Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 81
Hii Kitu nilitaka kuipost hapa miezi kadhaa iliyopita sema nikasahau, leo kuna jamaa kanipigia anataka nimtumie dolali za mchango wa harusi ya binamu yake ambaye hata simjui wala sijawahi msikia.
Tuendelee:-
Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.
Watu wanakutana kila wiki mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. Na katika vikao hivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu.
Kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo.
Jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much.
Badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye Elimu na Matibabu.
MJ
====================
Tuendelee:-
Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.
Watu wanakutana kila wiki mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. Na katika vikao hivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu.
Kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo.
Jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much.
Badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye Elimu na Matibabu.
MJ
====================
View attachment 235905
Kwa kweli michango ya harusi, sijui kitchen Party, Bag party, Send off party na kadhalika imekuwa too much. Unakuta mtu unakuwa na kadi za kudai michango hadi zaidi ya kumi kwa wakati moja. Tabu ya nyongeza ni kwamba viwango vinavyotegemewa ni vya juu. Tutafika?
Je, haijafika mahali wanajamii ya Tanzania tukapunguza madoido na gharama za shughuli hizi?
==============
Katika kumbukumbu zangu mimi, Harusi mtu ulikuwa unafanya kwa uwezo wako, unaita marafiki zako na ndugu mnasherekea hicho kilichopo.
Sasa mtu anakuletea Kadi tena ina kiwango na Watu hawakuchangii sababu wanakupenda ni kama wanakukopesha kwamba na wao siku yao ikifika na wewe utachanga.
Michango Inafika mpaka mamilioni ya pesa watu wanakuja wanakunywa na kula wewe na mwenza wako mnaenda kuanza maisha (wengine hata nyumba hamna) na deni la watu kama mia moja waliokuchangia ambao na wewe inabidi uwachangie.
Jamani hivi kuchangia harusi sasa imekuwa lazima?
Nahisi sasa harusi zinatuletea umasikini, yani mtanzania wa kawaida nina kadi tisa mpaka sasa.
Bado natafutwa na jamaa yangu mwingine, yani simu imejaa meseji za watu wanakumbushia michango.
Jamani hatuwezi kuwa na utaratibu mbadala kwenye hili swala? Tupungiziane stress.
Halafu na hii tabia ya mtu anakutumia tu ujumbe uje siku fulani mahala fulani kuna kikao cha harusi, kumbe kesha kuweka kwenye kamati ya harusi we bila kujua afu ukifika wanaweka kiwango cha kila mwanakamati kutoa.
Nadhani tuhitaji mbadala wa hili.
Napata kadi za kuchangia harusi karibu kila mwezi naletewa karibu kadi 3, @50,000 approximately =150 , 000 .
Haya majanga sana ,mshahara wangu 550,000 , which means 30% michango harusi ,Ninaacha haya mambo ,mimi mwenyewe sitafanya hiyo mambo, yaani kila weekend tupo busy kuchangisha harusi.
Kama tunataka kutokomeza umasikini na wakati tunatiana umasikini ,siwezi tena.
Jamani kama huna uwezo usisumbue watu bwana ,funga ndoa ya kawaida tuache mambo ya kuiga.
Ni kawaida kwa jamii yoyote duniani kuoa ama kuolewa na hasa kwa binadamu aliyekamilika. Kimsingi kuoa ni jambo la heri kwa mtu kupata mwenzi. Na ndugu jamaa na marafiki kuchangia kwa mawazo mali na misaada mingine ya kijamii ili kufanikisha shughuli hiyo kukamilika.
Hata hivyo uchangiaji huu umekuwa wa kiholela mno, kwani waoaji na wanaoolewa ni vyema wakawa na utaratibu mzuri wa kugawa kadi hizo. Nasema hivi kwa sababu kuwa mgawa kadi anapaswa kufanya mawasiliano na mtu anayetaka ampe kadi kwa ajili ya kumchangia mchango huo. badala ya kuzigawa kadi hizo pasipo hiari ya mchangiaji, maana mgaw kadi unashangaa anakuletea kadi, ama anaibwaga mezani kwako kama ni ofisin au anawaachia watoto kama ni nyumbani.
Ombi langu kwa waoaji wote fanyeni mawasiliano kabla ya kugawa kadi maana sasa zimekuwa kero kiasi kwamba ndani ya mwezi mmoja unaweza kugawiwa kadi zisizopungua kumi na wote wantaka mchango usiopungua elfu hamsini. kwa namna hii hatuwezi kwenda kabisa.
Hata hivyo niwaombe watanzaia wenzangu tunahitaji kubadilika ili mitizamo yetu isilenge zaidi katika uchangiaji wa harusi, tunahitaji kuchangia zaidi katika elimu kwani kuna vijana wetu hawana hata dwati la kukalia, yatima, wajane na wenine wengi wenye mahitaji badala ya kuchangia harusi.
Kufanya harusi kubwa katika kumbi kubwa zenye kugharimu mamilion ya shilingi za kazi gani, kwani hazina tija kwa maendeleo ya taifa hili ambalo wananchi wake wako katiak wimbi la umaskini mkubwa.
Sitoi tena Michango ya Harusi
BAADA ya matukio ya harusi ya Jumamosi iliyopita natoa onyo ole wake atakayeniomba mchango wa harusi, sitaki utani. Labda kwanza nikueleze jinsi tulivyopata misukosuko sana kwenye uchangiaji wa ile harusi, maana siku hizi hakuna pa kukimbilia, kila asubuhi unaamshwa saa kumi na mbili na meseji kwenye simu;
"Ndugu, rafiki na jamaa wa familia ya Pingapinga inakukumbusha kuwa harusi ya mtoto wao imekaribia hivyo mchango wako unahitajika", baada ya wiki meseji huwa kali zaidi;"Siku zinaisha kwa nini hautoi mchango, unajua familia ya Pingapinga ina shughuli ya harusi ya mtoto wao, toa upesi au la usitulaumu."
Basi hizi meseji zilikuwa nyingi kuliko zile za kampuni yangu ya simu inayobuni namna ya kunitoa mkwanja kila wiki. Hatimaye nikatoa faini, maana nisiite mchango, maana mchango haulazimishwi.
Sasa Jumamosi ndiyo ikawa siku ya harusi, kadi nililetewa mapema , nikahakikisha koti langu la kuendea harusini nalicheki vizuri, maana haya makoti yanayokaa kabatini miezi ni muhimu kucheki vizuri maana unaweza kukuta panya kazalia kwenye mfuko halafu wakatimka kutoka kwenye makazi yao wakati uko katikati ya kucheza mduara wa harusi.
Kweli tukaingia ukumbini viti vilikuweko swafi, meza zimepambwa kwa maua na MC alitukaribisha kwa maneno mengi yaliyojaa vichekesho visivyochekesha, au vichekesho vingine vimesharudiwa na kila MC hapa mjini halafu akawa analazimisha watu wapige vigelegele!
Yote bure watu walikuwa wamenuna maana hakukuwepo na dalili ya hata chupa moja ya kinywaji, ila ahadi kibao zikawa zinatolewa na MC, mara ‘Roli la bia linakuja toka breweries, mara shampeni leo inatoka Ufaransa kwa helikopta."
Ghafla wahudumu waliovalia vikofia kichwani wakapitisha sambusa mojamoja na kinywaji round moja kwa kila mtu, wakisindikizwa na MC akituhamasisha tule tufurahi na bwana harusi. Kwa kweli hela yangu ikaanza kuniuma, kwanza nililazimishwa kulipa, halafu sioni chochote hawa jamaa vipi?
Wakati ukumbi mzima ukiwa umeendelea kununa utadhani kikao cha msiba, MC akatuambia eti bwana harusi ana machache kabla ya kutuaga kwenda kupumzika na mkewe. Pamoja na kisirani tulikuwa na hamu kumsikia mshenzi huyu anataka kusema nini.
Bwana harusi akasimama hata suti aliyovaa ilikuwa haijamkaa sawasawa, akakohoa kidogo akaanza, "Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu, kiukweli hapa nimepata mke mtulivu, mpole asiye na makeke, yaani najisikia nina bahati sana.
"Naomba niwashukuru wakwe zangu kwa kukubali kupokea robo tu ya mahari na kuruhusu ndoa hii ifanyike. Pia nishukuru kwa zawadi zao za kitanda, godoro, kabati na makochi asante sana.
"Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii, pia wafanyakazi wenzangu kwa zawadi yenu ya jiko la gesi. Namshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.
"Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama waliopika sambusa hizi tulizokula kwa kweli zilikuwa tamu sana, kwa kweli leo ni furaha tupu. "MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali kuwa mc wa shughuli hiikwakweli upo vizuri, aksante sanaaaaa!
Yaani inamaanisha ela zetu za mchango sijui zilinunua nini maana kila kitu almost kilikuwa bure.. mnaoowa karibuni poleni msinihesabu.
Ni kipindi kingine cha mwaka ambapo kila mwisho wa mwaka kadi za michango ya harusi inakuwa mingi, inakuaje mtu anataka kufanya sherehe kubwa na hana uwezo?
Kwanini usifanye hiyo harusi kutokana na uwezo wako ulionao, ni mpaka usumbue watu wakuchangie?
Tena kinachoudhi ni mtu ameshakaa na mke/mme na wana watoto anataka kupasha kiporo chake nae anataka afanye sherehe kubwa na anachangisha!!
Na kero nyingine mtu anakupa kadi ya mchango wa ndugu yake ambaye humjui.
Sijawahi kupewa au kuona mtu akichangisha kwa ajili ya maendeleo kama vile ada ya shule etc kama majirani zetu na harambee zao zenye maendeleo, sijui wenzangu mnafikiria vipi.
Moja ya kero kubwa na ambayo kwa mtizamo wangu inaweza kuwa kikwazo kwa wananchi wa kawaida kuendana na kaulimbiu ya hapa kazi tu, ni namna tunavyoendesha sherehe mbalimbali za kijamii, kama vile harusi, send-off party, kitchern party na sasa imeongezeka sherehe zingine kama ubatizo, kipaimara, graduation na engagement party.
Raia maskini hulazimika kuchanga pesa nyingi na wengi hulazimika kuingia kwenye mikopo ambayo huwatesa mno, mtu hulazimika kuchangia hata kama hana pesa kwa kuogopa kutengwa na jamii.
Tatizo la pili ni muda ambao sherehe hufanyika. Nyingi huisha usiku sana, "sherehe inaisha saa saba usiku au saa nane, unafika nyumbani saa tisa usiku, kupata usingizi saa kumi alfajiri, asubuhi unatakiwa uwepo kazini saa moja asubuhi. Hivi hapo ufanisi utakuwepo kweli?"
Tatizo la tatu ni siku za sherehe, ukiondoa harusi, sehemu kubwa ya sherehe zilizobakia hufanyika katikati ya wiki, jambo ambalo hupunguza kwa kiasi kikubwa utendaji kazini na wakati fulani huathiri mahudhurio ya wafanyakazi.
Ili kuendana na kauli mbiu ya hapa kazi tu, napendekeza wizara inayohusika na ustawi wa jamii ifanye yafuatayo;
- Ipige marufuku michango yote ya sherehe, na atakayechangisha aadhibiwe vikali
- Sherehe zote zifanyike weekend au siku za mapumziko
- Mwisho wa sherehe zote uwe saa kumi na mbili jioni, adhabu kali itolewe kwa atakayezidisha muda
Familia ziendeshe sherehe kwa gharama zao wenyewe, wasiruhusiwe kuchangisha kwa mtu asiye mwana familia, nchi nyingine kama Zambia wameweza, kwanini sisi tushindwe. Kama nawe unakerwa na jambo hili, toa pendekezo, huenda wahusika nao wakapitia uzi huu.
Alamski!