Wanazunguka na chombo kuomba vinywaji!!! Naona jambo la ajabu na geni kweli kwangu... sijui ni kwavile siendagi hizo sehemu (kumbi) za starehe au vipi ila sikatai maana...
Kuna katabia kanakofanania na hako tunakutana nako sana migahawani kwa mama lishe hasa hasa mikoa ya ukanda wa pwani
Wamama/wadada wanaouza vyakula wakiona umeenda mteja ambae ni kijana aisee utajuta! Maana mtu anakupimia (anakuuzia) chakula halafu anakwambia yeye ana njaa ikiwezekana umnunulie na yeye chakula
Haitoshi unamuagiza kinywaji (maana mara nyingi ukienda mgahawani basi huduma zingine nyingi kama siyo zote wanakufanikishia wao- mamalishe) basi na yeye anadai kinywaji au chenji ya kinywaji
Haishii hapo bado wakati wa kuondoka unalipia msosi anakupa chenchi lakini huku anakushawishi usamehe jero akapate maji baridi duh!!!


Halafu tabia hiyo naona imeshamiri hasa kwenye migahawa yenye wahudumu zaidi ya mmoja. Unakuta mama mtu mzima (mara nyingi ndiye boss mmiliki wa biashara) halafu kunakuwa na binti au wadada na hao ndo wenye tabia ya kuomba omba sasa sijui hawalipwi vizuri na boss wao
Tena mara nyingi wanafanya hayo kimya kimya yule mama mtu mzima (boss) asisikie wala kuelewa kinachoendelea