mahusiano#
#acha uoga wa maisha#
vipo vitu vingi sana ambavyo vina thamani zaidi ya pesa ila hauwezi kuviona kama hauna pesa .

kiufupi tafuta pesa
 
Unaweza kuwa na milioni mfukoni na ukashidwa kumtongoza mwanamke umpendaye maana huwezi kumwambia mwanamke eti nina milioni kwa hiyo nimekupenda hilo sahau kutongoza kwanza ndipo issue ya pesa huja.
 
Utadumu vp na mwanamke bila pesa mjini labda huko vijijini watu wanapendana hivyo hivy
Hapo mjini hakuna shamba lakini si unaona watu wana familia zao na maisha yanaendelea Acha kujidanganya eti hawana pesa wanazo ila kipato hakilingani hata wewe kipato chako hakilingani na Mengi au Bakhresa ila hicho kidogo kinakutosha kuishi na mke na familia yako mjini.
 
Back
Top Bottom