Hii tabia inanikera sana

presider

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
1,027
1,273
Kuna tabia imeshamiri sana makanisani siku hizi, hasa haya makanisa ya 'kisasa'. Tabia ya matumizi ya simu nyakati za Ibada. It's either wakati wa sifa, kuabudu au hata neno unakuta vijana kwa wazee wamekazana na simu zao kurecord na wakati mwingine kuingia 'live' kwenye social networks.

Najiuliza tunaenda kanisani kuzungumza na Mungu au kuwaonesha watu kuwa huwa tunaenda kanisani?

Ni Mungu yupi huyo tunaemwendea kwa kuwa busy na smartphones zetu nyakati za kuzungumza nae? Mbona haya mambo hatuyaoni kwa Waislamu? Au wao hawana smartphones? Mbona makanisa kama Catholic, Lutheran na yanayofanana na hayo hatuyaoni hayo mambo? Au wao wakiingia kanisani wanaacha simu mlangoni?

Kuna haja kubwa sana hili suala kupigiwa kelele hasa na viongozi wa makanisa hayo, kiukweli tunamkosea sana Mungu na linakera sana.

NDUGU ZANGU WAKRISTO TUSIRUHUSU UTANDAWAZI KUTUWEKA MBALI NA MUNGU WETU...
 
mimi nakereka zaidi
unakuta wakati wa neno mtu anatoa simu anafungua biblia ya kwenye simu au wakati wa sifa anafungua tenzi kwenye simu,aisee napataga hasira sana
kuna ugumu gani wa kununua tu biblia yako na kwenda kanisani na ajabu kubwa ni kua imekua kama jambo la kawaida tu mashemasi wala wazee wa kanisa hawakatazi jambo ili,..
so sad
 
Usikereke mkuu tunakimbizana na teknolojia, mimi ni mmojawapo hapa umenigusa lakini sijaona shida ilipo huwa naweka flight mode chochote hakileti distraction.

Na nikiri nimekuwa msaada sana kwani naokoa mda sana pale tukiambiwa funua wakorintho 6, fasta wakati wengine wanahangaika na hardcopy, kamwe sijawahi kumkera mtu au simu ikawa kikwazo ibadani.

unaweza kua upo sahihi kwa namna yako ila kwa sisi wengine mnatupa makwazo,
na sio wote mnoweka flight mode wengine tunawaona kabisa wanasoma biblia na kuchart..aisee
 
Kabla ya biblia za karatasi kulikua na magombo, ambayo yalikuwa kama magamba ya miti yaliyoandikwa neno. But with the printing technology kukawepo na hizo biblia tulizo nazo leo. Kama watumia magombo wangekuwa na mindset kama yako sijui hata kama ungekuwa na hiyo bible ya karatasi.

You don't fight technology, you embrace it. Mtu kutumia biblia ya kwenye simu wewe kinakuuma nini hasa?, issue sio hiyo biblia, issue ni neno. Hakuna maelekezo yoyote kwenye bible yanayosema muonekana wa bible unatakiwa uwe je.

With the advancement of technology itafika kipindi tutatumia chips kwenye brain zenye bible. So you don't need to open anything, the whole bible inakuwa kwenye brain ni kurefer tu.
 
Tunatumia simu kusoma biblia,tenzi za rohoni nk.
Acha kuishi dunia ya kale.
 
Mimi napinga kabisa matumizi ya simu kanisani ilo moja, pili ao wachungaji hawawezi kukemea hayo coz kuna promotion hapo watajuaje kama ilo kanisa lina upako binafsi sipendi hichi kitendo
 
Kanisani kwetu kkkt ukishika tu simu huruhusiwi kabisa hayo makanisa ya kisasa hongera zao
 
Kuna tabia imeshamiri sana makanisani siku hizi, hasa haya makanisa ya 'kisasa'. Tabia ya matumizi ya simu nyakati za Ibada. It's either wakati wa sifa, kuabudu au hata neno unakuta vijana kwa wazee wamekazana na simu zao kurecord na wakati mwingine kuingia 'live' kwenye social networks.

Najiuliza tunaenda kanisani kuzungumza na Mungu au kuwaonesha watu kuwa huwa tunaenda kanisani?

Ni Mungu yupi huyo tunaemwendea kwa kuwa busy na smartphones zetu nyakati za kuzungumza nae? Mbona haya mambo hatuyaoni kwa Waislamu? Au wao hawana smartphones? Mbona makanisa kama Catholic, Lutheran na yanayofanana na hayo hatuyaoni hayo mambo? Au wao wakiingia kanisani wanaacha simu mlangoni?

Kuna haja kubwa sana hili suala kupigiwa kelele hasa na viongozi wa makanisa hayo, kiukweli tunamkosea sana Mungu na linakera sana.

NDUGU ZANGU WAKRISTO TUSIRUHUSU UTANDAWAZI KUTUWEKA MBALI NA MUNGU WETU...
hayo makanisa ni new software.nenda roma au kkkt kama utakuta
 
Kereka na yule ambaye haiweki flight mode halafu ghafula katikati ya mahubiri anapigiwa. Halafu anatoka nje kwenda sikiliza mambo ya mtaani. Je, huyu amekuja ibaada au amekuja subirisha muda tu??
Wazo langu ni kuwa, kweli twende na teknolijia lakini tuwe macho isituondoe kw enye uwepo wa Mungu.
 
mimi nakereka zaidi
unakuta wakati wa neno mtu anatoa simu anafungua biblia ya kwenye simu au wakati wa sifa anafungua tenzi kwenye simu,aisee napataga hasira sana
kuna ugumu gani wa kununua tu biblia yako na kwenda kanisani na ajabu kubwa ni kua imekua kama jambo la kawaida tu mashemasi wala wazee wa kanisa hawakatazi jambo ili,..
so sad
Kwan tofauti ipo wapi au karatasi ndo inahitajika? Kama kweli ni kwa matumizi hayo mm sioni tatizo ila kama anatumia simu kwa mambo yaliyo nje ya ibada sawa
 
Back
Top Bottom