Hii tabia tuache jamani, 'ni kabila gani'?

Hii tabia tuache jamani, 'ni kabila gani'?

Bahati mbaya jamii zetu na hata waoaji au waolewaji bado wana uelewa finyu kuhusu ndoa.....

Ndoa ni muunganiko wa watu wawili waliopendana na wakaamua kuishi pamoja....kama mwili mmoja....hapo haisemwi kama ni makabila gani na wala ni watu wa asili gani bali kinachoongelewa ni watu wawili waliopendana kwa kuwa mapenzi hayana mipaka.....
Na vile vile suala la mtu kuoa au kuolewa ni suala binafsi...nikiwa na maana linamhusisha mtu mmoja yeye kama yeye....kitendo cha kumuingilia mtu kwenye maamuzi yake yanayohusu ndoa ni sawa na kitendo cha kuyaingilia maisha ya mtu ingawaje kushauriana na mambo ya kawaida hakuna mkamilifu...lakini ushauri wako usiwe kwa shunikizo la yeye achukue maamuzi......

Kumbuka mtu anayeolewa au kuowa ni wewe na kama ni karaha na raha za ndoa utazipata wewe....changamoto zote za maisha ya ndoa utakumbana nazo wewe.....kwa hiyo kama wewe ndiye muhusika mkuu wa hili swala kwanini watu wengine wakufanyie maamuzi ya wewe kuingia kwenye ndoa....!!!???

Vile vile suala la watu kujadili makabila ni moja kati ya masuala yanayoonyesha ni jinsi gani jamii zetu zilivyo mbali na ustaarabu....
Kwa kawaida ubaya...umalaya, wizi na uchafu mwingine wowote hauna sehemu husika bali ni tabia tu mtu aliyoichukua kutoka kwenye jamii iliyomzunguka.....ni kama vile wadada wa kihaya walivyoamua kuuza miili yao ilihali kuna wadada wengi wa kihaya wenye tabia nzuri na wametulia kwenye ndoa zao....tusimuhukumu mtu kwa kabila lake wala kwa mahali alipotoka wala kwa historia yake bali mtu ahukumiwe kwa matendo kama ambavyo mwingine angeyafanya matendo hayo......

MAISHA NI YAKO , CHAGUO NI LAKO......

Always on point...
 
Hiz ndoa zinasumbua sana watu kwa sasa, mmeamia kwenye makabila sasa,
mkimaliza wachaga,
tuje wahaya alafu
wanyakyusa wafate. . .
 
Hiyo ni muhimu mkuu usichukue. Mimi hapa nikivutiwa na demu machoni na kumuita,baada tu ya salam naulizia mkoa wake wa asili ili nitabiri kabila lake, then namuuliza kabila nikisikia "nshomile" au jamii zao napiga chini na kuanza kuulizia ndizi badala ya gemu.
Kabila la mtu lina-determine maisha na future ya mtu.
 
mwambie awasikilize washauri wapare ni mto wa kuotea mbali
 
Mbona nimewahi kusikia wanawake wa huko mbeya ndio hatari? Nway haya mambo ya ukabila siyo issue kwa sasa.mfano Mimi baba na mama ni makabila tofauti tena na Mimi nimekuja kuowa mwanamke kabila lake tofauti kabisa kwa mamake na babake hivi unadhani watoto wetu watakuja kujuwa masuala ya ukabila? Oaneni kuuwa ukabila. Nyerere hakuwa mjinga alipoamuwa kutuchanganya watanzania.
 
Muhaya, mmachame, mrangi, mpare, mwanamke wa Tanga. Wala sitothubutu kuoa. Hawa wengine ni wa kuoana wao kwa wao.
 
nasikia wanawake wakichaga huwa wanakamchezo ka kuua mume especialy mkiwa mmechuma hela to the maxmum and na watoto wa kurithi tayar wapo ndani, nliskia tu wakuu msije anza kuninyea
Hizo ni stori za miaka ile na hata kama bado wapo basi ni 1 katika 10
 
Mnachekesha kweli: ingekuwa wanawake wa Kilimanjaro wanaua wanaume zao wakishapata mafanikio basi wengi wangekuwa marehemu sasa akina Mkapa, Chenge, Wenje na wengineo. Kama ukiongelea makabila yenye wanawake wanaoua wanaume wakishapata mafanikio au watoto wao wakiwa wakubwa usiwaache WASUKUMA
 
Ukabila umepelekea wasichana wengi kupoteza wachumba wao wakati mwingine kukosa wa kua nao tena wazazi acheni kuangalia makabila...mnaumiza wasichana wa watu...
 
Mbona nimewahi kusikia wanawake wa huko mbeya ndio hatari? Nway haya mambo ya ukabila siyo issue kwa sasa.mfano Mimi baba na mama ni makabila tofauti tena na Mimi nimekuja kuowa mwanamke kabila lake tofauti kabisa kwa mamake na babake hivi unadhani watoto wetu watakuja kujuwa masuala ya ukabila? Oaneni kuuwa ukabila. Nyerere hakuwa mjinga alipoamuwa kutuchanganya watanzania.
Lakini kumbuka Nyerere hakuoa kabila tofauti na lake
 
Ukabila hauna nafasi ktk mapenzi ya siku hizi! Afanye aonalo ni jema machoni pake!
 
Wenyewe ndo Wa kwanza kufichua hiyo siri kama cwao makabila engine yasingejua
 
Wachaga wakiolewa na kabila tofauti na wao huwa ni shida, walio wengi huwa wanamfanya mwanaumwe aonekane choo
 
Back
Top Bottom