Hii siyo Tanzania niijuayo!

Hii siyo Tanzania niijuayo!

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,646
Reaction score
10,859
Inasikitisha sana!

1. Mtu "anatekwa" Mchana kweupe huku watu wakishangaa mithili ya nyumbu wa Serengeti?

2. Mtu anapiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna hata anayejaribu "kuigiza" kusaidia?

3. Kama sura ya "mtekaji" imeonekana wazi kabisa lakini bado Polisi "wanashindwa" kumkamata, ingekuwaje kama sura yake isiongeonekana?

Inasikitisha sana!

Iko wapi Tanzania ya Nyerere iliyomfanya Mwinyi kujiuzulu Uwaziri wa Mambo ya Ndani kwa makosa yaliyosababishwa na watu wa Wizara yake?

Iko wapi Tanzania ya Kikwete ilyomsulubisha Kamanda Abdallah Zombe kwa kosa la kuwaua wafanyabiashara wa madini?

Iko wapi Tanzania ambayo raia wake waliamini kuwa wapo salama wawapo penye watu nchini mwao?

Iko wapi Tanzania yenye Jeshi la Polisi wenye intelijensia kali inayoweza kufukunyua hata yaliyofanyika sirini?

Iko wapi Tanzania Kisiwa cha amani?

Ni vigumu kuamini kuwa "hayo" yametokea Tanzania!

Pole sana ndugu Deogratius Tarimo!
 
Attachments

  • VIDEO_YA__UTEKAJI__YAWAIBUA_POLISI(144p).mp4
    2.7 MB

Zombies state
 
Siku hizi ulinzi wako ni wewe mwenyewe, watu Wala hawajishughulishi na wewe na ndo kwanza wanakukimbia, hivyo ukiishi chunga mienendo yako kama circle yako ni ya watu wadogo wadogo.
 
Mkuu tuwe wakweli tu hata ingekuwa wewe usingefanya lolote.

Ni watu wachache mno wenye hizo guts za kureact katika mazingira kama hayo.
 
Back
Top Bottom