Hii speed ya Nape vipi waungwana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii speed ya Nape vipi waungwana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zamwamwa, Feb 15, 2012.

 1. z

  zamwamwa Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu vuvuzela wa CCM hii kasi yake inakwenda wapi? Kaacha kutukanwa sasa kwa sehemu kubwa, anaandikwa na kuripotiwa vizuri na media kwasasa ukilinganisha na mwanzo! Haya yanatokea yenyewe au yanatengenezwa?

  Na kama yanatengenezwa na nani? Maana naamini Nape hana akili hiyooo! Nadhani iko haja ya kuangalia speed ya huyu dogo hasa anapokuwa kimya sana!

  Wameshirikiana na J.........Kitaifa kuwadhibiti kina Eddo na kwa dalili wanafanikiwa na hii nilidhani kama wangeshindwa ingekuwa kete muhimu sana kwa CDM..... Ushindi huu japo ni nusu hivi si salaam njema kwa chama dume cdm... Tafakari
   
 2. T

  T. 2015 CCM Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Moja ya matumizi ya akili kwa watu wasiofikiri, ni kuishi kwa kudhani na kuwadharau wanaofikiri, si tatizo kwa watu waina hiyo kuwa wepesi pia wa kufuata upepo, na kuiga mambo kutokana na mwenendo wa makundi, yaani kuathiriwa na Mob Psychology.

  Zamwamwa wewe ni miongoni mwa watu wa alina hiyo. Unajidhihirisha kwa maandiko yako kuwa kumbe haupo kwa ajili ya kutetea maslahi ya taifa, badala yake watetea chama.

  Nape ni kijana ambaye kwa sehemu kubwa ametetea kwa vitendo mambo muhimu ambayo mara nyingine hata sehemu kubwa ya wanaCCM hata wana Chadema wasingeweza kuyatolea matamko ya aina hiyo, huku wakionesha msimamo wa dhahiri. Nape si Mnafiki, ni mkweli na muwazi wa kutosha, ni kijana anayepambana na Mataikuni, wenye fedha nyingi na mbinu chafu, lakini yeye kwa uwezo mdogo amesimamia anachokiamini, na kukitenda, lazima apongezwe.

  Hongera Nape, usitishike na wapuuzi wenye kubeza yale mema unayoyatenda kwa taifa hili. Uwezo huo umeoneshwa na vijana wengine kama Mnyika J. Zito K. na wengine kama hao, tusiwakatishe tamaa badala yake tuwaunge mkono ili wasaidie harakati za kuongeza kasi ya mafanikio katika taifa letu.
   
 3. z

  zamwamwa Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  T 2015 CCM,
  Aaah hadi wewe wanikejeli ama kweli nyani bwana..... Hivi vuvuzela baada ya kuburudisha anafaida gani? Nilichouluza kimetokea nini mbona kaachwa kunyukwa kila siku kama zamani? Au kachanyamazishwa??? Wabunge walishindwa nini kumtoa wakati walimpania kwa kuingilia posho zao????
   
 4. T

  T. 2015 CCM Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zamwamwa sikukejeli, ninachotaka kuonesha hapa ni kwamba, ukisema ukweli na kuusimamia, daima watakaokunuia mabaya hawataweza furukuta mbele yako, kwani daima Mungu anakuwa pamoja nawe!! ni lazima uone sawa kumwita Nape Vuvuzela, lakini unapomwita Nape Vuvuzela, wewe na wengine wanaofikiri kama wewe waitwaje? kama sio Bangusilo, tena la kizaramo kabisaa!!!

  Nasisitiza tena sina mashaka na uelewa wako, lakin katika hili, naona ni kwa kiasi gani humjui Nape unayemjadili na kumwelezea, badala yake unawajua mafisadi, hasa kwa sababu ya misaada ya kilimbukeni mnayoipokea kutoka kwao. Townsend, wewe ndiyo ushaathiriwa na umangimeza, ule wa kutetea kitu hata kwa makosa na uozo wa dhahili, Nape ni zaidi ya hao wote unaowasifia na kuwaona wanajua kitu.

  Pamoja na mazingira ya matusi, maneno ya kashfa na hata kudharauliwa, bado Nape ameendelea kuonekana ni mpambanaji jasiri, unafiki unaouzungumzia wewe, labda unaonekana kutokana na uwezo wako mdogo wa kuangalia mambo!!
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu T.2015 nadhani mtoa mada amemsifu Nnape in a way aliposema kwamba sasa Nnape anaandikwa vizuri. Nadhani anaandikwa vizuri kwa sababu anafanya vizuri.

  Pili amesema Nnape na JK wanafanikiwa kiwazuia watu fulani ambao wangepitishwa kugombea urais ingekuwa rahisi kwa CDM kushinda: kwa hapa pia anaonyesha Nnape anafanya kitu kizuri kwa chama chake na kuipunguzia CDM nafasi ya ushindi 2015. Ametoa sifa nyingi kwa Nnape (kwa kujua ama kutokujua) kuliko kashfa/matusi ambayo nadhani lilikuwa lengo lake!
   
 6. Mwakiluma

  Mwakiluma Senior Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ...kumbuka EL ana wafuasi wengi sana ndani ya ccm na harakati zozote za kumdhibiti ambazo tayari zimeshafanikifa zitakisabababishia madhara makubwa ccm kwa uamuzi wowote atakaouchukua lowasa...akiamua kuwa kimya wafuasi wake hawatapigia kura ccm...akiamua kuhama atakigawa ccm mara mbili na kugawanya kura za ccm maamuzi yote haya yatasaidia cdm....kuropoka kwa nape ni faida kubwa kwa cdm....kumbuka alianza na spidi ya gamba iliyosaidia sana cdm kule igunga....
   
 7. A

  Ashoboza Kabalim Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siasa ni hisia, hasa, za kiitikadi. Uvumilivu katika siasa za kidemokrasia ndio GAMBA pekee linalostahimili. Kila mawazo binafsi ni sahihi kwa aliyenena; hivyo, si ajabu NAPE, MTATILO, MNYIKA, Dr. MVUNGI kuitwa majina mengi kwa mitamazamo tofauti ya wa waumini wa siasa, kama vile, vuvuzelas, kutokana na kazi zao za uenezi wa vyama vyao, na porojo nyingi ku'campaign vyama vyao.
   
 8. K

  Karata JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Vijana tukiwezeshwa tunaweza!
   
 9. T

  T. 2015 CCM Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haswaaa karata, umenena kweli, vijana tunaweza, hii haihitaji kuwezeshwa. Mifano ipo, ya watu waliofanikiwa bila kutegemea wala kupitia migongo ya watu wengine. Shime tushikamane kwa pamoja tutafika!!
   
 10. T

  T. 2015 CCM Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ashoboza nawe umenena kweli, ingawa si busara kuwa sehemu ya kuzusha au kuelezea mambo juu ya watu fulani bila kuwa na ushahidi. madhara yake ni kujenga jamii inayopenda kuzusha na kuibua hja za uongo bila kufikiria wala kutathmini madhara yake baadae
   
 11. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusiwe wepesi sana kushutuma juu ya ama mtu kununua au kununuliwa manake JF humu humu ndani wanajamvi walitoa maoni na ushauri mwingi juu ya Nape na CCM sasa ni kwa nini tusifikiri kuwa labda Nape kachukua mawazo ya humu ndani na kuyafanyia kazi jambo ambalo linapelekea sasa hata vyombo vya habari kuona utofauti huo?? Tuwe wepesi wa kutoa changamoto na tutumie wepesi huo huo vile vile kuhakikisha kuwa tunatoa pongezi pale ambapo tunaona kuna mabadiliko......... Na huo ndio uungwana
   
 12. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Yaani wewe ndio bure kabisa, mpaka sasa unashindwa kubaini kwamba hana mvuto wowote kisiasa japokuwa ni kijana,hii ni kutokana na sababu zifuzatazo:-
  1. Chama chake sisiemu kinazidi kudidimia kwa sababu inazojitengezea chenyewe, kila kunapokucha sisiemu
  inaelekea shimoni, hivi wewe zumbukuku mpaka sasa huoni hili?
  2. Kushindwa kwake kutoa maamuzi ndio chanzo cha kupoteza umaarufu wake, mfano hivi sasa kimeazimia
  kwao viti maalumu kuwe na ukomo wa vipindi viwili, baada ya kuamua eti wamerudisha tena UWT watoe
  uamuzi kama siyo usaniii ni nini?
  Hivyo huyo NAPE wako kuwa katika chama hiki nae anapoteza umaarufu, angalia katika uchaguzi wa ubunge aligombea Ubungo. akahenyeshwa na wanawake akawa wa tatu kwenye mapendekezo, kuja kwenye uchaguzi mkuu hao waliomhenyesha walitupwa mbali vibaya sana
  Nape ni vuvuzela tu na wala si vinginevyo.
   
 13. z

  zamwamwa Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Blayi wa Mpwapwa,
  Unatia kichefuchefu sasa kwa hoja zako. Hivi nani zumbukuku kati yangu na wewe? Hivi Chama kinachokufa kilitufanya nini Igunga?? Kimetufanya nini Uzini? Sisi tumepeleka wakubwa wote, mkiti,katibu na kadhalika wao wamewaachia vijana tu matokeo CCM 5680, sisi CDM 218!!!!!! Shame !!!!! Ushabiki mwingine huu mpaka unapitiliza na kuacha kuona ukweli unakera!-

   
 14. z

  zamwamwa Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Blayi,
  Fanya utafiti mwanasiasa kijana anayejadiliwa sana kwa sasa'"..........
   
 15. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Igunga pesa billioni 3, nyama za pori ,akina Rage na bastola na matangazo asubuhi ya siku ya kupiga kura kwamaba CDM wamejitowa ndio hizo kura 25,000 kwa 23 za CDM, mbona huyo mteule kafumu kila siku anazomewa? ushindi wa uzini is not determinant huyo mzungu wa unga anaweza kuwazungukia wapiga kura wote na kuwapa each laki moja,mbona ni wachache? Narudia Nape hana mvuto na wewe Zanwana ni mbwiga tu kimtazamo.
   
 16. m

  mharakati JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  EL hana wafuasi wengi..ana makuadi wengi
   
 17. g

  greenstar JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilishawaambieni kuwa NAPE ni JEMBE muhimu sana kupambana na MaFIsaDI,anajua anachokifanya pia anamsimamo kiasi bila kujali kufanyiwa mambo ya kinyama kama waliyofanyiwa watu wengine.Huo ndiyo uzalendo ambao tunahitaji viongozi wapambanaji wasikubali kununuliwa.......Tafakari kwa nini MAFISADI hawamtaki,wameshindwa kumshawishi na vijisenti ambavyo watu wengi hukimbilia kupokea na kunyamaza kupambana.

  NAPE anaweza kuongoza NCHI katika level yoyote pindi atakapo ona anaweza fanya hivyo.....Pia anakubali kukosolewa.....Nakumbuka alifanya mdahalo mgumu kupita yote pale alipopambanishwa na FISADI wa MAHAKAMANI aka MARANDO,JUSSA akawafunika ile mbaya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...