Hii siyo hekima

Juandeglo

JF-Expert Member
Dec 20, 2014
1,022
2,723
Salamu wakuu,

Imekuwa kawaida watu kufanya sherehe baada ya ndoa kufungwa makanisani. Wengi wetu tumekuwa tukilazimika kuharibu bajeti na akiba zetu ili sherehe iwe kubwa ama kufurahisha wazazi, wakwe, mke, washkaji.

Kuna bwana harusi mmoja baada ya harusi akatuambia kwenye shughuli yake kulikuwa na ugomvi. Akaeleza kuwa, kwa hela aliyokiuanayo yeye alitaka watu 150 mpaka 200. Akatoa kadi wakwe waje 30. Wakwe wakaja 65. Kukatokea mtafaruku, mama mkwe anataka kususia shughuli. Tena akawa anafoka sana.

Nikatafakari nikaona hii si sawa. Tumekuwa tukiongea humu kuwa kama huna fedha fanya jambo unaloweza kumudu. Kama una milioni mbili fanya shughuli ya milion mbili. Hivyohivyo kwa laki tano au tatu. Tunashona suti kwa ukubwa wa kitambaa.

Sasa wewe mzazi, ndugu, rafiki unamsukuma mwenzako kufanya jambo asiloliweza. Kisa tu ama asikupoteze au akufurahishe kwa nini, wapi, kipi, nani?

Badilisha mtanzamo wako kaka, dada, baba, mama. Kila mmoja afanye analolimudu. Mwisho tunaishia kwenye madeni, tena yasiyo na ulazima. Kama huna dusco, fanya sherehe ya kawaida. Ninayo mipango ya mpaka laki 5, nini chaguo lako?

NB: Upande wa bwana harusi ikabidi wasile chakula ili wakwe wale kumfurahisha. Uzuri bibi harusi alikuwa anamwelewa mama yake kwahiyo haikuleta mtafaruku baina yao. Ulimbukeni gani huu? Umaskin mbaya sana!
 
Kuna jamaa alisema kwamba,

marekani: wakialikwa kwenye sherehe watu 100, wanakuja 50-70

Bongo: wakialikwa 100, wanakuja 321
 
Harusi owa mwanamke umeishi nae miaka hata minne kwenda mbele, mbali na hapo mwanamke anayelilia ndoa mapema huyo ni bomu, kama na wewe ni bomu basi waweza Fanya harus faster tu
 
Back
Top Bottom