Quinton Canosa
JF-Expert Member
- Nov 2, 2012
- 1,228
- 1,264
Habari za mchana wanajamvi,
Kuna hiki kitu binafsi mimi sikipendi japo bado kimekuwa kigumu kutoka kwenye baadhi ya vichwa vya watu.Wiki moja iliyopita jamaa yangu ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Mbeya alitembelewa na binti nyumbani kwao,jamaa akaona isiwe shida ikabidi amtambulishe kwa wanafamilia kama mchumba wake mtarajiwa,cha ajabu baadhi ya ndugu wa mwanaume wakauliza huyo msichana ni kabila gani, jamaa akawajibu ni mchaga wa machame, basi wote wakakaa kimya.
Yule binti alipoondoka tu maneno yakaanza mara oooh ndugu yetu sisi hatutaki uoe mwanamke kutoka uchagani aidha machame,au mpare na makabila yote ya mkoa wa Kilimanjaro,ukawa mjadala mrefu jamaa akaanza kubishana kwamba anaoa anayejisikia yeye ukawa ugomvi mkubwa sana na ndugu wa mwanaume wakaanza wakamwambia likimpata la kumpata asiwashirikishe kwani wao wanajua tabia za makabila haya.
Jamani hii tabia itaisha lini kwani makabila haya yana nini kibaya mpaka kunakuwa na ubaguzi wa aina hii.
Maoni yenu wakuu