Hii si Tanzania salama tena:

Hii si Tanzania salama tena:

Eberi Manya

Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
35
Reaction score
41
Hii si Tanzania salama tena pa kuishi,
Damu iliyomwagika Kinondoni haitawaacha salama wauaji na mawakala wao waliowatuma.

Uvumilivu kwa Tanzania sasa inaelekea mwisho,, ubaguzi sasa baina ya makabila na vyama ni dhahiri.

Ni nani aliyewaambieni ninyi tume ya uchaguzi na mkurugenzi wa Kinondoni kuwa wenye haki ya kupewa hati ya viapo ni CCM tu?? Kwani vyama vingine havina haki hiyo?? Mbona sheria iko wazi??

Kwanini mnatumia ubaguzi huo waziwazi?? Kwanini mnaleta machafuko na kuondoa amani katika nchi hii?? Kwa mauaji haya yaliyotokea na kuua na kujeruhi watu, nani yupo salama??

Kwanini tume ya uchaguzi na wakurugenzi/wasimamizi wa uchaguzi mnavuruga uchaguzi?? Uchaguzi huu mnavuruga kwa maslahi ya nani??
Damu hiyo iliyomwagika haitawaacha salama hakika,,mtadaiwa juu yenu wenyewe na vizazi vyenu.

Na ninyi polisi,,miguu yenu na mikono yenu imejaa damu, wote mliohusika katika kuwapiga watu wasiokuwa na hatia, damu hiyo itadaiwa mikononi mwenu na juu ya familia na vizazi vyenu.

Mungu na awalipizie maradufu kwa damu hiyo mliyoimwaga isiyokuwa na hatia,,
Mungu na awalaani wote mliohusika katika kuua na kumwaga damu isiyokuwa na hatia,,,hamtabaki salama hakika daima,,,,.
 
Nashindwa kuelewa kwanini Mkurugenzi amechelewesha kutoa fomu hadi watu waandamane? Kuna nini nyuma ya hiki kitendo? Hivi angetoa fomu kwa wakati haya yangetokea? Watanzania tusipotoshwe hata kidogo inawezekana huyu bwana kapewa maelekezo kutoka juu na ndo maana mamlaka yake ya uteuzi imejifanya hata haijaona hiyo tatizo. Wameona bora wamwage damu za Watanzania ili tu ccm ishinde hilo jimbo. Ni watanzania wasiojielewa tu huweza kuwapigia kura ccm na wale wanaonufaika moja kwa moja. Pengine wamelenga kuwaumiza mawakala wa Chadema na wengine wakamatwe ili kesho wasiwepo vituoni. Chadema mjipange kukabili hilo, isije kuwa mtego kwenu.
 
Ukiskia Ngoma inavuma sana ujue inakaribia kupasuka.
Time will tell

Sisi mi waoga, hakunacha ngoma kupasuka wala nini. Ccm wameshajua wanatawala nchi ya waoga na ndio maana wanafanya watakalo. Na wataendelea kutawala miaka nenda rudi labda mungu aamue mwenyew ila kwa uoga wetu huu hawatoki ng'oo.
 
Kuna video nimeitizama polisi wakipiga na kudhalilisha wananchi huko Kinondoni, imenisikitisha sana!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mtu akikaidi amri halali na apigwe tu.
Acheni kutetea uvunjivu wa amani. Fikiria kama nchi haitakuwa na utaratibu wa kuzuia watu kuandamana, kuna watu wengine wana vikundi vya vibaka watasingizia wanaandamana kumbe ni wezi.

Halafu jiulize unaowatetea wanapata faida gani kuandamana zaidi ya hasara, hapo kiongozi wao mbowe alikimbilia wapi badala ya kuwatetea watu wake?

Mamlaka lazimwa iheshimiwe mkuu
 
Back
Top Bottom