Hii tabia Musoma inakera sana

School face

JF-Expert Member
Sep 12, 2019
247
406
Habari wana JF,

Moja kwa moja niende kwenye mada.

Kumekuwa na tabia ya ajabu sana na ya kusikitisha sana hasa kwenye kumbi mbalimbali za starehe yaani ukiingia kwenye kumbi nyingi za starehe hapa Mjini Musoma Kuna kuwa na vijana wengi sana wa kike na wakiume.

Lakini jambo linalo nisikitisha nikua vijana hawa hasa wakiume wamekua ombaomba wakiwa kwenye kumbi hizo za starehe tena kazi yao ni kuzunguka na cup wakikufikia kwako wanasogea karibu na kukuambia uwawekee kinywaji kidogo haijalishi ni kinywaji gani unatumia yeye ili mladi aonekane anakunywa na kinachoniudhi zaidi ni pale anapokuja mmoja akikuomba ukimuwekea kidogo tu anaenda kuwaambia wenzake nao wanakuja kukuomba na ukisha mpa mmoja basi jua kuanzia siku hiyo wewe ni rafiki yake wa karibu sana kila unapokuwa unaenda akikuona tu anakufuata na kukubembeleza umnunulie kinywaji au umuwekee kidogo kwakwel hii tabia imekuwa ikinikwaza sana wanapokuona umeingia wanakuja na kuanza kukusumbua.
 
Ndio hapo hapo amepaongelea mleta mada, kuna mmoja alikuja na glasi kuniomba nimpunguzie K Vant ambayo mi nilikuwa napiga tarumbeta, ikabidi nimnunulie.......basi alihangaika ukumbi mzima kunitafutia mtoto mkali wa kwenda kumgegeda
Haha Haha, nimeenda mara kadhaa pale nikiwa musoma ila sijawahi katana na iyo adha. Au labda kwakuwa mm nasimamaga kaunta tuu.
 
Attention seekers mna shida sana....

Ni nchi nzima ya Tanzania ipo hivyo sababu ya umasikini uliotopea...hii kujifaragua ni Musoma tu ni namna fulani ku-undermine eneo na watu wake

Nchi nzima ni ombaomba...usibague!
Tanga, Moro, Dar, Mbeya na Mwanza sijaiona hii tabia.
Hii ndio mikoa nimeingia kwenye kumbi za starehe bila kukutana na hao ombaomba wa vinywaji.
 
Attention seekers mna shida sana....

Ni nchi nzima ya Tanzania ipo hivyo sababu ya umasikini uliotopea...hii kujifaragua ni Musoma tu ni namna fulani ku-undermine eneo na watu wake

Nchi nzima ni ombaomba...usibague!
Acha ujinga wewe. Eti nchi nzima ya Tanzania ndo ilivyo!! Wewe unaendaga sehem za starehe kweli?

Yaani uende club ukasumbue kuomba omba pombe wanaume wenzako eti ndo utanzania ulivyo?? Acha wanaokosea wakosolewe, shwaini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom